Tafuta

2020.05.22 MTAKATIFU RITA WA CASCIA 2020.05.22 MTAKATIFU RITA WA CASCIA 

Papa awashukuru wamonaki wa Cascia kwa zawadi ya mawaridi ya Mtakatifu Rita!

Katika barua ya Papa Francisko kwa Jumuiya ya watawa wa Cascia na mapadre wa Mtakatifu Agostino,anaonesha shukrani zake kwa kupokea zawadi ya mawaridi ya Mtakatifu Rita mahali ambapo watawa hao wa Mtakatifu Agostini wamemfikishia mara baada ya baraka siku ya kumbu kumbu ya Mtakatifu wa maombezi ya mambo yasiyowezekana.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko amewashukuru wamonaki wote kike na kiume wa Mtakatifu Agostino katika Monasteri ya Mtakatifu Rita wa Cascia kutoka na mawaridi matano yaliyobarikiwa tarehe 22 Mei na kumtumia  Papa kama msimamiz wa Kanisa Katoliki katika mabara yote.  Katika taarifa iliyowafikia jumuiya ya watawa hao Jumatano iliyopita, Papa amewaandikia barua na kuwaeleza jinsi ambavyo maua hayo aliyaweka chini ya miguu ya Maria ili kwa maombezi  Bikira na Mtakatifu wa miujiza ya mambo yasiyowezekana waweze kutumiza mapenzi ya Mungu kwa kile ambacho hakiwezekani.

Yesu ndiye tumaini pekee katika wakati wa majaribu

Papa Francisko katika barua yake ya kushukuru anabainisha kuwa “katika kipindi hiki cha janga (…) Yesu ndiye tumaini pekee kwa uaminifu wake. Hatupaswi kujiachia katika mateso na wala katika kifo, bali ni kujikita katika safari kwa ajili ya kujenga wakati ujao ambao Mungu anataka kutimiza kwa ajili ya watoto wake wote”. Watawa wa ndani wa Cascia wamepokea barua hiyo ya Papa Francisko kwa furaha kubwa. Kwa mujibu wa Makamu Mama Mkuu wa Jumuiya hiyo Sr. Natalina Todeschini amesema, “ wazo lake limetufurahisha, maneno yake yametuonesha umakini wake na ukaribu mbele yetu. Sikuwahi kufikiria kwamba tendo la kutuma mawaridi yaliyo barikiwa ya Cascia katika Siku ya Mtakatifu Rita yangeweza kupendwa hata na Papa”.

Mawaridi yaliyobarikiwa ya Mtakatifu Rita kwa Papa na Italia nzima

Kutokana na dharura ya kiafya iliyotokana na virusi vya corona, au covid-19 siku kuu ya Mtakatifu Rita imeandaliwa kufuatana na kanuni zote zilizowekwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi zaidi, na kwa maana hiyo katika madhabau huko Cascia hawakuweza kupokea maelfu na maelfu ya waamini ambao hufika kwa kawaida na utamaduni kila mwaka tarehe 22 Mei ili kuadhimisha liturujia hiyo ya Mtakatifu wa kiagostino.

Mawaridi yametumwa hata kwa viongozi wengine

Ili kuweza kuwafikia hata  kwa mawazo yao mahujaji wote duniani, mawazo ya watawa wa kike na kiume wameamua kufanya ishara kama hiyo ya kutuma mawaridi ya Mtakatifu Rita yaliyobarikiwa katika siku kuu katika sehemu mbali mbali kama vile , mawaridi( 5) kwa Papa, mawaridi (20) kwa wakuu wa mikoa ya  Italia kama kuwakilisha mikoa ya nchi, Waridi (1) kwa Baraza la Maaskofu Italia, mawaridi (16) kwa Marais wa Mabaraza ya Maskofu kikanda, waridi (1) kwa Rais Sergio  Matarella wa Italia, waridi moja kwa Waziri Mkuu wa Italia Bwana  Giuseppe Contena, na  waridi (1) kwa Meya wa mji wa Cascia.

Cascia ni 'Oasi' ya amani

Papa Francisko ambaye kwa ukaribu wa ishara na shukrani zake kutokana na sala zao kwa ajili ya huduma yake ya kipapa amewatumia hata baraka Jumuiya hii ya wamonaki wa kike na mapadre wa Mtakatifu Agostino, aidha hata kwa watoto ambao wanaishi karibu na  jengo la Monasteri hiyo ambao wanatoka  katika familia zenye matatizo. Na hatimaye ni matarajio ya Papa kwamba mahujaji wanaweza kurudi mapema iwezekanavyo huko Cascia ambayo ameiita kuwa 'Oasi' yaani chemi chemi ya amani  na ili  wote wenye kusongwa na matatizo waweze kupata mwanga na  njia mpya za kufuata ukweli ambao unafanya kuwa huru.

Shukrani kutoka wa Rais Mattarella na Waziri Mkuu Conte

Hata hivyo kufuatia na ishara hiyo ya mawaridi kwa viongozi wa serikali, Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella naye amependa kuwashukuru kwa kuwatumia barua iliyoandikwa kwa mkono wake kwa wamonaki wa Cascia kutokana na kupokea mawaridi yaliyo barikiwa. Katika maneno yake anamesema “ sherehe za Mtakatifu zimesindikiza kwa namna ya pekee katika ufunguzi wa Italia na nitumaini langu kuendelea kuisindikiza kwa wa ulinzi wake”. Naye Waziri Mkuu  Giuseppe Conte, mawazo yake kwa wanashirika wa Agostiniani amesema “sala zenu katika kipindi nyeti kwa ajili ya maisha ya Nchi, yananipa nguvu binafsi na  yanatia nguvu shughuli zote za serikali kufanya kazi kwa ajili ya wema wa pamoja”.

14 June 2020, 09:00