Tafuta

2020.06.09 Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano 2020.06.09 Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano 

Roma:Papa aunda mfuko kwa wafanyakazi wenye shida kufuatia na Covid-19!

Mfuko utaitwao “Yesu Mungu Mfanyakazi” na ambao utaanza na euro milioni moja kwa ajili ya watu wenye shida kufuatia na matokeo ya janga la covid-19 katika mji wa Roma.Katika Barua aliyomwandikia Kardinali De Donatis,makamu wake,Papa amezindua mshikamano uitwao “Agano la Roma” huku akiomba Taasisi na raia wote wa Roma kuwa wafanye kuzaliwa mji kwa upya kwa njia ya moyo wa mshikamano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hakuna njia nyingine kwa Papa Francesco, ambaye kwa siku chache zilizopita katika kuanzisha Tume ya baada ya Covid alikuwa ameonesha wasiwasi wake juu ya matokeo ya kijamii ya janga hilo. Mtazamo wake umejikita wakati huu kwenye mji ambao yeye kama Askofu, Roma anathibitisha “tunaona kuwa watu wengi wanaomba msaada, na inaonekana kwamba 'mikate mitano na samaki wawili' haitoshi”. Ni Ufufuko wa Roma ambao unaanzia kwa wadhaifu. Ni kuwarudishia hadhi walio katika hatari ya kutoonekana chini ya vizingiti vya umakini, hadhi ambayo wiki za karantini  zimepunguzwa kama vumbi na wepesi wa masaa.

Kutokana na hili unazaliwa mtindo  mpya wa dhati wa Papa, ambao umejionesha katika barua yake aliyoituma kwa makamu wake wa Roma Kardinali, Angelo De Donatis.  Huu ni mfuko mpya uliopewa jina “Yesu Mungu mfanyakazi” ambao utakuwa na kiasi cha kuanzia euro milioni moja zilizowekwa katika mfuko wa Caritas ya Roma na ambazo kama anavyoandika zinataka kukumbusha hadhi ya kazi kwa kundi kubwa la kila aina ya wafanyakazi wa kila siku na wa kawaida, wale walio na mikataba ya muda, yani isiyosasishwa, wale wanaolipwa kwa saa, na kwa mawazo yake  Papa Francisko anaorodhesha aina hizo za wafanyakazi kama vile: wafanya mazoezi, wafanyakazi wa ndani, wajasiriamali wadogo, wafanyakazi wa kujiajiri, hasa walio katika sekta ya walioathirika zaidi na shughuli zao zilizoachwa.  Kati yao, amesema, “wengi ni baba na mama wa familia ambao kwa shida wanapambana ili kuweza kuandaa mezani ya watoto wao na kuwahakikishia mahitaji yaliyo msingi”. “Ninapenda kufikiria kuwa inawezekana kuwa fursa ya muungano wa kweli kwa ajili ya  Roma ambayo kila mtu, kwa upande wake, anahisi kuwa mhusika mkuu wa kuzaliwa upya katika  jamuiya yetu baada ya mgogoro”.

Papa Francisko hata hivyo anajua kuzungumza kwa lugha ya ubinadamu. Katika hili anaonesha na anatambua idadi kubwa ya watu ambao katika siku hizi wamejifunga kibwewe ili kusaidia na kuwatunza walio wadhaifu. Amejaribu kubainisha juu ya kuongezeka kwa ufadhili, kwa wale ambao wanasaidia wagonjwa na maskini, na kwa ujumla “zile ishala ambao zilionekana kwa waroma wakichungulia madirishani huku wakiwapongeza madaktari na wahudumu wa afya, wakiimba na kupiga vyombo mbali mbali kwa shangwe na kuunda jumuiya kwa namna ya kuvunja ule upweke ambao ulikuwa unazidi kusonga mioyo ya wengi kati yetu” ameandika. “Ni mifano isiyo ya hisia rahisi tu, lakini ya watu ambao wanataka kutenda kwa ajili ya faida ya wote”.

Uundaji wa Mfuko kwa ajili ya Papa Francisko ni hatua muhimu  ya Kanisa ambalo linatembea na linatambua wazi na kushirikishana wasi wasi wa yule ambaye leo hii hana uhakika. Ni Kanisa ambalo linasindikiza kiukweli na upendo wake kwa wadhaifu na kuwa tayari kushirikishana na taasisi za umma na hali halisi ya kijamii na kiuchumi. Kwa upande huo ndipo Papa anawageukia moja kwa moja wawakilishi wa vyama vya kijamii vya raia na katika ulimwengu wa kazi “kualikwa kuwa na usikivu wa maombi haya na kuyabadili katika siasa na matendo ya kweli kwa ajili ya wema wa mji. Aidha papa anaandika kuwa será za kisasa zilinda hasa wale ambao wako hatari ya kubaki wamebaguliwa katika ulinzi wa kitaasisi na ambao wanahitaji msaada wa kuwasindikiza ili waweze kweli kutembea kwa upya kwa kujitigemea.

Ni matarajio ya Papa Francisko kuwa uundaji wa pamoja na mshikamano katika athari za janga, yanaweza kuunda ukweli na mapatano kwa ajili ya Roma ambayo "kila mtu anaweza kuwa sehemu ya ushiriki na kuhisi kuwa mstari wa mbele wa kuzaliwa kwa jumuiya yetu baada ya janga”. Papa Francisko anawahamaisha maadre “wawe wa kwanza kuchangia mfuko huo na wafadhili wa shauku ya ushirikishano katika jumuiya zao”. Hatimaye maombi yake ya mwisho ni kwa moyo mwema wa waroma, kwamba kwa sasa haitoshi kushirikishana tu yale mabaki. “Ningependa kuona mshikamano katika 'mlango wa jirani' ukiongezeka katika jiji letu, vitendo ambavyo vinakumbusha hata mitazamo ya mwaka wa kisabatiko, ambayo madeni yanasamehewa, mabishano yanaondolewa, fedha zinaombwa kulingana na uwezo wa mdaiwa na siyo kwa ajili ya masoko".

Kwa mujibu wa barua ya Kardinali De Donatis kufuatia na kuundwa kwa mfuko huo, anatoa shukrani za kina kwa Papa.  Ambaye anasema haishi kujionesha kwa wanawake na wanaume wa mji wao” Kwa mujibu wake amethibitisha kwamba pamoja na taasisi kuanzia na Mkoa wa Lazio hadi Wilaya ya Roma, kila moja kwa upande wake ,” sote tutajibu pamoja na kwa kujitolea kuunda mshikamano wa kweli kwa ajili ya Roma kuwa wahusika wakuzaliwa upya wa jamuiya yetu baada ya mgogoro’. Kuhusiana na maelezo zaidi ya Mfuko, huo kwa mujibu wa taarifa ya Jimbo Kuu, utawasilishwa kwa vyombo vya habari Ijumaa ijayo saa 5.00  asubuhi, majira ya Ulaya , katika Chumba cha Kardinali Ugo Poletti cha Jumba Kuu la Laterano.

09 June 2020, 13:34