Papa asali kwa ajili ya Brazil waliokumbwa na  janga Papa asali kwa ajili ya Brazil waliokumbwa na janga  

Papa asali kwa ajili ya nchi ya Brazil waliokumbwa na janga!

Tarehe 10 Juni Papa Francisko amempigia Simu Askofu Mkuu Orlando Brandes, wa Aparecida na kumwakikishia sala zake huku akiwaomba watu wote nchini Brazil wamtazame Mama Maria wa Aparecida katika kipindi kigumu cha matatizo ya janga la virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mazungumzo kwa simu ya Papa Francisko na Askofu Mkuu Orlando Brandes wa Aparecida, tarehe 10 Juni 2020, Papa ameonesha upendo, mshikamano na  sala kwa ajili ya watu wa Brazil  pia kuwakumbusha kumtamza Mama Maria wa Aparecida. Ni simu ya Papa ya kuonesha ukaribu wake kwa watu ambao kwa sasa wamejaribiwa na janga la virusi vya corona, ambavyo hadi sasa vimeathiri watu karibia 40,000. Papa Francisko amemweleza Askofu Mkuu kwamba awaeleze watu wa Brazil kuwa si kwamba anasali kwa ajili yao tu, lakini pia anawasindikiza daima kwa moyo. Kwa mujibu wa mahojiano ya Askofu Mkuu ameeleza ni namna gani ya  kuzungumzia juu ya  zawadi kubwa aliyoipata katika kesha la Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Yesu.

Katika simu hiyo kwa mujibu wa Askofu Mkuu Brandes amesema  Papa Francisko amewahikishia sala zake na kuwaomba watu wote wamkabidhi Mama Maria wa Aparecida na ambaye kwake yeye anayo ibada maalum. Picha ya Bikira Maria wa Aparecida kwa dhati ipo hata katika Bustani za Vatican tangu mwaka 2016 na kwa maana hiyo Papa anahisi huo ukaribu.  Katika mazungumzo yao na Askofu Mkuu Brandes, vile vile wamekumbushana uwepo wake Aparecida kunako  2007 wakati wa Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Bara la Amerika ya Kusini na kunako mwaka 2013 wakati wa Siku ya Vijana Duniani huko Rio de Janeiro, ambapo Papa amesema kuwa ziara hiyo alipata nafasi ya kumgusa Mama bikira huyo na hivyo” ninawahimiza wote kujiweka kwenye mikono ya Mama wa Aparecida”.

Katika mazungumzo yao pia katika simu  Papa Francisko amekumbuka hata Mtakatifu Giuseppe Anchieta, Mjesuit aliyetangazwa na Papa mwenyewe kunako mwaka 2014, ambaye kumbu kumbu yake kwa Kanisa inaadhimishwa tarehe 9 Juni. Hatimaye akimsalimia Askofu Mkuu wa Aparecida, amewashauri watu wa Mungu nchini  Brazil wawe na ujasiri na imani  kwamba “ sisi ni watu wa imani” na zaidi amemuhimiza kuwabariki watu wote na kuomba wao wasisahu kusali kwa ajili ya utume wake.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa tangu mwanzo wa janga hili la virusi, Papa Francisko amekwisha waita kwa simu nchini  Brazil, ambapo tarehe 25 Aprili alimpigia simu Askofu Mkuu Leonardo Steiner, wa Jimbo Kuu Manaus, baadaye tarehe 9 Mei akamwita Askofu Mkuu wa Mtakatifu Paulo, Kardinali Odilo Pedro Scherer, kuelezea mshikamano wake. Na kwa njia ya simu kwa mara ya tatu, amefafanua  Askofu Mkuu Brandes  “ Papa wetu amefanya mapigo yake ya moyo kuwa karibu nasi”, hebu tumsindikize kama “ baba mmoja”.

11 June 2020, 14:43