Kufika kwa wahamiaji katika kisiwa cha Malta. Kufika kwa wahamiaji katika kisiwa cha Malta.  

Ziara iliyofutwa ya Papa kwenda Malta:shida,janga,wahamiaji na Utalii!

Mwishoni mwa Mei mwaka huu ilikuwa imeandaliwa ziara ya Papa kwenda katika kisiwa cha Malta.Kufuatia na vizuizi vya kuenea kwa virusi vya corona tukio hilo limefutwa.Katika mahojiano ya Padre Oliver Borg,Mjesuit wa Malta amesisitiza juu ya hali halisi wa Wakatoliki na huduma ya Kanisa kwa ajili ya wakimbizi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kauli mbiu iliyokuwa iongoze ziara ya Papa Francisko tarehe 31 Mei, mwaka huu huko kisiwa cha Malta na Gozo ilikuwa ni “tulitendewa ubinadamu sio wa kawaida”( Mdo 28,2). Maamuzi ya nembo hiyo kulikuwa na ishara zilizokuwa zinaonesha mikono iliyoinuliwa juu ya msalaba, ndani ya  ya meli inayoyumbishwa na mawimbi. Mikono ilikuwa ni ishara ya ukarimu wa wakristo kwa jirani na msaada kwa wale ambao wana matatizo, walioachwa peke yao katika hatima yao. Mtumbwi unaoyumba uliokuwa unaelezea, manusura ya Mtume Paulo katika Kisiwa cha Malta na ukarimu wa watu wa Malta kuelekeza kwa Paulo na manusura wenzake. Padre Olive Borg, mjesuit na ambaye kwa miaka 45 amekuwa ni mmisionari katika nchi za Mashariki na ambaye kwa sasa amerudi katika kisiwa chake cha kuzaliwa Malta, katika mahojiano na Vatican News, aelezea kusikitika kwa watu kufuatia na kufuta ziara hii.

Watu wote walikuwa wanamsubiri Papa Francisko kwa hamu na upendo, amesema Padre Borg.  Wao walikuwa wanatambua ya kuwa moja ya sababu ambayo Papa alitamani kwenda, ilikuwa ni kutaka kuzungumza juu ya hali halisi ya wakimbizi ambao walio wengi wanaishia baharini. Walikuwa na matumaini hasa wao ambao wanashirikiana na Kikundi cha Huduma ya Wakimbizi cha Wakijesuit, kuweza  kuzungumzia hili na kuwafanya watu waweze kuwa na utambuzi wa hali halisi , katika wakati huu wa kihistoria ambo kwa namna ya pekee wanahitaji, kwani serikali yao, inaogopa sana kwa sasa kufika kwa wahamiaji.

Lakini wao hawajasahau kuwa baada ya vita, na kama ilivyojitokeza hata kwa waitalia wao ndiyo walikuwa wahamiaji. Kulikuwa na wahamiaji wengi sana kuelekea Canada, Australia, Uingereza, na Amerika. Wote tulikuwa tunakaribishwa. Wakati mwingine lakini walikuwa hawatupokei kwa ukarimu, kwani anakumbuka kwamba walipokuwa wakizungumzia juu ya Kisiwa cha Malta, akiwataja kuwa ni Mafia wa nyumbani.

Padre Borg aidha akielezea juu ya hali halisi ya sasa ya kazi yao kama kikundi kwa ajili ya huduma ya wakimbizi (JRS), amethibitisha juu ya ugumu na shida zilizopo, hata kwa upande wa kifedha. Kuna idadi kubwa ya wakimbizi ambao wako katika vituo.  Mwanzo angalau wachache walikuwa wanaweza kutoka nje na  kufanya kazi, lakini kwa sasa hakuna kazi. Mapadre hao wanasaswa kuwasadia wao chakula na kuwasaidia katika masuala ya kiafya na kulipa kodi za nyumba. Kuna matatizo makubwa.

Na kwa upande wa hali halisi ya janga la Corona, anabainisha kwamba wanaishi karibu kama walivyo watu wote, kwa wasiwasi mkubwa. Wanajiuliza je ni jambo gani litatokea baadaye? Je ukawaida utakuwa namna gani? Ni wasiwasi mkubwa walio nao  kwa ajili ya maskini wengi wapya ambao watasababishwa na janga hili. Na wakati huo huo yey binafsi anaamini kuwa wito wa Kanisa uweze kuitikiwa wa kuwa wabunifu katika kutafuta njia mpya za kuwa karibu na watu. Na hii ndiyo anaamini kuwa watu wako wanaiunga mkono na labda kwa kugundua upya Kanisa ambalo liko karibu zaidi na watu. Papa Francisko anarudia kusema mara nyingi nyingi na ndiyo kweli sisi sote tuko katika mtumbwi mmoja. Kipindi hiki ni fursa kwa ajili ya wote.

Padre Borg amebainisha ni wa jinsi gani watu wengi huko Malta wanafuatialia Misa ya Papa ya kila siku katika Kanisa la Mtakatifu Marta.  Na labda kwa sasa watu wanakwenda kwenye misa japokuwa wako majumbani mwao kuliko awali.  Na hii ndiyo njia mpya ya kiutume. Aidha ameongeza kusema “ sisi tumefunga nyumba zote za kufanyia mafungo kwa wageni wetu lakini suala hili halikutuzuia kutoweza kutoa mafundisho na sala kwa njia ya mitandao, kwa mfano nimeendesha mafungo ya kiroho kwa walimu. Ninawasindikiza kiroho kwa njia ya skype jambo ambalo sikuwahi hata kufikiria kwanza na kutenda”.

Padre akisimulia juu ya nchi yao ambayo imeishi ma kufanya uzoefu wa wito wa utalii anaeleza mateso ambayo ni makubwa kwa kipindi hiki. Hofu kubwa ni ikiwa janga litaendelea kwa muda mmrefu watu wengi hawatakuwa na kazi. Kisiwa hicho kilikuwa ni moja ya uchumi ulio na nguvu kwa upande wa Ulaya na hii ni kutokana na kwamba uchumi wao wote unategemea na utalii. Kwa maana hiyo matokeo yatakuwa ni kushuka.

Katika sala ya Papa Francisko Alhamasi 30 Aprili alisali kwa ajili ya Udugu Ulaya kwa mtazamo wa Padre huyo katika bara la kizamani ni kwamba ameishi miaka mingi akiwa nje ya Ulaya.  Inamsikitisha sana kuona jinsi ambavyo Umoja wa Ulaya umedhoofika. Na kwamba kinachoonekana ni kuzungumzia muungano uliondikiwa katika karatasi lakini siyo matendo ya kweli. Kwa bahati mbaya utaifa ambao umejionesha kwa upya katika baadhi ya nchi hauleti matumaini. Ni huruma sana amesisitiza. Kwa maana wanasahau ni kitu gani wameweza kufanya baada ya vita, matatizo yote ambayo waliyapata, misaada ambayo waliipokea kutoka nje… Leo hii ambapo tuna usitawi na tuko vizuri hatutaki kwamba watu waje kusumbua hali zetu nzuri. Tumegeuka kuwa wabinafsi sana. Papa Francisko anayo sababu sana ya kutualika kwa upya katika mshikamano. Haiwezekani kuwa na muungano bila mshikamano”.

02 May 2020, 16:40