Siku ya Wauguzi Duniani Papa amaesema wauguzi ni walinzi na wahudumu wa maisha. Siku ya Wauguzi Duniani Papa amaesema wauguzi ni walinzi na wahudumu wa maisha. 

Ujumbe wa Papa Francisko:Siku ya wauguzi:ni mashujaa na wahudumu wa maisha!

Wauguzi daima wanajikita katika nafasi msingi ya huduma ya kiafya.Kila siku katika kukutana na wagonjwa,wanafanya uzoefu wa kiwewe kitokanacho na mateso ya maisha ya mtu.Ni wanaume na wanawake ambao walichagua kujibu“ndiyo”kwa wito fulani:ule wa msamaria mwema anayejitwisha maisha na majeraha ya jirani.Ni,”Walinzi na wahudumu wa maisha, wakati wa kutoa tiba ya lazima wanahimiza ujasiri,matumaini na imani.Ni Ujumbe wa Papa kwa Siku ya Waufuzi Duniani.

Tunaadhimisha leo hii Siku ya Kimataifa ya Wakunga katika mantiki ya Mwaka wa Kimataifa wa Wakunga na Wauguzi iliyotangazwa na Shirika la  Afya la Umoja wa Mataifa (WHO). Katika siku hii tunakumbuka maadhimisho ya miaka milenia tangu kuzaliwa kwa Florence Nightngale muasisi wa uuguzi wa kisasa. Ndivyo unaanza ujumbe wa Papa Fracisko wa Siku ya Kimataifa ya waguzi ambayo maadhimsho hufanyika kila tarehe 12 Mei ya  kila mwaka. Katika ujumbe wake Papa anasema katika kipindi hiki cha kihistoria kilichokumbwa na dharura ya kiafya duniani, kwa kusababishwa na janga la virusi vya Covid-19, tumegundua sura ya uuguzi, lakini pia hata ile ya ukunga ya kwamba ni nafasi msingi kabisa.

Ushuhuda wa kila siku wa ujasiri

Kila siku tunashuhudia ujasiri na sadaka ya wahudumu wa afya kwa namna ya pekee wauguzi wa kike na kiume ambao kwa utaalam, kujikana mwenyewe, hisia ya uwajibikaji na upendo kwa wengine ambao husaidia watu walioathiriwa na virusi, hata katika hatari ya afya yao binafsi, Papa Francisko amesema. Ni ushuhuda kwamba, kwa bahati mbaya idadi kubwa ya wahudumu wa afya imeongezeka ya waliokufa katika uaminifu wa kutimiza huduma yao.  Kwa maana hiyo Papa Francisko anasali kwa Bwana kwa ajili yao, kwamba Yeye anajua majina yao kila mmoja na kwa waathirika wote wa janga hili. Mfufuka awapatie kila mmoja mwanga wa mbingu na familia zao awapatie nguvu ya imani. Wauguzi daima wanajikita katika nafasi msingi ya huduma ya kiafya. Kila siku katika kukutana na wagonjwa, wanafanya uzoefu wa kiwewe ambacho kinatokana na mateso ya maisha ya mtu. Ni wanaume na wanawake ambao walichagua kujibu “ndiyo”kwa wito fulani: ule wa msamaria mwema anayebeba maisha na majeraha ya jirani. Papa ameongeza ni ”Walinzi na wahudumu wa maisha, wakati wa kutoa tiba ya lazima wanahimiza ujasiri, matumaini na imani".

Taaluma iangazwe na uhusiano wa kibinadamu

Papa Francisko akisisitiza juu ya wauguzi hao kike na kiume anasema uwajibikaji kimaadili uwaongoze katika taaluma yao ili isiweze kuishia katika maarifa ya kisayansi na kiufundi, lakini iangazwe kila wakati na uhusiano wa kibinadamu na ubinadamu na mgonjwa “kwa kuwatunza wanawake na wanaume, watoto na wazee, kila hatua ya maisha, kuanzia kuzaliwa hadi kifo: “ ninyi mnajikita katika usikivu wa kuendelea, kwa maana ya utambuzi na  mahitaji ya mgonjwa yule, katika hatua ambayo anaipitia”. Mbele ya kila hali yoyote kwa hakika haitoshelezi kamwe itifaki, bali inahitajika  nguvu na nguvu zinazoendelea za kufanya mang’amzi na umakini wa kila mtu binafsi”( Hotuba ya Papa kwa wajumbe wa Shirikisho la Vyo vya Taaluma ya Uuguz,3 Machi 2018).

Wakunga nao ni sura ya Kanisa, hospitali kambini:umuhimu wa miundo ya kiafya

Kwa mujibu wa Papa anafikiria hata wakunga, kuwa wao wako karibu na watu wakati wa kipindi kigumu cha maisha yao, wakati wa kuzaliwa na wakati wa kifo, wagonjwa na katika kuponyesha, ili kuwasaidia washinde hali  hiyo ngumu sana. Na mara nyingi, wao wanakuwa karibu yao wakati wanakufa, kwa kuwatia nguvu na faraja katika dakika za mwisho. Kwa kujitoa kwao, wao ni kati ya wale “watakatifu wa mlango wa jirani”(Rej Mahubiri, 9 Aprili 2020).  Papa ameongeza “ Ninyi ni sura ya Kanisa “hospitali ya kambini”, mahali ambapo mnaendelea kujikita na utume wa Yesu Kristo ambaye aliwakaribia na kuponyesha watu wenye mateso kwa kila aina ya mabaya na kuinama ili awaoshe miguu wafuasi wake. Asante kwa huduma yenu kwa ubinadamu!

Katika Nchi nyingi, janga limeweka mwanga hata kwa ukosefu kubwa kwa ngazi ya huduma ya kiafya. Kwa maana hiyo Papa Francisko awageukia “wahusika wa Mataifa ulimwenguni kote, ili wawekeze katika afya kama faida msingi wa wote, kuongeza miundo na vifaa na kuajiri wauguzi zaidi, ili kuhakikisha utunzaji wa kutosha kwa kila mtu, katika kuheshimu hadhi ya kila mtu. Ni muhimu Papa anongeza kutambua kikamilifu jukumu msingi ambalo taaluma hii inachukua katika utunzaji wa mgonjwa, shughuli ya dharura katika maeneo, kuzuia magonjwa, kuhamasisha afya, utunzaji katika muktadha wa kifamilia, kijumuiya na kishule. Wauguzi wa kike na kiume kama vile wakunga, wanayo haki na inayostahili kuthamanishwa vema na kuwaunganisha katika mchakato ambao unatazama afya ya watu na ya jumuiya.

Matokeo mema ya kuwekeza katika afya

Papa Francisko amesema kuwa hii imejionesha wazi kwamba kuwekeza juu yake inaboresha matokeo kwa maana ya utunzaji na afya kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo amebainisha, inahitaji kukuza wasifu wao wa kitaalam kwa kutoa zana zinazofaa za kisayansi, kibinadamu, kisaikolojia na kiroho katika mafunzo yao; na kama ilivyo pia ubora wa hali ya kazini kwao na kuhakikisha haki ili waweze kujikita kikamilifu hadhi ya huduma yao. Kutokana na  hiyo Vyama vya wahudumu wa kiafya vina jukumu muhimu ikiwa pamoja na kutoa mafunzo, kuwasindikiza kila mmoja ili kuwafanya wahisi kuwa kiungo kimoja na kamwe wasipotee na kuwa peke yao, mbele ya changamoto za kimaadili, kiuchumi na za kibinadamu ambazo zinajumuishwa katika taaluma hiyo.

Kazi ya wakunga ni muhimu kati ya kazi zote zilizopo

Kwa wakunga, kwa namna ya pekee wale wanaoshughulikia wanawake wajawazito na wanawasaidia kutoa nje mwanga wa watoto wao, Papa Francisko anawambia kuwa “ Kazi yenu ni moja muhimu sana kati ya zile zilizopo, kwa kujikita moja kwa moja katika huduma ya maisha na ya umama. Katika Biblia yapo majina mawili ya mashujaa wakunga, Sifra na Pua, hawa wanatajwa katika mwanzoni mwa Kitabu cha Kutoka1,15-21. Kwa maana hiyo Papa Francisko amesema kuwa “hata leo hii Baba wa Mbingu anawatazama kwa shukrani kubwa”. Kwa kuhitimisha ujumbe wake,Papa Francisko anasema “wapendwa wauguzi kike na kiume, katika kilele hiki inawezekana kuweka kiini cha kazi yenu, kwa faida ya afya ya jamii nzima. Kwa ajili ya familia zetu na kwa wale wote mnao watunza, ninawakikishia sala zangu na kuwabariki kwa moyo Baraka ya Kitume”

Ikumbukwe mwaka huu 2020 umechaguliwa na umoja wa mataifa kuwa wa wauguzi na wakunga

Katika kuenzi wataalam  hawa wauguzi na wakunga Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani mwezi Januari mwaka huu, Bwana Tedross Adhamon Ghebreyesus alikuwa amesema “wauguzi na wakunga ni uti wa mgongo wa kila mfumo wa afya na mwaka 2020 tunatoa wito kwa nchi zote kuwekeza kwa wauguzi na wakunga kama sehemu ya ahadi ya huduma za afya kwa wote.” Aidha alikumbusha kwamba mwaka 2020 pamoja na kuwa Mwaka wa wauguzi na wakunga ni sambamba na maadhimisho ya miaka milenia tangu kuzaliwa kwa Florence Nightngale muasisi wa uuguzi.

Mwaka huu  2020  kwa maana hiyo ni  kusherehekea wataaluma ambao wanatoa huduma mbalimbali muhimu kwa watu kila mahali. Mbali ya kuzuia, kubaini, kupima magonjwa na kutoa huduma ya kitaalam wakati wa kujifungua wauguzi na wakunga pia wanaokoa Maisha ya watu katika majanga na dharura za kibinadamu na vita. Hivi sasa duniani kuna wauguzi milioni 22 na wakunga milioni 2 wakiwa ni nusu ya wafanyakazi wote wa huduma za afya kwa mujibu wa shirika la Afya duniani WHO. Kwa mujibu wa shirika hilo limesema dunia inahitaji wahudumu wa afya milioni 18 zaidi na takribani nusu yao ni wauguzi na wakunga ili kuweza kutimiza lengo la huduma za afya kwa wote kabla ya kumalizika muongo huu kwenda sanjari na ahadi iliyowekwa na viongozi wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka 2019.

12 May 2020, 12:00