Baba Mtakatifu Francisko amewaandikia watu wa Mungu nchini Argentina ujumbe wakati wa maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Lujan, 8 Mei 2020. Baba Mtakatifu Francisko amewaandikia watu wa Mungu nchini Argentina ujumbe wakati wa maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Lujan, 8 Mei 2020. 

Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Watu wa Mungu nchini Argentina!

Papa Francisko akiwa ameungana na watu wa Mungu nchini Argentina, watachukua fursa hii, kumshirikisha Bikira Maria hofu na mashaka; furaha na matamanio yao halali kwa siku za usoni. Anataka kumwomba Bikira Maria aweze kuwalinda na kuwaombea huruma na msamaha kwa Mwanae mpendwa Kristo Yesu, bila kuchoka, kwa kutambua kwamba, kamwe Yesu hawezi kuchoka kusamehe.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Familia ya Mungu nchini Argentina kila mwaka ifikapo tarehe 8 Mei inaadhimisha kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Luján “"Nuestra Señora de Luján". Haya ni Madhabahu ambayo Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake, aliyatembelea mara kwa mara na kutoa Sakramenti ya Kitubio kwa waamini waliokuwa wamejiandaa vyema. Ni katika muktadha wa kumbu kumbu endelevu katika maisha na utume wake, Baba Mtakatifu amemwandikia barua Askofu mkuu Jorge Scheinig wa Jimbo kuu la Mercedes Luján, kumwelezea kwamba, hata yeye ataungana pamoja nao katika maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Luján.

Baba Mtakatifu anasema, anataka kufanya hija ya maisha, huku akiwa ameungana nao kiroho, ili kumwangalia Mama mpendelevu na kumwachia pia fursa ya kuweza kumwangalia kwa mcho ya huruma na upendo yanayopyaisha maisha ya mwamini na kumkirimia nguvu ya kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu! Hii ni hija ya kiroho anayoifanya kwa kuungana na kushikamana na watu wa Mungu, wanaopenda na kumheshimu Bikira Maria. Ni waaminifu lakini pia ni wadhambi kama alivyo Baba Mtakatifu Francisko mwenyewe! Akiwa ameungana na watu wa Mungu nchini Argentina, watachukua fursa hii, kumshirikisha Bikira Maria hofu na mashaka; furaha na matamanio yao halali kwa siku za usoni. Anataka kumwomba Bikira Maria aweze kuwalinda na kuwaombea huruma na msamaha kwa Mwanae mpendwa Kristo Yesu, bila kuchoka, kwa kutambua kwamba, kamwe Yesu hawezi kuchoka kusamehe.

Baba Mtakatifu anapenda kuahidi mbele ya Bikira Maria kwamba, atajitahidi kadiri ya uwezo wake kuwa mtu mwema zaidi. Ni matumaini yake kwamba, ataweza kurejea nyumbani akiwa ameombewa neema na baraka! Ibada kwa Bikira Maria wa Luján “Nuestra Señora de Luján" ilianza kunako mwaka 1630 baada ya Sanamu ya Bikira Maria wa Lujan kuwasili nchini Argentina ikiwa imebebwa na Manuel, ambaye alikuwa ni mtumwa kutoka nchini Angola. Mapokeo yanaonesha kwamba, gari lililokuwa limeibeba Sanamu ya Bikira Maria wa Luján haikuweza kuendelea na safari kutokana na kuzuiliwa na Mto Luján. Sanamu hii ikakaa mjini Luján kwa siku kadhaa na watu, wakalifahamu jambo hili na kwenda huko, ili kumtolea Bikira Maria heshima. Kunako mwaka 1887, Papa Leo wa XIII aliridhia Ibada kwa heshima ya Bikira wa Luján na kuagiza kwamba, Ibada kwa heshima ya Mama huyu iadhimishwe Jumamosi baada ya Jumapili ya IV ya Kipindi cha Pasaka!

Papa: Arentina

 

 

 

 

05 May 2020, 14:18