Tafuta

Vatican News
Jumapili ya Kwanza ya Mwezi Mei ya Kila Mwaka ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Watoto Wanaodhulumiwa, Kunyonywa na Kutothaminiwa nchini Italia. Jumapili ya Kwanza ya Mwezi Mei ya Kila Mwaka ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Watoto Wanaodhulumiwa, Kunyonywa na Kutothaminiwa nchini Italia. 

Siku ya Kitaifa Ya Watoto wanao nyonywa, dhulumiwa na wale wasiothaminiwa Italia

Baba Mtakatifu anawahamasisha viongozi wa ngazi mbali mbali pamoja na wafanyakazi katika sekta mbali mbali za maisha, kuendelea kujizatiti katika mchakato wa kuzuia pamoja na kuamsha dhamiri nyofu huku wakisaidiwa na wadau mbali mbali katika sekta ya elimu. Baba Mtakatifu anawashukuru watoto wa Chama hiki cha "Meter" waliomtumia picha iliyochorwa na watoto hawa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Tafakari ya Sala ya Malkia wa Mbingu, Jumapili tarehe 3 Mei 2020 ameyaelekeza mawazo yake kwa wanawachama wa “Meter”, ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Watoto Wanaodhulumiwa, Kunyonywa na kutokuthaminiwa nchini Italia. Baba Mtakatifu anawahamasisha viongozi wa ngazi mbali mbali pamoja na wafanyakazi katika sekta mbali mbali za maisha, kuendelea kujizatiti katika mchakato wa kuzuia pamoja na kuamsha dhamiri nyofu huku wakisaidiwa na wadau mbali mbali katika sekta ya elimu. Baba Mtakatifu anawashukuru watoto wa Chama hiki waliomtumia picha iliyochorwa na watoto hawa!

Itakumbukwa kwamba, Chama cha “Meter” kilianzishwa kunako mwaka 1989 na Don Fortunato Di Noto, ili kusaidia kukuza na kudumisha mchakato wa kuzuia na kuwahabarisha watu wa Mungu nchini Italia kuhusu dhuluma, nyanyaso na unyonyaji wanaofanyiwa watoto wadogo. Chama cha “Meter” kimeendelea kujipambanua kwa kusimama kidete kulinda, kudumisha na kutetea haki msingi za watoto nchini Italia. Kuanzia mwaka 1996 nchini Italia kunaadhimishwa Siku ya Kitaifa ya Watoto Wanaodhulumiwa, Kunyonywa na kutokuthaminiwa. Maadhimisho haya ni kuanzia tarehe 24 Aprili na kuhitimishwa Jumapili ya Kwanza ya Mwezi Mei ya kila mwaka.

Papa: Meter

 

03 May 2020, 13:10