Tafuta

2020.05.10 Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana (Regina Coeli 2020.05.10 Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana (Regina Coeli 

Papa Francisko:Tuombe Yesu atuelekeze njia ya kwenda mbinguni pasipo machozi!

Katika Jumba la Maktaba ya Kitume Vatican Dominika ya V ya Pasaka,Papa Francisko ametoa tafakari yake kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu.Amejikita kufafanua juu ya hotuba ya buriani ya Yesu kwa mitume wake akiwambia kuwa Yeye ni njia.Yesu amekwisha toa ombi la nafasi yetu Mbinguni mahali ambapo hapatakuwa na kilio na wala migawanyiko.Inatakiwa njia ya kufuata nyayo za Yesu katika upendo mnyeyekevu na huduma kwa wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika Injili ya leo (taz Yh 14,1-12) tumesikia kwa kile kiitwacho “ Hotuba ya buriani” ya Yesu. Ni maneno aliyo waelekeza wafuasi wake wakati wa Karamu ya mwisho kabla ya kukabiliana na Mateso. Katika wakati huo mgumu Yesu alianza kusema Msifadhaike mioyoni mwenu. Anasema hayo hata kwetu sisi katika wakati mgumu sana wa maisha. Lakini je ni kufanya nini ili moyo husifadhaike? Na kwa nini moyo unafadhaika?

Njia mbili za kuzuia mfadhaiko wa roho

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko, Jumapili tarehe 10 Mei 2020 ambayo ni Dominika ya V ya Kipindi cha Pasaka, akiwa katika Jumba la Maktaba mjini Vatican. Papa Francisko akiendelea na tafakari hiyo anasema kuwa Bwana anaelekeza njia mbili za kuzuia mfadhaiko. Ya kwanza ni “Niamini mimi (Yh 14,1). Utafikiri ni ushauri wa kinadharia kidogo. Kinyume chake Yesu anataka kutuambia jambo moja msingi. Yeye anatambua kuwa maisha, wasiwasi wa hatari, mfadhaiko vinazaliwa kutokana na hisia ya kushindwa kufanya jambo, kuhisi upweke na bila kuwa na sehemu ya kuegemea mbele ya kile kinachotokea. Huzuni huo mahali ambapo matatizo uongezeka juu ya matatizo mengine na ambayo huwezi kuyashinda peke yako. Papa Francisko amebainisha kuwa “tunahitaji msaada wa Yesu na kwa maana hiyo Yesu anatuomba tuwe na imani kwake, yaani tusiegeme nguvu zetu tu, bali kwake Yeye. Hii ni kutokana na kwamba ili kuondokana na wasi wasi, unapitia njia ya kujikabidhi.

Ninakuletea mfadhaiko wangu na mahangaiko yangu

Papa Francisko amesema kuwa "Kujikabidhi kwa Yesu ni kufanya hatua iliyo ya juu. Na ndiyo huo huru wa kuondokana na mfadhaiko. Na  Yesu amefufuka, Yeye yupo kwa ajili hiyo kuwa nasi daima  karibu. Kwa njia hiyo tunaweza kumwambia “ Yesu ninakuamini kuwa ulifufuka na uko karibu nami. Ninaamini kwamba unanisikia. Nikuletea mfadhaiko wangu, mahangaiko yangu, nina imani kwako na ninakuamini Wewe".

 Yesu alituandalia nafasi kule mbinguni

Njia nyingine ya pili ambayo Papa Francisko anashauri  ili kuondokana na mfadhaiko wa roho ni ambayo Yesu anaeleze kuwa “ Katika nyumba ya Baba kuna makao mengi(…) Ninakwenda kuwaandalia makao. Tazama Ni jambo gani Yesu alifanya. Yeye alifanya maombi ya kuandaa nafasi mbinguni. Alichukua ubinadamu wetu na kuupeleka zaidi ya kifo katika nafasi mpya Mbinguni, kwa sababu na sisi tuwepo mahali alipo Yeye. Ni uhakika ambao unatufariji ya kuwa kuna nafasi kwa ajili ya kila mmoja. Kuna nafasi hata kwa ajili yangu. Kila mmoja wetu anaweza kusema kuwa “ kuna nafasi kwa ajili yangu” Papa Fancisko amefafanua. Sisi hatuishi bila kusudi na bila mwelekeo. Tunatarajiwa, sisi ni wenye thamani. Mungu anatupenda sisi , sisi ni watoto wake. Na kwa ajili yetu ameandaa mahali panapostahili na pazuri yaani Mbingu. Tusisahau ya kuwa makao yanayotungojea ni Mbingu. Hapa duniani tunapita. Tumeumbwa kwa  ajili ya Mbingu, kwa ajili uzima wa milele, ili kuishi milele. Milele ni kitu ambacho hatuwezi hata kufikiria kwa sasa. Lakini Papa Francisko ameshauri kuwa ni nzuri zaidi kufikiria kwamba hii itakuwa kwa furaha ya milele, katika ushiriki kikamili na Mungu na wengine, bila machozi zaidi, bila hasira, bila migawanyiko na usumbufu.

Ni jinsi gani ya kufika Mbinguni?

Lakini je jinsi ya kufikia Mbingu? Njia ni ipi?  Kwa kujibu Papa Francisko anabainisha kuwa “Hapa kuna maneno ya Yesu yenye uamuzi. Leo anasema “Mimi ndimi njia" (Yhn14, 6). Ili kuweza kwenda mbinguni njia ni Yesu. Ni kuwa na uhusiano wa kuishi pamoja naye, kumwiga kwa upendo, na kufuata nyayo zake. Na mimi, kama Mkristo, wewe, kama Mkristo, kila mmoja wetu Wakristo, tunaweza kujiuliza: “Nafuata njia ipi?”. Kuna njia ambazo hazielekezi Mbingu kwa mfano  njia za ulimwengu, njia za kujithibitisha mwenyewe na njia za nguvu za ubinafsi.

Kuna njia ya Yesu, njia ya upendo mnyenyekevu

Na kuna njia ya Yesu, njia ya upendo mnyenyekevu, ya sala, ya upole, ya imani na ya kuwahudumia wengine. Papa Francisko amengeza kusema kuwa “Siyo njia yangu kuwa mstari wa mbele, ni njia  ya Yesu kuwa mtari wa mbele na mhusika wa maisha yangu.  Inabidi kuelendea mbele kil siku kumuuliza: “Yesu, unafikiria nini kuhusu chaguo langu? Je! Ungefanya nini katika hali hii na watu hawa?”Papa Francisko kwa kuhimisha na maswali hayo anasema kuwa “Itatufaa sana sisi kumuuliza Yesu, ambaye ndiye njia, kutupatia maelekezo ya Mbingu. Mama yetu, Malkia wa Mbingu, atusaidie kumfuata Yesu, aliyetufungulia Mbingu.

10 May 2020, 14:08