Mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Papa Francisko amekumbusha siku ya upashanaji habari tarehe 24 Mei. Mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Papa Francisko amekumbusha siku ya upashanaji habari tarehe 24 Mei. 

Papa Francisko:Siku ya Upashanaji Habari:sisi sote ni historia kubwa.Tutazame wakati ujao kwa tumaini!

Katika Siku kuu ya Kupaa kwa Bwana,sambamba na siku ya 54 ya Upashanaji wa Habari ulimwenguni Papa Francisko amesema tukio hili lifanye kuwa na utambuzi kwamba sisi sote ni sehemu ya historia.Ni kutazama wakati ujao kwa matumaini huku tukisaidiana mmoja na mwingine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 24 Mei 2020 Mama Kanisa anasheherekea Siku kuu ya Kupaa Mbinguni Bwana, ambapo Papa Francisko sambamba na siku hiyo amekumbuka siku Siku ya 54 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni na kwamba siku hii itusaidie kuelewa kuwa sisi sote ni sehemu ya historia kubwa kuliko sisi na tunaweza kutazama siku zijazo kwa tumaini ikiwa tutatambua kweli namna ya kutunza mmoja na mwingine.

Katika maneno ya Papa Francisko amesema  kuwa leo ni siku ya Upashanaji Habari Ulimwenguni ambayo imejikita kwa mada inayohusu simulizi. “Nawe upate kusema masikioni mwa wanao, na masikioni mwa mjukuu wako”, kutoka Kitabu cha Kutoka10, 2. Maisha yanakuwa ni historia”. Papa Francisko amesema kuwa tukio hili liweze kuwatia moyo wa kusimulia na kushirikishana historia zenye kujenga, ambazo hutusaidia kuelewa kuwa sisi sote ni sehemu ya historia kubwa kuliko sisi na tunaweza kutazama siku zijazo kwa matumaini ikiwa tutambua kweli namna ya kutunza mmoja na mwingine”.

Hata hivyo katika ujumbe wa Papa Francisko kuhusiana na mada ya kusimulia na kwamba hakuna historia ya mwanadamu isiyokuwa na maana au iliyo ndogo. Na kwa maana hiyo mada hiyo“ inatusaidia sana  kutafakari juu ya jitihada za kazi tulizoalikwa kutenda kama wapashanaji wa habari katika nyakati hizi zilizodidimia ndani ya janga la habari za kidunia katika historia ya maisha ya mwanadamu. Ili kukaribia na kuingia ndani kwa kina, inahitajika zaidi kuliko hapo awali kutumia macho ya Msimuliaji kwa utambuzi kwamba hakuna mtu hasiye onekana kwenye ulimwengu na historia ya kila mtu inawezekano kabisa wa kubadilika.

Hii ni kuruhusu kubadili kutoka katika mtazamo umimi na kwenda ule wa sisiNi fursa ya kuachana na mtazamo wa kujitoshelezwa katika kulenga mzunguko wa  digrii 180, bila kuatazama nyuma yetu  bali kile cha mbele yetu. Kusimulia ya leo hii inageuka kuwa msingi sana kwa ajili ya kujenga kesho, kwa kukusanya pamoja mambo ambayo yataunda msingi wa kumbukumbu yetu. Na katika wakati ambao Covid-19, inavuna waathirika wengi sana na miongoni mwao zaidi wazee tumo hatari ya kunyimwa sehemu muhimu ya kumbukumbu yetu hivyo hii inakuwa  na maana zaidi.

24 May 2020, 18:16