Papa kwa tukio la Thy Kingdom Come:Kuna haja ya kufariji mioyo ya wenye kuhangaika!

Katika fursa ya tukio la Thy kingdom Come,yaani Ufalme wako Uje,Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki hao akibainishakuwa hatuwezi kuomba binadamu abaki katika umoja ikiwa tunatembea njia tofauti.;kwa maana hiyo tusali kwa ajili ya mmoja na wengine na tuhisi uwajibikaji kwa wengine.Roho Mtakatifu atupatie hekima na ushauri.Ameomba kusali kwa wanaotakiwa kuchukua uamuzi nyeti na dharura ili walinde maisha ya binadamu na hadhi ya kazi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 31 Mei 2020 Papa Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya video kuwa anaungana kwa furaha na Askofu Mkuu Justin Welby na washiriki wote wa tukio la ufalme wa mungu uje “Thy Kingdom Come” ili kushirikishana kwa kile alichokuwa nacho moyoni. Ni katika katika mkesha wa siku kuu ya ujio wa Roho Mtakatifu ambapo makanisa mengi ya kipentekoste yanaadhimisha kwa namna ya pekee siku kuu hii. Kwa njia hiyo Papa Francisko katika ujumbe anakumbusha kuwa Pentekoste inakumbusha siku ya ujio wa nguvu ya Roho wa Mungu. Siku hiyo maisha ya Mungu yalivuviwa kati yetu, kwa kuleta matumaini mapya, amani na furaha ambayo ilikuwa haijulikani.

Kuna haja ya kufarijiwa kwa mioyo ya wengi wenye kuhangaika

Katika siku ya Pentekoste, iliambukiza maisha duniani. Ni maambukizi mangapi kwa meizi hii ambayo yameleta vifo katika nchi! Kwa maana hiyo hakuna kipindi kama hiki kilichowahi kuwa na ulazima wa kuomba Roho Mtakatifu ili aweze kuleta maisha ya Mungu, na upendo katika mioyo yetu. Ili wakati wetu uweze kuwa bora kuna pia  lazima wa mioyo yetu igeuke kuwa bora. Siku ya Pentekoste watu walikuwa wakuzungumza kwa lugha zao tofauti. Katika miezi hii Papa amebainisha kuwa kinyume chake tumeombwa kuzingatia kanuni za hali na ulazima wa kukaa mbali. Lakini tunaweza kuelewa vema ndani mwetu kile ambacho wanahisi wengine. Hofu na ukosefu wa uhakika unatujumuisha sisi wote. Kuna haja ya kufarijiwa kwa mioyo ya wengi wenye kuangaika.

Yesu alitumia neno 'Msaidizi' au 'Mfariji'

Papa Francisko amefikiria kile ambacho Yesu alikuwa anasema wakati wa kuzungumza juu ya Roho Mtakatifu, na kwamba alitumia kwa namna ya pekee neno “Msaidizi” yaani “mfariji”. Walio wengi walihisi faraja yake na ile amani ya ndani ambayo tunahisi kupendwa, ile nguvu mwanana ambayo daima inatupatia ujasiri , hata wakati wa uchungu. Roho Mtakatifu, anatupatia uhakika kuwa sisi hatupo peke yetu bali kwa kusaidiwa na Mungu. Ushauri Papa Francisko kwa washiriki hawa ni kwamba kile ambacho wamepokea lazima kitolewe kwa maana “tunaalikwa kusambaza faraja ya Roho na ukaribu wa Mungu”. Lakini Je tufanyeje? Tufikire kile ambacho sasa tunataka kuwa nacho kama vile  kutiwa moyo, kupewa ujasiri na kupata mtu mwingine ambaye anaweza kutusaidia, mtu ambaye asali kwa ajili yetu, ambaye alie kwa ajili yetu, na mwenye kutusaidia kukabiliana matatizo yetu. Jibu lake “ Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo. (Mt 7,12). Tunataka kusikilizwa? Wasikilize. Tunataka kutiwa moyo? Basi watie moyo wengine,   Tunataka mmoja aweze kutusaidia? Basi   Tusaidie wengine ambao hawana mtu. Tunahitaji matumaini ya kesho? Basi tutoe matumaini kwao leo hii.

Leo hii tunaona majanga, ni majeraha mangapi?

Papa Francisko aidha akiendelea kwa njia ya video amesema, “ leo hii tunaona majanga. Ni majeraha mangapi, ni utupu kiasi  ambao haukuweza kujazwa, ni machungu mangapi ambayo hayana faraja! Kwa maana hiyo basi tutafsiri faraja hiyo ya roho na kuonesha matumaini na Bwana atafungua njia mpya katika safari yetu”. Kadhalika Papa amependa kushirikisha jambo katika safari yetu. Ni jinsi gani anatamani kuona wakristo wanakuwa na umoja zaidi  katika kushuhudia huruma ya Mungu kwa ajili ya ubiandamu uliojaribiwa kwa nguvu. Tuombe Roho zawadi ya umoja kwa sababu tutaweza kueneza udugu tu ikiwa tutaishi kidugu kati yetu, ameshauri Papa.

Hatuwezi kuomba ubinadamu ubaki katika umoja wakati njia ni tofauti

Hatuwezi kuomba ubinadamu ubaki katika umoja ikiwa tunatembea njia tofauti.  Kwa maana hiyo tusali kwa ajili ya mmoja na mwingine, na tuhisi uwajibikaji wa mmoja na mwingine  Roho mtakatifu atupatie hekima na ushauri. Katika siku hizi tusali kwa ajili ya wale ambao wanapaswa kuchukua uamuzi nyeti na dharura ili walinde maiisha ya binadamu na hadhi ya kazi. Katika hili, ni kuwekeza katika afya juu ya kazi na uondoaji wa ukosefu wa usawa na umaskini. Hakuana wakati kama huu, kama hapo awali ambao unasaidia kuwa na mtazamo wenye utajiri wa ubinadamu.  Hatuwezi kuanza kutazama juu katika kufuata mafaniko bila kuhangaikia ambaye amebaki nyuma.

Kuna haja ya kurudia kutembea pamoja kuelekea kwa Mungu

Papa Francisko amesema , hata kama wengi wanafanya hivyo, Bwana anatuomba tubadili mapigano. Siku ya Pentekoste Petro alisema kwa lugha ya Roho kwamba “ongokeni” (Mdo 2,38), kubadilisha mwelekeo, kubadilisha gia nyigine. Kuna haja ya kurudi kutembea katika kuelekea kwa Mungu na kwa jirani. Hatuwezi kutengenisha, wala kusimama mbele ya kilio cha waliosahauliwa na sayari iliyojeruhiwa. Kuna haja ya kuungana kwa ajili ya kukabiliana na janga ambalo limesambaratika, la virusi lakini pia hata janga la njaa, vita, kudharau maisha na sintofahamu. Ni kwa njia ya kutembea pamoja tunatakwenda mbali. Kwa kuhitimisha Papa amewahimiza kueneza tangazo la maisha ya Injili na wawe ishara ya matumaini. Amewashukuru kwa moyo na kuwaomba wasali kwa ajili yake!

31 May 2020, 10:00