Tafuta

Mtakatifu Paulo VI Mtakatifu Paulo VI  

Papa Francisko akumbusha kumbu kumbu ya Mtakatifu Paulo VI na Pentekoste!

Mara baada ya katekesi yake Papa FRancisko ametoa salam kwa waamini wote kwa lugha mbalimbali na kuwakumbusha maandalizi ya ujio wa Roho Mtakatifu na wakati huo huo kumbuka mtangulizi wake Mtakatifu Paulo VI ambaye anakumbukwa na mama Kanisa kila tarehe 29 Mei ya kila mwaka.

Tarehe 27 Mei 2020 mara baada ya tafakari ya Katekesi yake, Papa Francisko amesalimia waamini wote kwa mataifa mbali mbali. Amekumbuka Maadhimisho ya kumbu kumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Papa Paulo VI ambaye mama Kanisa anafanya maadhimisho kila tarehe 29 Mei ya kila mwaka. Papa Francisko amesema kuwa "mfano wa Askofu wa Roma ambao ulimfikisha kilele cha utakatifu, uwatie moyo kila mtu aweze kukumbatia mawazo ya kiinjili".

Kuwa na upole katika matendo ya Roho Mtakatifu

Mawazo yake pia Papa Francisko yamekuwa ni kwa wazee vijana, wagonjwa na wanandoa. Hakusahahu hata siku kuu ya Pentekoste kwana amesema , hali halisi ya maandalizi wa Siku Kuu ya Ujio wa Roho Mtakatifu ina karibia. Kwa maana hiyo amewashauri  wawe daima wapole katika matendo ya Roho Mtakatifu ili maisha yao daima yaweze kupashwa joto na kuangazwa na upendo ambao Roho Mtakatifu anayevuvia ndani ya mioyo. Kwa wote amewabariki.

Kumbu kumbu ya Mtakatifu Paulo VI

Ikumbukwe kuwa kila tarehe 29 Mei ya kila mwaka kiliturujia ni siku ya kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI na hiyo ni kutokana na kwamba Papa Francisko mwaka jana 2019  aliridhia tamko lililotolewa na Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa kwamba kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI itakuwa inaadhimishwa kila tarehe 29 Mei ili kutoa umuhimu wa ulimwengu mzima wa mifano ya utakatifu wa watu wa Mungu. “Kwa kuzingatia utakatifu wa maisha ya Papa Paulo VI, ushuhuda wake katika matendo na maneno, kwa kuzingatia huduma yake katika uchungaji wa kitume kwa ajili ya Kanisa duniani kote, na  kwa kusilikiza maoni na matashi ya Watu wa Mungu, ninaridhia kwamba maadhimisho ya Mtakatifu Paulo VI yaandikwe katika Kalenda Kuu ya Kirumi na kufanyiwa kumbukumbu ya kawaida ya kiliturujia kila tarehe 29 Mei”.

Ndiyo maandishi yaliyokuwamo katika Hati kutoka kwa Baraza la Kipapa la Ibadan a Nidhamu ya na Sakramenti za Kanisa iliyotolewa tarehe 6 Februari lakini ikionesha sahihi ya tarehe 25 Januari 2019 sambamba na Sikukuu ya Mtakatifu Paulo mtume wa watu. Katika Hati hiyo iliandikiwa kuwa kumbukumbu hii inapaswa iwekwe katika Kalenda na Vitabu vya kiliturujia kwa ajili ya maadhimisho ya Misa na masifu. Maandishi ya kiliturujia lazima yaandaliwe na kuambatanisha na hati hiyo, ambayo inatakiwa itafsiriwe na kuidhinishwa mara baada ya kupitishwa kwa waraka na kutangazwa na Mabaraza ya Maaskofu. Hati hiyo inaonesha maisha, kazi na huduma ya Mtakatifu Papa Paulo VI.

27 May 2020, 13:30