Vatican News
10-09-2013 Ziara ya Papa Francisko kwa wakimbizi kwenye kituo cha Astalli 10-09-2013 Ziara ya Papa Francisko kwa wakimbizi kwenye kituo cha Astalli 

Papa ameshukuru jitihada za ukarimu wa kituo cha Astalli!

Papa Francisko amemwandikia Padre Ripamonti,Mkurugenzi wa Kituo cha Wajesuit (JRS) cha Wakimbizi nchini Italia akiwashukuru kwa kutetea haki ya waomba hifadhi.Juhudi zao ni mfano wa utamaduni wa ukarimu na amewahakikishia ukaribu wake wa sala na upendo kwa wote wanaohama.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Ripoti ya hivi karibuni ya Kituo cha Astalli cha Shirika la Yesu (JRSI, iliyochapishwa siku chache zilizopita, inasimulia juu ya maisha ambayo yamesimama ya wahamiaji, walio katikati ya mtego wa janga na ambalo linazuia au kupunguza maisha ya kila siku. Kwa hakika ni pigo la kitokuwa na uhakika kwa wale ambao maisha yao kila siku lazima ni kubuni namna ya kuanzia mwanzo katika Nchi mpya!

Kati ya watu elfu 20,000 waliokutana na Kituo hicho mnamo mwaka 2019, pamoja na wakimbizi na wanaotafuta hifadhi, watu11,000 wako Roma. Na kama hiyo haitoshi, ripoti ya hivi karibuni inasema kwamba  sera za kisiasa kuhusu wahamiaji, kubana, kufungwa ikiwa siyo za kibaguzi zimeonyesha katika miaka ya mwisho kuwa na maisha magumu, kwa kutengwa na kukosekana kwa usawa, na kuifanya jamii yote kuwa hatarini zaidi.

Kukarimu kwa upendo kidugu

Katika kunukuu Ripoti hiyo kwenye ujumbe wa Padre Camillo Ripamonti, mkurugenzi wa Kituo cha  Astalli, Papa “anamshukuru sana kwa ujasiri ambao wanauonesha katika kukabiliwa na changamoto za uhamiaji hasa katika wakati huu nyeti, kwa ajili ya kutafuta haki kwa waomba hifadhi kama vile maelfu ya watu wanaokimbia vita, mateso na machafuko makubwa ya kibinadamu”.

Francisko pia anaonesha ukaribu wake hata kwa watu ambao kwa mujibu wa sheria za kimataifa wanafafanuliwa kama “wakimbizi” na kwamba “ninyi wakaribisheni na upendo wa kindugu. Na kwa ninyi nyote niko karibu na wote kwa sala na upendo na ninawasihi kuwa na imani na tumaini katika ulimwengu wa amani, haki na udugu miongoni mwa watu”.

Mfano wa ukaribu na mshikamano

Kwa kuhitimisha ujumbe wake kwa kituo hiki cha Astalli, na ambacho ni hali halisi ya ulimwengu, anasema “Mfano wenu uweze kuwa chachu iliyopyaishwa jitihada kwa ajili ya utamaduni halisi wa ukarimu na mshikamano”.

28 May 2020, 16:00