Tafuta

Vatican News
Mtakatifu Yohane Paulo II akiwa mlimani. Mtakatifu Yohane Paulo II akiwa mlimani. 

Maneno ya Papa Mstaafu kuhusu huruma ya Mtakatifu Yohane Paulo II!

Papa Benedikto XVI ametuma barua kwa Baraza la Maaskofu wa Poland kufuatia na maadhimisho ya miaka mia moja ya mtangulizi wake inayotarajiwa kufanyika tarehe 18 Mei 2020.

VATICAN NEWS

Maisha yote ya Papa yalijikita juu ya mapendekezo ya kukubali na kama kiini chake cha imani ya kikristo katika mafundisho ya wokovu na kuruhusu wengine wakubali”. Ndivyo anaandika Papa Mstaafu Benedikto XVI katika barua yake kutokana na fursa ya kumbu kumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II. “Shukrani kwa Kristo Mfufuko, huruma ya Mungu ni kwa ajili ya wote”, Papa mstaafu anakumbusha “wote wanapaswa kujua kuwa katika huruma ya Mungu, mwisho wake inaoneshwa kuwa na nguvu zaidi ya udhaifu”.

Papa Mstaafu Mstaafu  aidha anaandika kwamba“hapa tunahitaji kutafuta umoja wa ndani katika ujumbe wa Yohane Paulo II na malengo msingi ya Papa Francisko; kinyume na kile kinachosemwa wakati mwingine kuwa Yohane Paulo II hakuwa mtoaji adhabu ya maadili. Kwa kuonesha umuhimu msingi wa huruma ya Mungu, yeye anatupatia fursa ya kukubali mahitaji ya kimaadili yaliyotolewa kwa mtu ili kwamba  tusiweze kamwe kujitosheleza. Jitihada zetu kimaadili zipo chini ya mwanga wa huruma ya Mungu, ambaye anajionesha kuwa mwenye nguvu inayoponya udhaifu wetu”.

15 May 2020, 14:13