Tafuta

2020.04.15 Kateksi ya Papa Francisko 2020.04.15 Kateksi ya Papa Francisko 

Papa Francisko:amani siyo utulivu,lakini utafutaji wa maridhiano!

Amani ya Kristo ni tunda la kifo na ufufuko wake.Kuwa wapatanishi wa amani ni kutoa maisha kwa kutafuna njia mpya daima za kupenda.Amani siyo utulivu bali ni utafutaji wa maridhiano daima na kwa hali yoyote.Ndiyo ujumbe uliosikika katika tafakari ya Katekesi yake Papa akidadavua Heri ya Saba ya Mlimani katika Injili na ambaye amefafanua kuwa ni heri inayofanya kazi zaidi na yenye ubunifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katekesi ya leo ni mwendelezo wa Heri ya saba isemayo:“heri wapatanishi” na ambao wanaitwa wana wa Mungu. Ninafurahi kwamba inatafakariwa mara baada ya Pasaka kwa sababu amani ya Kristo ni tunda la kifo chake na ufufuko, kama tulivyosikia katika barua ya Mtakatifu Paulo. Ili kutambua vema Heri hii ni lazima kuelelezea maana ya neno “amani” ambayo inawezekana isieleweke au wakati mwingine kudharauliwa. Ndiyo mwanzo wa  tafakari yake Papa Francisko katika katekesi yake, tarehe 15 Machi 2020 akiwa katika maktaba ya kitume mjini Vatican. Tunapaswa kutambua kati ya mawazo mawili kuhusu amani. Kwanza ni ile ya kibiblia, mahalia ambapo inaonesha uzuri wa neno shalòm ambalo linafafanuliwa kama wingi wa uchanuzi na ustawi. Na wakati katika lugha ya kiyahudi wakitoa salam ya shalòm, ina maana ya kutakiana matashi mema ya maisha, yaliyo kamili, ya matarajio, lakini pia hata kwa mujibu wa ukweli na amani ambao wanatarajia kuupata katika ukamilifu wa masiha, mfalme wa amani (Rej. Is 9,6; Mik 5,4-5).

Amani kama utulivu wa ndani

Maana nyingine ya pili  Papa Francisko amesema ni ile ambayo imeenea , ambapo neno “ amani inaeleweka  kama kitu fulani cha utulivu wa ndani: yaani mimi ni mtulivu, nina amani. Haya ni mawazo ya kisasa, kisaikolokia na zaidi ya kibinafsi. Wengi wanafakiria kuwa amani ni utulivu, maelewano na utulivu wa ndani.  Maana hii ya pili ya neno “amani" haijakamilika na haiwezi kukamilisha, kwa sababu kutotulia maishani kunaweza kuwa wakati muhimu wa ukuaji. Mara nyingi ni Bwana anayepanda ndabi mwetu wasi wasi ili kwenda kukutana na Yeye na kumpata. Katika maana hiyo ni muhimu katika wakati wa makuzi; wakati inawezekana kutokea kuwa utulivu wa ndani unalingana na dhamiri iliyozikwa nyumbani na siyo ukombozi wa kweli wa kiroho. Mara nyingi Bwana lazima awe "ishara ya kupingana” (Lc 2,34-35), yeye hutikisa usalama wetu wa uwongo, ili kutupeleka katika wokovu. Na wakati huo inaonekana kuwa hauna amani, lakini ni Bwana anayetuweka kwenye njia hii ya kufikia amani ambayo Yeye mwenyewe atatupatia.

Amani ya mwanadamu tofauti na ya Bwana

Katika hatua hii lazima Papa Francisko ameendelea kusema tukumbuke kuwa  Bwana atukumbusha kuwa amani yake ni tofauti na ile ya mwanadamu na ile ya ulimwengu, wakati anaposema: "Ninawaachieni amani, ninawapa amani yangu. Siyo kama vile ulimwengu unavyowapatia, mimi nawapa”(Yoh 14: 27). Kwa maana hiyo amani ya Yesu ni amani nyingine, tofauti na ile ya kidunia. Tujiulize Papa Francisko anasema: Je amani dunia ikoje? Ikiwa tunafikiria migogoro ya kisilaha na vita,  wakati mwingine vinaishia kwa kwa kawaida kwa njia mbili: au kushinda kati ya sehemu mbili za mapginao ya vita au kufanya mkataba wa amani. "Tunaweza tu kutumaini na kuomba kwamba njia hii ya pili iweze kuchukuliwa kila wakati; Walakini, lazima tuzingatie kuwa historia ni mlolongo usiyo na mwisho wa mikataba ya amani inayokataliwa na vita mfululizo, au kwa wazo lile lile la vita kwa njia zingine au sehemu zingine. Hata katika wakati wetu, vipo vita vilivyogawanyika “vipande vipande” vinavyo endeshwa kwenye hali nyingi na kwa njia tofauti. Siyo njia hiyo na siyo amani ya Kristo!" Papa Francisko amesisitiza.

Je Bwana anatoa amani yake namna gani?

Kinyume chake Bwana anatoa amani yake namna gani? Katika kujibu swali hili Papa amesema: "Tunapaswa tusikiliza Mtakatifu Paulo ambaye anasema kuwa amani ya Kristo ni kufanya mambo mawili  kuwa kimoja (Ef 2,14), yaani kufuta uadui na kupatana. Na njia ya kutumiza katika kazi ya amani ni mwili wake. Yeye kwa hakika aliyepatanisha kila kitu na anaweka amani  yake kutokana na  msalaba kama asemavyo tena mtume Paulo (Rej. Kol 1,20).  “Na hapa ninajiuliza, Papa Francisko ameongeza, sisi sote tunaweza kujiuliza: ni nani, basi, ni “wapatanishi wa amani”  Heri ya saba ndiyo inayofanya kazi zaidi; ni kielelezo waziwazi; Ni matamshi ambayo ni ya kushangaza kwa yale yaliyotumika katika aya ya kwanza ya Bibilia wakati wa uumbaji ambao unaonyesha juhudi na bidii.

Upendo wake kimaumbile ni wa ubunifu

Upendo katika maumbile yake ni wa ubunifu, upendo ni ubunifu kila wakati na hutafuta maridhiano kwa gharama zozote Papa Francisko amefafanua.. Wanaitwa watoto wa Mungu wale ambao wamejifunza sanaa ya amani na kujikita katika matendo kwa maana wanajua kuwa hakuna maridhiano bila zawadi ya maisha, na kwamba amani lazima itafutwe kila wakati. Daima na zaidi  msisahau hii! Inapaswa kutafutwa namna hii. Hii siyo kazi ya binafsi ambayo ni matunda ya uwezo wa mtu mwenyewe, ni dhihirisho la neema iliyopokelewa kutoka kwa Kristo, ambaye ni amani yetu, ambaye alitufanya tuwe watoto wa Mungu.

Shalom ya kweli hutiririka kutoka katika amani ya Kristo

Shalòm ya kweli na ukweli wa usawa wa ndani hutiririka kutoka katika amani ya Kristo, ambayo hutoka Msalabani wake na hutoa ubinadamu mpya, ulio ndani ya umati wa jeshi lisilo na kipimo la watakatifu, wa kike na kiume wavumbuzi, wabunifu, ambao wameunda njia mpya za kupenda. Ni Watakatifu, kike na kiume ambao hujenga amani. Maisha haya kama watoto wa Mungu, ambao kwa damu ya Kristo hutafuta na kupata ndugu zao, ni furaha ya kweli. Heri wale ambao watakwenda katika njia hii. Papa Francisko amehitimisha kwa kuwatakia tena Pasaka njema kwa wote, katika amani ya Kristo!

Mara baada ya katekesi yake Papa Francisko amewatumia salam mbalimbali waamini na watazamaji wa vyombo vya habari:

Mara baada ya katekesi yake, Papa Francisko wamewasalima watu wote wanaotazama kupitia vyombo vya habari na mitando yote ya kujamii kwa lugha mbalimbali   Na katika lugha ya kutaaliano anawatakia matashi ya kuishi ujumbe wa Pasaka kikamilifu na katika imani ya ubatizo binafsi, ili kuwa mashuhuda wa furaha ya Kristo aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu.

Hatimaye salam kwa wazee na vijana, wagonjwa na wanandoa wapya: " wapendwa ninawashauri kutazana mara kwa mara Yesu ambaye ameshinda kifo na ambaye anatusaidia kupokea mateso na majaribu ya maisha kama tunu yenye fursa ya wokovu". "Bwana anawabariki na Bikira Maria awalinde”.

15 April 2020, 11:37