Papa Francisko Mtakatifu Caterina alinde Italia na Ulaya dhidi ya Janga!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mara baada ya Katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 29 Aprili 2020, amekumbuka kuwa Kanisa linaadhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Caterina wa Siena, Mwalimu wa Kanisa na Msimamizi wa Italia na Ulaya na kwa maana hiyo ameomba ulinzi wake. Hata hivyo katika misa ya asubuhi katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta likuwa ameomba kwa maombezi yake kwa ajili ya Umoja wa Ulaya. Kwa kusisitiza juu ya mtakatifu huyo kwa namna ya pekee amesema ni mfano wa mwanamke kijana na jasiri ambaye licha ya kutokujua kusoma na kuandika, aliweza kutoa wito mkubwa kwa viongozi wakuu wa raia na kidini,na hata kuwakaripia au hata kuwaonyesha upendo wa matendo halisi. Kati ya matendo hayo ni amani kati ya Italia na kurudi kwa Papa kutoka Avignon, Ufansa kuja Roma. Ni Mwanamke aliyekuwa kama chachu katika nyanja ya umma, hata katika ngazi za juu zaidi na ya Kanisa.
Papa Francisko amesema kuwa mfano wake uweze kuwasaidia kila mmoja kutambua kuungana na uthabiti wa kikristo kwa maana ya upendo wa Kanisa na uhamasishaji mwema kwa ajili ya jumuiya ya raia hasa katika kipindi cha majaribu. Tuombe Mtakatifu Caterina wa Siena alinde Italia katika janga hili na alinde Ulaya kwa sababu ni Msimamizi wa Ulaya; "alinde Ulaya nzima kwa sababu iweze kubaki imeungana".
Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu
Hali kadhalika Papa Francisko amependa kukumbuka siku kuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi wakati wa salam zake kwa lugha ya kifaransa na kusema kuwa anawakabidhi kwa Mungu watu wote ambao hawana ajira tena kutokana na janga la virusi. Bwana mpaji aweza kuwasaidia wote wenye kuhitaji na kututia moyo wa kuwasaidia.
Kusali Rosari
Mtazamo mwingine wa Papa Francisko pia ulikuwa ni mwelekezo wa uchungu mkubwa uliotokana na virusi vya covid -19 na kwa mwezi wa Mei , ameomba kwa maana hiyo kusali Rosari. Amewaashauri waamini wote kusali sala hii ya Maria kama alivyokuwa tayari amewatumia barua siku za karibuni. Ameruda hiyo wakati anasalikia lwa lugha ya kipoland. Amesisitiza kuwa kubaki ndani ya nyumba kwa sababu ya virusi, muda huo uweze kutumika vizuri kugundua uzuri wa kusali Rosati na utamaduni wa kazi ya Maria. Katika familia na hata binafsi, kila wakati kuwa na mtazamo wa sura ya Kristo na moyo wa Maria. Maombezi na umama wake uwasaidie kukabiliana na kipindi hiki maalum cha majaribu.