Tafuta

14.04.2020 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta akihitimisha kwa kuabudu Ekaristi Takatifu 14.04.2020 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta akihitimisha kwa kuabudu Ekaristi Takatifu 

Papa Francisko ameomba ili matatizo yatufanye tuungane na tushinde migawanyiko!

Katika misa ya asubuhi tarehe 14 Aprili 2020 katika kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, Papa ameomba Mungu neema ya kushinda migawanyiko katika kipindi hiki kigumu. Katika mahubiri yake anabainisha kuwa kuongoka ni kurudi kuwa mwaminifu,tabia ya kibinadamu ambayo siyo ya kawaida katika maisha yetu:uaminifu wakati mzuri na katika wakati mbaya, uaminifu kwa Mungu na kati yetu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mahubiri ya  Petro siku ya Pentekoste yalichoma moyo wa watu: “Yule mliye msulibisha amefufuka” (Mdo 2,36). Baada ya kusikia hayo walihisi kuchomwa moyo na kumwambia Petro na mitume wengine, je tunafanyeje? (Mdo 2,37). Petro yuko wazi, “tubuni. Tubuni. Badilisha maisha.  Ninyi mliopokea ahadi ya Mungu na nyinyi ambao mmekwenda mbali na Sheria ya Mungu kwa sababu ya mambo mengi, kati ya hayo ni miungu na mambo mengine mengi… ongokeni. Rudieni kuwa  waaminifu  (Mdo 2, 38).  Ndiyo mwanzo wa Mahubiri ya Papa Francisko, wakati wa misa ya asubuhi Jumanne tarehe 14 Aprili 2020 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican ambapo katika utangulizi wa Misa hiyo ameomba kusali kwa Bwana ili atujalie neema ya kuwa na umoja kati yetu na hasa katika matatizo ya kipindi hiki tuweze kugundua muungano kati yetu, umoja mbao ndiyo daima kiongozi wa kushinda  migawanyiko.

Msiwe kama mfalme Yeroboamu

Katika kuendelea na mahubiri hayo Papa Francisko anasema kuongoka maana yake ni kurudia kuwa waaminifu. Uaminifu ambao katika tabia ya mwanadamu siyo suala la kawaida katika maisha ya watu na katika maisha yetu. Daima tumezungukwa na mihadaiko ambayo inaondoa ule umakini na mara nyingi tunataka kwenda nyuma ya mihadaiko hiyo. Uaminifu unahitakiwa uwe hata wakati mzuri na hata wakati mbaya. Kufuata na ukosefu wa uaminifu na kujiona na uhakika zaidi, Papa Francisko amekumbuka juu ya kushangazwa na ufalme uliokuwa umeimarishwa na Mfalme Yeroboamu na wakati huo huo yeye hakahisi kuwa na uhakika  au kujihamini na kwenda mbali na sheria ya Bwana na Israeli nzima ikamfuata kuabudu miungu.

Tabia ya kujiamini ni ya ulimwengu mzima

Tabia ya namna hiyo ni ya ulimwengu mzima Papa Francisko amesisitiza, na kwamba mara nyingi tunapohisi kuwa na uhakika wa kufanya mipango yetu, bado tunakwenda taratibu mbali na Bwana, hatubaki kuwa waaminifu. Ndiyo, tunaweza kusema kuwa  tunakwenda mbali na Bwana taratibu, amesisitiza Papa Na hatubaki katika uaminifu. Lakini tunaweza wakati mwingine kusema…. Padre mimi sipigi magoti mbele ya miungu. Sawa labda hupigi magoti, lakini hata wewe unaitafuta na mara nyingi katika moyo wako unaabudu miungu hiyo.

Kuwa na uhakika siyo vibaya bali lazima uhakika katika Bwana

Je uhakika binafsi ni mbaya? Papa Francisko anauliza swali hili na kutoa jibu kwamba,  hapana ni neema  lakini una uhakika kwamba Bwana yupo pamoja nawe au unapokuwa na uhakika wewe unakwenda mbali ya Bwana kama Yerobohamu aliyekengeuka na kuacha kuwa mwaminifu?

Ni vigumu kubaki waaminifu

Ni vigumu sana kubaki mwaminifu, Papa amebainisha na kuelekeza kuwa katika historia yote ya Israeli na baadaye historia ya Kanisa imejaa ukosefu wa uaminifu, imejaa ubinafsi, kuwa na uhakika binafsi ambao unawafanya watu wa Mungu kwenda mbali na Bwana, kupoteza ule uaminifu, neema ya uaminifu, hata kati yetu na kati ya watu.

Uaminifu siyo fadhila yenye soko nzuri

Papa Francisko amehitimisha kwa kusema kuwa, uaminifu, siyo fadhila yenye soko nzuri, kwa njia hiyo anahimiza akisema: “ ongokeni, rudi katika uaminifu kwa Bwana”. Tuombe Bwana leo hii  hili atujalie neema ya uaminifu tupate kushukuru Bwana anapotupatia uhakika,  lakini kamwe tusihisi kuwa na  uhakika wetu binafsi na daima atujalie  neema ya kutazama upeo  zaidi ya uhakika binafsi.

14 April 2020, 11:56