Tafuta

Vatican News
Papa Yohane Pauloi Papa Yohane Pauloi 

Papa ameunda mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo I

Rais wa Mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo I ni Kardinali Petro Paroli Katibu wa Vatican ambaye katika maoni yake amebainisha juu ya mafundisho ya Albino Luciani kuwa ni mafundisho ya sasa.Ukaribu,unyenyekevu,urahisi,kuhimiza juu ya huruma ya Mungu,upendo wa jirani na mshikamano mambo ambayo bado ni ya sasa.

Vatican News

Papa Francisko ameunda mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo I kwa lengo la kukidhi pendekezo la kuunda taasisi inayokusudiwa kukuza takwimu kwa kina ya sura, mawazo na mafundisho ya Papa Pauli I, kwa jina Albino Luciani aliyechaguliwa kuwa Papa kunako tarehe 26 Agosti 1978 na kifo kifo chake kikawa  tarehe 18 Septemba 1978 ili  kukuza utafiti na usambazaji wa maandishi yake.

Mfuko huu una lengo la kulinda na kuhifadhi urithi wa utamaduni na kidini ulioachwa na Papa Yohane Paulo I katika kuanzisha na kuhamasisha kongamano, mikutano, semina, na vipindi vya mafunzo; kuanzisha hata tuzo na ufadhili wa masomo; kutunza shughuli ya kuchapisha matoleo ya matokeo ya tafiti zake binafsi, iwe ya kazi za mtu wa tatu; kutoa pendekezo kama hatua ya kumbukumbu, nchini Italia na nje ya nchi, kwa wale wanaofanya kazi katika eneo moja na kwa madhumuni sawa.

Papa Francisko amemteua Rais wa Mfuko  huo, kuwa Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ambapo katika Makala iliyotangzwa na vyombo vya habari Vatican, anabainisha kuwa “ Papa Yohane Paulo I alikuwa  na anaendelea kuwa mfano wa  kuigwa katika hatua ya kumbukumbu ya historia ya Kanisa la Ulimwengu, umuhimu wake, kama alivyokuwa amesema Mtakatifu Yohane Paulo II  hauwezi kubadilika hata kwa kipindi chake kifupi alichoishi kama Papa”

Historia ya Albino Luciani, anaandika Kardinali Parolin, “ni ile ya mchungaji aliye karibu na watu, aliyezingatia kiini cha imani na hisia maalum ya kijamii. Mafundisho yake ni ya sasa. Ukaribu, unyenyekevu, urahisi, kusisitiza juu ya huruma ya Mungu, upendo kwa jirani na mshikamano ni sifa muhimu hata za sasa”. 

“Alikuwa Askofu ambaye aliishi uzoefu wa  Mtaguso wa II wa Vatican, aliutangaza na kwa maelezo yake mafupi yalifanya Kanisa liendelee kuwa kando ya  barabara kuu kama alivyoonyesha yeye kwamba:kuelekea kwa upya katika kisima cha Injili na hali mpya ya umisionari;kushirikiana wa umoja wa maaskofu, huduma katika umaskini wa kanisa,utafutaji wa umoja wa Kikristo, mazungumzo ya kidini, mazungumzo na ulimwengu wa kisasa na mazungumzo ya kimataifa, unaofanywa kwa uvumilivu na msimamo, kwa ajili ya  haki na amani".

28 April 2020, 12:05