Msalaba wa Vijana Kutoka Panama utakabidhiwa kwa Vijana wa Jimbo kuu la Lisbon, Ureno tarehe 22 Novemba 2020: Sherehe ya Kristo Mfalme wa Ulimwengu Msalaba wa Vijana Kutoka Panama utakabidhiwa kwa Vijana wa Jimbo kuu la Lisbon, Ureno tarehe 22 Novemba 2020: Sherehe ya Kristo Mfalme wa Ulimwengu 

Siku ya XXXVII Vijana Ulimwenguni 2022: Msalaba wa Vijana

Jumapili ya Matawi, tarehe 5 Aprili 2020 ilikuwa ni siku ya vijana kutoka nchini Panama kukabidhi Msalaba wa Vijana, lakini kutokana na hali tete ya maambukizi makubwa ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19, tukio hili kwa sasa limesogezwa hadi hapo tarehe 22 Novemba 2020 wakati wa Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu. Ushuhuda!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho Ibada ya Misa Takatifu Jumapili ya Matawi, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 5 Aprili 2020 ambako amekazia: umuhimu wa utumishi katika huduma kama kielelezo cha upendo wa Mungu unao okoa, amewakumbuka na kuwashukuru wale wote waliokuwa wamejiunga pamoja naye kwa njia ya vyombo vya mawasiliano na mitandao ya kijamii. Maadhimisho ya Siku ya XXXVII ya Vijana Ulimwenguni kwa Mwaka 2022 yatafanyika Jimbo kuu la Lisbon, nchini Ureno, kwa kuongozwa na kauli mbiu “Maria aliondoka akaenda kwa haraka.” Lk. 1:39.

Jumapili ya Matawi, tarehe 5 Aprili 2020 ilikuwa ni siku ya vijana kutoka nchini Panama kukabidhi Msalaba wa Vijana, lakini kutokana na hali tete ya maambukizi makubwa ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19, tukio hili kwa sasa limesogezwa hadi hapo tarehe 22 Novemba 2020 wakati wa Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu. Katika kipindi hiki cha maandalizi, Baba Mtakatifu anawataka vijana kujenga na kudumisha ndani mwao ushuhuda wenye mvuto na mashiko; wawe ni vyombo na mashuhuda wa Injili ya matumaini, ukarimu na mshikamano; mambo msingi yanayohitajika kwa wakati huu!

Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha waamini kwamba, kwa maadhimisho ya Jumapili ya Matawi, Mama Kanisa ameanza kufuata njia ya imani, katika: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu. Kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema ambao hawatapata fursa ya kushiriki katika Liturujia mbali mbali za Kanisa, wanahimizwa na Mama Kanisa kubaki majumbani mwao katika hali ya sala, wakisaidiwa na vyombo vya mawasiliano na mitandao ya kijamii. Waoneshe umoja, upendo na mshikamano na wagonjwa pamoja na familia zao; madaktari, wauguzi na wafanyakazi katika sekta ya afya wanaoendelea kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa! Katika mwanga wa imani ya Fumbo la Pasaka, Baba Mtakatifu anawaalika waamini kusali na kuwaombea marehemu waliotangulia mbele ya haki wakiwa na tumaini la ufufuko na maisha ya uzima wa milele. Marehemu wote wakumbukwe na kuombewa!

Papa: Msalaba wa Vijana 2022

 

 

05 April 2020, 14:15