Tafuta

Vatican News
2020-04-29 Katekesi ya Papa Francisko 2020-04-29 Katekesi ya Papa Francisko  (Vatican Media)

Katekesi Papa Francisko:wakristo wanaweza kuwa kisima cha dharau!

Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;Maana ufalme wa mbinguni ni wao.Ndiyo ilikuwa heri ya mwisho kutafakariwa na kwa Papa Francisko katika katekesi yake Jumatano tarehe 29 Aprili kama mwendelezo wa tafakari za heri nyingine zilizopita,ambapo katika heri hiyo ameonya kwamba hata wakristo wanaweza kuwa kisima cha dharau wakati wakitoa msamaha ambao ni sabuni ya Kristo na ya Injili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika katekesi ya leo tunahimitisha mchakato wa safari  kuhusu Heri za Kiinjili. Kama tulivyosikia, mwishoni  inatangazwa furaha kwa walioteswa kwa haki. Heri hii inatangaza furaha ile ile ya kwanza. Ufalme wa mbinguni ni kwa wanaoteswa kama ilivyo kwa maskini wa roho; kwa  maana hiyo tunaelewa kuwa tumefikia mwisho wa mchakato wa njia ya umoja iliyowekwa katika heri zilizotengulia. Ndiyo Mwanzao wa tafakari ya Papa Francisko, katika Katekesi yake siku ya Jumatyano tarehe 29 Aprili 2020 wakiwa katika ukumbi wa Maktaba ya Kitume mjini Vatican. Katika katekesi hii, anahitimisha mwendelezo wa Heri za Mlimani alizoanza nazo katika katekesi zake zilizopita. Kabla ya kuanza katekesi, imesoma Injili ya Matayo “ Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.( Mt 5.10-12).

Mwisho wa mateso ni dhawabu

Papa Francisko akiendelea amesema ,umaskini wa roho ,  wa kilio,  wa upole,  wa kiu, wa utakatifu. Wa uhuruma , wa kutakasika katika mioyo, na katika matendo ya amani ambayo yanaweza kuepekeleka kuteza kwa sababu ya Kristo, lakini mateso haya mwisho wake ni sababu ya kufarahi na kupata dhawabu mbinguni. Njia ya Heri ni safari ya Pasaka ambayo inaongoza kutoka katika maisha kwa mujibu wa  ulimwengu kwenda kwa  kwa ujibu wa Mungu, kutoka katika maisha yanayoongozwa na  mwili  ambayo ni ubinafsi  kwenda katika yale yanayoongozwa Roho. Ulimwengu, pamoja na miungu yake , miadaiko yake  na vipaumbele vyake, haviwezi kukubali kushi aina hii ya maisha. Miundo ya dhambi, ambayo mara nyingi hutolewa na mawazo ya kibinadamu, ni ya kigeni kama ilivyo kwa Roho wa ukweli ambayo ulimwengu hauwezi kupokea (taz. Yh 14:17), inaweza tu kukataa umaskini au upole au usafi na kuthibitisha maisha kwa mujibu wa  Injili kama kosa na shida, kwa  maana hiyo kama kitu cha kukataliwa. Na ndiyo ulimwengu unafikiria, kwamba hawa ni wenye mawazo potofu. … wanafikiria hivyo wao”.

Mantiki za ulimwengu 

Ikiwa ulimwengu unaishi kwa msingi ya fedha, mtu yeyote anayeonyesha kuwa maisha yanaweza kutimizwa kwa njia ya  zawadi na kujinyima  inakuwa kero katika  mfumo wa uchoyo,a amesema Papa. Neno hili "kero" ni muhimu, kwa sababu ushuhuda wa Kikristo peke yake, ambao hufanya vizuri sana kwa watu wengi kwa sababu wanamfuata, huwachukiza wale walio na mtazamo wa kidunia. Wanaishi kama kukemea.  Ubapoibuka utakatifu  na maisha ya watoto wa Mungu yanajionesha, katika uzuri huo kuna kitu kisichofurahisha  ambacho kinahitaji msimamo: ama kujiruhusu mwenyewe kuhojiwa na kufunguliwa katika wema au kukataa hiyo nuru na kuifanya mioyo kuwa migumu hadi kufiika upinzani mkali na ghadhabu (taz Sap 2,14-15). Papa Francisko amethibitisha kwamba “inashangaza kuona jinsi gani katika mateso ya wafia dini , inazidi kuongezika ugumu na ghadhabu. Inatosha kutazama mateso ya karne ya mwisho iliyopita ya kipindi cha udikteta Ulaya: Jinsi ilivyofikia gadhabu dhidi ya wakrisot na dhidi ya ushuhuda wa kikristo na dhidi ya ushujaa wa Wakristo”.

Walioteswa wanafurahi kwa sababu gani?

Papa Francisko amebainisha kuwa lakini hii inaonyesha kuwa mchezo wa mateso pia ni mahali pa ukombozi kutoka kwa kujitiisha kwa mafanikio ya ulimwengu, ubatiri  na miadahiko  ya ulimwengu. Je! Ni nini kinachofurahisha wale ambao wamekataliwa na ulimwengu kwa sababu ya Kristo? Wanafurahi kwa sababu wamepata kitu cha thamani zaidi kuliko ulimwengu wote. Kiukweli “kuna faida gani mtu kupata ulimwengu wote na kupoteza maisha?” (Mk 8,36). Kuna faida gani? Papa Francisko amebainisha ilivyo na uchungu kukumbuka kipindi hiki ambacho kuna wakristo wengi wanateswa katika sehemu mbalimbali za dunia, na tunapaswa kutumainia na kusali ili mapema mateso hayo yaishe. Ni wengi. Mashuhuda wa leo ni zaidi ya mashuhuda wa karne za kwanza. Tunaonesha ukaribu wetu na hawa kaka  na dada: sisi ni mwili mmoja,na Wakristo kwa hawa ambao tunashirikia damu wa mwili wa Kristo ambao ni Kanisa.

Kuwa waangalifu:chumvi inaweza kupoteza ladha

Lakini lazima pia tuwe waangalifu kwani tusisomeheri hii katika  ufunguo wa waathirika, hasa wa wakutaka wenyewe. Kiukweli,siyo dharau zote kwa watu ni sawa kwa kila wakati na mateso  Kwa kuthibitisha, : mara tuada ya Yesu kusema kwamba Wakristo ndiyo chumvi ya dunia, na analionya dhidi ya hatari ya kupoteza ladha, vinginevyo chumvi haisaidii kitu chochote inahitajika kutupwa mbali na kukanyagwa na watu (Mt 5: 13). Kwa njia hiyo Papa Francisko amesema kuna dharau ambayo ni kosa letu wakati tunapoteza ladha ya Kristo na Injili. Ni lazima kuwa waamni katika nia ya unyenyekevu wa Heri kwa sababu ndiyo inapeleka kuwa katika Kristo na siyo katika dunia. Inabidi kukumbuka mchakato wa safari ya Mtakatifu Paulo  alipokuwa akifikiri kuwa mwenye haki lakini kwa hakika alikuwa ni mtesaji, lakini alipogundua kuwa mtesaji akageuka kuwa mtu wa upendo ambaye alikabiliana kwa fuaha masumbuko na mateso aliyopata( taz Kol 1,24).

Udhihirisho wa maisha mapya

Kwa mujibu wa kutengwa na kuteswa, ikiwa Mungu hutupatia neema, na kutufanya kufanana na Kristo aliyesulubiwa na kutuunganisha na mateso yake, ni udhihirisho wa maisha mapya. Maisha haya ni sawa na yale ya Kristo, ambaye kwa sisi na kwa wokovu wetu alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu" (taz. 53: 3; Matendo 8: 30-35). Kukaribisha Roho wake kunaweza kutuongoza kuwa na upendo mwingi mioyoni mwetu kiasi  kwamba tunatoa maisha kwa ulimwengu bila krubuniwa na udanganyifu wake na kuukubali. Kurubuniwa na ulimwengu ni hatari. Mkristo hujaribiwa kila wakati kufanya maelewano na ulimwengu, na roho ya ulimwengu. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema Kukataa ulagahi huu na kwenda  katika njia ya Yesu Kristo  ndiyo maisha ya Ufalme wa mbinguni, furaha kuu, furaha ya kweli. Na baadaye  katika mateso daima kuna uwepo wa Yesu ambaye uongozana nasi, uwepo wa Yesu ambaye hutufariji na nguvu ya Roho ambaye hutusaidia kwenda mbele. Tusikate tamaa wakati maisha yaliyo thabiti ya Injili yanavutia mateso ya watu. Kuna Roho ambaye anatuunga mkono katika njia hii.

29 April 2020, 14:03