Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko: Sala kwa Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa: Mei 2020 Baba Mtakatifu Francisko: Sala kwa Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa: Mei 2020  (ANSA)

Papa Francisko: Sala kwa Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa

“Bikira Maria unang’aa daima katika njia yetu kama alama ya wokovu na matumaini. Sisi tunakutumainia Wewe, Afya ya wagonjwa, ambaye chini ya Msalaba ulishiriki mateso ya Yesu, ukabaki thabiti katika imani yako. Wewe ambaye ni wokovu wa Warumi, unatambua ni kitu gani ambacho tunakihitaji kwa wakati huu na tuna matumaini kwamba, utaweza kutuombea, kama ilivyokuwa kule Kana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ifuatayo ni Sala ya Pili kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko kama kiambatanisi cha Barua yake kwa Waamini Wote kwa ajili ya Mwezi Mei, 2020 ambao kadiri ya Mapokeo ya Kanisa umetengwa maalum kwa ajili ya Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa. “Bikira Maria unang’aa daima katika njia yetu kama alama ya wokovu na matumaini. Sisi tunakutumainia Wewe, Afya ya wagonjwa, ambaye chini ya Msalaba ulishiriki mateso ya Yesu, ukabaki thabiti katika imani yako. Wewe ambaye ni wokovu wa Warumi, unatambua ni kitu gani ambacho tunakihitaji kwa wakati huu na tuna matumaini kwamba, utaweza kutuombea, kama ilivyokuwa kwenye Harusi ya Kana ya Galilaya, furaha iweze kurejea tena baada ya kipindi hiki cha majaribu makubwa.

Utusaidie Bikira Maria wa Upendo wa Mungu, utuimarishe katika kutekeleza mapenzi ya Mungu kwa kufanya kile ambacho Yesu atasema, kwani amejitwika mateso na kuchukua machungu yetu na kutuongoza, ili kwa njia ya Msalaba, tuweze kufikia furaha ya Ufufuko. Amina. Tunakimbilia ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu. Usitunyime tukiomba katika shida zetu, tuopoe siku zote kila tuingiapo hatarini, Ee Bikira Mtukufu na mwenye baraka. Amina.

Papa: Sala
25 April 2020, 13:49