Tafuta

Vatican News
Virusi vya Corona, COVID-19: Papa Francisko asimamisha shughuli za Mahakama za Vatican hadi tarehe 3 Aprili 2020. Virusi vya Corona, COVID-19: Papa Francisko asimamisha shughuli za Mahakama za Vatican hadi tarehe 3 Aprili 2020.  (Vatican Media)

Virusi vya Corona: Vatican yasitisha shughuli za Mahakama

Papa Francisko ameamua kuanzia tarehe 18 Machi 2020, kusimamisha shughuli zote za Mahakama za Vatican, hadi hapo tarehe 3 Aprili 2020. Tahadhari hii imechukuliwa pia na Serikali ya Italia. Lakini, shughuli za uchunguzi wa makosa mbali mbali zitaendelea kama kawaida. Shughuli za dharura Kimahakama zinaweza kuendelea kwa ruhusa na uratibu wa Rais wa Mahakama za Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kusoma alama za nyakati sanjari na kuzingatia hali halisi ya mlipuko wa Virusi vya Corona, COVID-19 na athari zake katika jamii, ameamua kuanzia tarehe 18 Machi 2020, kusimamisha shughuli zote za Mahakama za Vatican, hadi hapo tarehe 3 Aprili 2020. Tahadhari hii imekwisha kuchukuliwa pia na Serikali ya Italia. Lakini, shughuli za uchunguzi wa makosa mbali mbali zitaendelea kama kawaida. Pamoja na kuzingatia kanuni, masharti na itifaki ya kupambana na Virusi vya Corona, COVID-19, shughuli za dharura Kimahakama zinaweza kuendelea kwa ruhusa ya Rais wa Mahakama, kwa kuratibu muda wa kuingia na kutoka.

Agizo hili kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko, limetolewa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwa vyombo vya mawasiliano ya jamii. Virusi vya Corona, COVID-19 vinaendelea kusababisha majanga makubwa pamoja na kugumisha maisha ya watu wengi duniani!

Mahakama

 

19 March 2020, 13:54