Tafuta

Vatican News
Tarehe 27 Machi 2020: Sala katika Uwanja wa Mtatifu Petro na Baraka ya Urbi et Orbi Tarehe 27 Machi 2020: Sala katika Uwanja wa Mtatifu Petro na Baraka ya Urbi et Orbi  (ANSA)

Sala ya Papa Francisko katika janga la corona:Bwana usituache katika dhoruba!

Papa Francisko ameongoza kipindi cha sala cha kihistoria katika uwanja wa Mtakatifu Petro ukiwa mtupu,lakini uliokuwa unafuatiliwa na wakatoliki na waamini wengine duniani ili kuomba Mungu aweze kusitisha janga hili ambalo linahatarisha kuenea kwa covid-19.Wewe,Bwana,usituache katika wimbi la dhoruba.Rudia tena:kusema Ninyi msiogope.Na sisi,pamoja na Petro tunaweka wasiwasi wote kwako,kwa sababu unatujali.Imefuata kuabudu na Baraka ya Urbi et Orbi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ilikuwa ni saa 12 jioni masaa ya Ulaya tarehe 27 Machi 2020 ambao Papa Francisko ameanza kusali na  waamini wote dunia katika sala ya pamoja na baadaye kufuatia baraka ya 'Urbi et Orbi' katika kipindi hiki cha dharura ya virusi vya corona vilivyonea duniani kote.  Tafakari yake imeongozwa na Injili ya Marko sura ya nne na kuanza kusema  “Siku ile kulipokuwa jioni (Mk 4,35). Ndivyo inaanza Injili ambayo tumesikia”. Kwa wiki hizi utafikiri umeshuka usiku. Giza nene limetawala katika maisha yetu na kujaza kila kitu katika ukimya na utupu wa upweke ambao umegandamiza kila kitu katika hatua zote inasikika katika hewa na kuhisi katika ishara. Halio hii inajionesha katika mitazamo. Tumejikuta tunaogopa na kuhangaika.

Kama wafuasi  katika Injili sisi tumejikuta tunaogopeshwa na dhoruna kali isiyotarajiwa. Tumejikuta tuko katika mtumbwi mmoja, sisi wote tukiwa wadhaifu na bila kuwa na mwelekeo, lakini wakati huo huo, ni muhimu na lazima wote tumealikwa kubaki pamoja  kwa maana wote  ni wahitaji na kufarijiana pamoja. Katika mtumbwi huu tuko ndani mwake wote. Kama wafuasi ambao walizungumza kwa sauti moja na katika uchungu wakisema "tumeangamia"(Mt.4, 38) Hata sisi tumetambua kuwa hatuwezi kwenda mbele kila mmoja peke yake, bali kwenda pamoja. Ni rahisi kujitambua katika simulizi hii. Kile ambacho kinaonekana kuwa kigumu ni kuona ule mtindo wa Yesu. Wakati mitume wanaonekana kuwa na wasiwasi, Yeye alikuwa amelala usingizi, pembeni mwa mtumbwi ambao ulikuwa karibu uzame. Je anafanya nini licha ya machafuko hayo?,Amelela kwa utulivu, akiwa na matumaini kwa Baba. Papa Francisko ameongea hii ndiyo moja ya sehemu pekee katika Injili tunayoiona Yesu akiwa amelala.

Alipozinduliwa na baada ya kutuliza dhoruba  na maji, akawageukia mitume wake kwa sauti ya kukaripia “Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? (Mt 4, 40),Papa Francisko amesema kuwa tujaribu kuelewa. Ni jambo linahusu ukosefu wa imani kwa wafuasi ambao wanakwenda kinyume na imani katika Yesu. Lakini wao hawakuwa wameacha kuamini katika Yeye  kwa maana hakika tunawaona wanamwambia, “Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? ( 38). Wanafikiri kwamba Yesu hawajali  na hawatunzi. Kati yetu, katika familia zetu, moja ya mambo ambayo yanaumiza ni pale tu tuposikia wakisema “ hunijali” . Ni sentensi ambayo inatoka katika dhoruba ya moyo na ambayo ilimwandama hata Yesu. Japokuwa hakuna yoyote anayejali  sisi zaidi ya Yeye. Na hii inajionesha wazi kwa uhakika mara moja walipomwamsha aliwaokoa mitume wake wasio na imani.

Dhoruba inaficha kuathirika kwetu na inafunua ule ulaghai, ule ujujuu wa usalama ambao sisi tumeujenga katika ratiba zetu, katika mipango yetu katika mazoea yetu na vipaumbele vyetu. Inajionesha jinsi gani tumejiachia kulala na kuacha kila ambacho kinamwilisha, kinasaidia na kutoa nguvu ya maisha yetu, na katika jumuiya zetu. Dhoruba inafunua wazi mapendekezo yote na kufunga na kusahau kila ambacho kunamwilisha roho ya watu wetu; ile hali  ya kutaka kugandishwa na mazoea ya kijujuu “tuokoe”, na  wasio kuwa na uwezo kurudia mizizi yetu ilikukabiliana magumu haya. Katika dhoruba ilitokea jambo moja la kile tunachoitwa mazoea na kufunika ubinafsi wetu ambao daima ni wasiwasi wa sura picha binafsi na imebaki imefunikwa kwa mara nyingine ile iliyobarikiwa na ambayo ya ni ya pamoja na hatuwezi kujiondoa kama ndugu.

Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

Papa Francisko ameendelea kusema: Ee  Bwana Neno lako jioni hii linatushangaza na linatugusa sisi sote. Katika dunia yetu , ambayo Unaipenda zaidi yetu sisi tumekwenda mbele kwa kasi , kwa kuhisi kuwa na nguvu na wenye uwezo wa yote. Wenye uchu wa kupata , tumejiachia kutawaliwa na mambo mengi na kuzugwa na haraka. Hatukuitikia wito wako, mbele ya vita hatukuweza kuzuia, katika ukosefu wa haki wa sayari na hatukusikiliza kilio cha masikini na cha sayari ambayo imeugua. Tumeendelea mbele tukifikiria kubaki daima wenye afya katika dunia ambayo imeugua. Sasa Bwana wakati tupo bahari iliyochafuka tunakuomba “amka Bwana"

Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

Bwana tunatoa wito wa imani. Siyo tu kwamba wewe upo, lakini uje wewe na tunakuamini. Katika Kipindi hiki cha Kwaresima tunasikia wito wako wa dharura, usemao "nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote". Unatuita kupokea kipindi hiki cha majaribu kama kipindi cha uchaguzi. Siyo kipindi tu cha kuhukumu, bali cha hukumu yetu. Kipindi cha kuchagau ni kipi nyenye maana na kipi kinapita, kutenganisha kile ambacho ni muhimu na kile ambacho siyo. Ni wakati wa kuweka upya kazi ya maisha kwako, Bwana, na kwa wengine.Tunaweza kutambua watu wengi  wa kuigwa ambao ni wasindikiza wa safari katika hofu wanaweza kutoa maisha yao. Ni nguvu inayofanya kazi ya Roho mwenye uwezo wa kuondoa , kuthamanisha na kuonesha jinsi ambavyo maisha yetu yamesukana na kusaidiwa na watu wa kawaida na mbao kwa kawaida wamesahuliwa. Wale ambao hawaonekani katika vivhwa vya habari za magazeti na hata katika makala, wala kuonekana katika mtindo mipya ya mwisho, bali bila shaka wakiwa wanaandika  leo hii matukio wazi ya maisha yetu.

Hawa ni Madaktari, wauguzi, wafanyakazi wa supermarket, polisi, watu wanaotunza wazee, wa vyombo vya uchukuzi, vyombo vya kisheria, watu wa kujitolea, mapadre , watawa na watu wengi ambao wametambua kuwa hakuna mtu yoyote anayejiokoa mwenyewe. Mbele ya mateso, mahali mabapo kipimo cha kweli na watu wetu tunagundua na kufanya uzoefu wa sala ya kikuhani ya Yesu isemayo ” ili wote tuwe wamoja (Yh 17,21). Je Ni watu wangapi kila siku wanafanya uzoefu wa uvumilivu na wanaeneza matumaini kwa kuwatunza na siyo kuchanganya watu  bali kuwa waajibikaji?. Mapadre wangapi, mama, babu, bibi ,walimu wanaonesha watoto wetu kwa ishara ndogo za kila siku, jinsi gani ya kukabiliana na kukatisha hiki kipeo na kukabiliana na hali halisi, kwa kuinua mtazo juu , kutoa chachu ya sala. Ni watu wangapi wanasali , wanatoa sadaka na kuomba kwa ajili ya wema wa wote. Sala na huruma ya kimya ndizo silaha za ushindi.

Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

Mwanzo wa imani ni kujitambua kuwa sisi ni wahitaji wa wokovu. Sisi hatujitoshelezi, peke yetu tunazama. Tunahitaji Bwana kama wale wale wataalam wa nyota. Tumkaribishe Yesu katika mtumbwi wa maisha yetu. Tumkabidhi hofu zetu, kwa sababu Yeye azishinde. Kama wafuasi tunafanya uzoefu wa maisha yetu ya hofu kwa sababu  tuko naye ndani ya mtumbwi na hatuzami. Kwa sababu hii ndiyo nguvu ya Mungu,  ya pindua kila kitu kinachotokea kwetu kuwa kizuri, hata iliyo mbaya. Yeye huleta amani katika dhoruba zetu, kwa sababu katika Mungu maisha hayafi kamwe. Bwana anatupa changamoto na katikati ya dhoruba yetu, anatualika kuamka na kuanza mshikamano na tumaini lenye uwezo wa kutoa uthabiti, msaada na maana katika masaa kama haya wakati kila kitu kinaonekana kuwa kimezama. Bwana aweze kuamsha  tena na kufufua imani yetu ya Pasaka. Tunayo nanga: katika msalaba tuliokombolewa. Tunayo helmeti, katika Msalabani tumekombolewa. Tunalo tumaini kwa maana katika msalaba wake tumeponywa na kukumbatiwa ili pasiwepo chochote na hakuna mtu atakayotutenganisha na upendo wake wa ukombozi.

Bado tunasikia wito wako wa wokovu

Katikati ya kutengwa ambamo tunateseka kutokana na ukosefu wa upendo na kukutana, tunakabiliwa na ukosefu wa vitu vingi, tunasikiliza tena wito ambao unatuokoa kuwa, amefufuka na anaishi karibu yetu. Bwana anatuomba  kutoka katika msalaba wake ili kupata uzima unaotungojea, kuangalia kwa wale wanaotuliza, kuimarisha, kutambua na kuhimiza neema inayoishi ndani yetu. Tusiwazimie moto uliokufa  ili wasije kuwa wagonjwa kamwe na tumaini limewashwe tena(taz. Is 42,3). Kukumbatia msalaba wake kunamaanisha kupata ujasiri wa kukumbatia mambo yote yaliyo kinyume na wakati huu. Ni kumwachia wakati huu wasiwasi wetu juu ya uweza na milki yake ili kutoa nafasi kwa ubunifu ambao ni ni Roho tu anaweza kuamsha tena. Inamaanisha kupata ujasiri wa kufungua nafasi ambapo kila mtu anaweza kuhisi kuitwa na kuruhusu njia mpya za ukarimu, udugu na mshikamano. Katika msalaba wake tuliokombolewa ili kuupokea kwa matumaini na kuiruhusu tuimarishwe na kusaidia hatua na njia zote zinazoweza kutusaidia kujiweka salama na kutulinda. Kumkumbatia Bwana ili kuweza kukumbatia tumaini ndiyo nguvu ya imani, ambayo inatoa uhuru dhidi ya woga na inatoa tumaini.

Mbona unaogopa? Je! Bado huna imani?

Ndugu na kaka na dada wapendwa, Papa Francisko hatimaye amesema, kutoka mahali hapa, panapo simulia  imani za mwamba wa Petro usiku wa leo ningependa kuwakabidhi ninyi nyote  kwa Bwana, kupitia maombezi ya Mama yetu, afya ya watu, nyota ya bahari katika dhoruba. Kutoka kwa katika mzunguko wa uwanja huu ambao unakumbatia  Roma na ulimwengu, baraka za Mungu ziwashukie juu yenu na kuwakumbatia kwa utulivu ... Bwana, ubariki dunia, ipe afya miili na faraja katika mioyo. Unatuomba tusiogope. Lakini imani yetu ni dhaifu na tunaogopa. Lakini Wewe, ee Bwana usituache katika dhoruba kuu ya upepo. Rudia tena kutwambia: "Msiogope ninyi"(Mt 28.5). Na sisi pamoja na Petro  tunaweka  wasiwasi wote kwako, kwa sababu unatujali (taz.1 Pt 5,7).

PAPA URBI ET ORBI
27 March 2020, 19:30