Tafuta

Vatican News
Waamini waliokuwa Vatican tarehe 8 Machi kuungana na sala ya Malaika wa Bwana na Papa Francisko Waamini waliokuwa Vatican tarehe 8 Machi kuungana na sala ya Malaika wa Bwana na Papa Francisko   (ANSA)

Papa Francisko:Yesu hachagui kutokana na mantiki zetu!

Ni katika Maktaba ya Jumba la Kitume ambapo sala ya Malaika wa Bwana ya Papa Francisko imesikika.Tukio hili ni kutokana na kuenea kwa maambukizi ya Covid 19.Katika kiini cha tafakari ya siku ni uchaguzi wa pendo wa Yesu ambaye anaita wafuasi wakae naye karibu.Papa Franciso hakuvumilia kukaa ndani ya “kiota”kama alivyo tafisri,baada ya sala alichungulia dirishani na kuwasalimia waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Imekuwa ni Sala ya Malaika wa Bwana isiyo kuwa ya kawaida katika Jumapili ya pili ya Kwaresima tarehe 8 Machi 2020 katika kipindi ambacho ulimwenguni  kote watu wote wapo wanaendelea kuungana pamoja katika kupambana dhidi ya kuenea kwa vurusi vya corona (COVID-19)  ambayo tayari vimeisha waambukiza watu zaidi ya miamoja elfu. Ilikuwa ni saa sita kamili  ambayo  kama kawaida mjini Vatican ni muda wa kusali sala ya Mama Maria, lakini Dirisha ambalo Papa huwa anazungumzia na kubariki dunia nzima, katika Jumapili hii halikuwa wazi mbele ya Uwanja wa Mtakatifu Petro. Kinyume chake ilikuwa ni kutazama uso wa Luninga ili kuweza kuona ndani ya Jumba Kuu la Kitume mahali ambapo Papa Francisko alikuwa amekaa. Hata hivyo waamini wote walikuwa  tayari wameandaliwa kwa njia ya msemaji Mkuu wa vyombo vya habari Vatican kuhusiana na tukio hili  kufuata na kufuata taratibu zote zilizotolewa na mamlaka  ili kuzuia maambuziki ya covid 19, iwe  kwa upande wa mamlaka ya Italia pamoja na Vatican kwa  pamoja katika ushirikiano huo.

Papa Francisko akianza tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana amesema:  “Ni jambo kidogo la kushangaza katika sala hii ya Malaika wa Bwana leo hii, Papa akiwa amefungwa katika maktaba ya vitabu lakini ninawatazama na niko karibu nanyi. Ninapendelea kuanza kutoa shukrani, kwa kundi ambalo lipo katika uwanja na ambao wanaonesha kupambana kwa ajili ya waliosahauliwa wa Idlib. Asante kwa kile mnachofanya. Lakini namna  ya kusali leo hii sala ya Malaika wa Bwana, tunaifanya ili kutumiza na kuweza kuzuia makundi ya umati wa watu, ambayo yanaweza kusababisha kuenea zaidi  kwa virusi. Papa Francisko akiendelea amesema, katika Dominika ya Pili ya Kwaresima ( Mt 17,1-9) inawakilishwa na  simulizi ya “Kugeuka sura  kwa Yesu”.  Yeye aliwapeleka Petro, Yakobo na Yohane na kupanda nao kilima cha juu, ishara ya ukaribu na Mungu ili kuwafungulia uewelewa mpana wa fumbo la Yeye binafsi na kwa jinsi  gani anapaswa ateseke, afe na baadaye afufuke, lakini wao hawakuweza kukubali matarajio hayo. Kwa maana hiyo mara baada ya kufika kwenye mlima, Yesu alijikita katika sala ya kina na kugeuka sura yake mbele ya mitume hao watatu. Uso wake, Injili inasema, ulikuwa unang’aa kama jua na mavazi yake yalimelemeta sana kama mwanga

Kwa njia ya tukio hili la kushangaza la Kugeuka Sura, Mitume watatu wanaalikwa kutambua Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu  na mwenye kuangazwa na utukufu. Hawa katika dhamiri yao sasa wanamtambua Mwalimu wao na kuelewa kuwa mtazamo wa kibinadamu hauwezi  kabisa kuelezea uhalisi wake wote;  macho yao yalioneshwa ukuu usio wa kidunia na umungu wa Yesu.  Na kutoka juu mbinguni ndipo ikasikika sauti isemayo “ Tazameni huyo ni Mwanangu Mpendwa wangu (…) msikilizeni Yeye. Ni Baba wa Mbinguni anayethibitishwa kuvikwa kwake na ambaye tayari alikuwa amethibitishwa pia siku ya Ubatizo wake katika Mto wa Yordan na anawaalika wafuasi wamsikilize na kumfuata. Ni lazima kusisitiza kuwa katika kundi la kumi na mbili, Yesu aliwachagua watu watatu, Petro, Yakobo na Yohane. Hawa ndiyo waliopata bahati ya kushuhudia kugeuka kwake sura. Lakini ni kwa nini alifanya uchaguzi huo wa watatu. Je walikuwa ni watakatifu zaidi? Hata hivyo Petro katika siku ya mateso, atamkana; ndugu wawili Yakobo na Yohane watamuomba  Yesu baadaye waweze kupata nafasi za kwanza katika Ufalme wa Mungu ( Mt 20, 20-23).  Yesu lakini hachagui kutokana na mantiki zetu. Bali kwa mujibu wa ishara  ya upendo. Upendo wa Yesu hauna kipimo; ni upendo tu na Yeyey anachugua ishara ya Upendo tu.

Hili ni chaguo la bure, bila kulazimishwa na kitu fulani, anaanzisha jambo lake  kwa uhuru, urafiki wa Mungu ambaye haombi lolote la kubadilishana nalo.  Kama alivyowaita wafuasi wake watatu , ndivyo hata leo hii anawaita baadhi ili kukaa naye karibu, kwa ajili ya kushuhudia. Kuwa shuhuda wa Yesu ni zawadi ambayo tumepewa bure bila kustahili. Tunahisi kutotendewa hivyo japokuwa hatuwezi kurudi nyuma kwa njia ya sahamani kutokana  ukosefu wa uwezo wetu. Papa Francisko amesema “sisi hatukwenda juu ya mlima Tabor, hatukuona kwa macho yetu uso wa Yesu uking’ara kama jua. Licha ya hayo yote, tumekabidhiwa Neno la Wokovu ambalo tumepewa kwa imani na tumelishuhuhudia katika  mitindo  tofauti, furaha ya kukutana na Yesu . Hata sisi Yesu anatwambia “Simameni msiogope” ( Mt 17,7). Katika ulimwengu huu unaoonyesha ishara za ubinafsi na tamaa  mwanga wa Mungu umetiwa kivuli na wasi wasi za kila siku. Papa Francisko anongeza kusema “ tunasema kila siku sina nafasi ya kusali, sina uwezo wa kufanya huduma katika parokia, kujibu maombi ya wengine … Lakini hatupaswi kusahau kuwa Ubatizo tuliopokea ndiyo unatenda ushuhuda  na si kwa ajili ya uwezo wetu bali kwa ajili ya zawadi ya Roho. Katika kipindi hiki muafaka cha Kwaresima, Bikira Maria atusadie kuwa na upole ambao ndiyo wa lazima kwa ajili ya kutembea kwa hakika katika njia ya uongofu.

09 March 2020, 10:39