Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anawakumbua watu wanoteseka na vita huko Siria kwa namna ya pekee mji wa Idlib na pia kuwaombea wagonjwa wa mlipuko wa virusi corona Papa Francisko anawakumbua watu wanoteseka na vita huko Siria kwa namna ya pekee mji wa Idlib na pia kuwaombea wagonjwa wa mlipuko wa virusi corona 

Papa Francisko:Toeni kipaumbele hali halisi ya Siria!

Kwa mara nyingine tena Papa Francisko ametoa wito wake wa nguvu kutokana na uelewa wa hali halisi isiyo kuwa ya kibinadamu kwa mamia elfu ya raia ambao bado nchini Siria wanaendelea kuteseka kwa vita visivyo na mwisho na kwa namna ya pekee katika mji wa Idlib na Magharibi mwa nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana  Papa Francisko akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume tarehe 8 Machi 2020 katika Dominika ya Pili ya Kwaresima Papa Francisko amerudia kukumbuka vita nchini Siria na majanga ya kibinadamua ambayo baada ya miaka tisa bado yanaendelea kutesa watu hasa katika Kaskazini Magharibi mwa nchi nchi hiyo. Papa Francisko amewasalimia watu wote kwa namna ya pekee washiriki wa Mafunzo “walezi wa mtindo mpya ya mawasiliano” na waamini kutoka pande zote waliokuwapo katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Amewasalimia waamini na zaidi kikundi na makundi ambayo yanajikita katika jitihada za mshikamano kwa ajili ya  watu wa Siria hasa kwa wakazi wa mji wa Idlib na Kaskazini magharibi wa Siria. “Niko nawatazama kutoka hapa mkilazimika kikimbia kutokana na kuongezeka kwa vita”. Amesema Papa. Aidha  Papa Francisko amepyaisha wito wake kwa nguvu  kutokana  na uelewa wa uchungu mkubwa katika hali hiyo isiyo ya kibinadamu ambayo inasababaishawatu wengi kuteseka  miongoni mwao wakiwemo watoto wanao hatarisha maisha yao. Papa anasema hawapawi kuondoa mtazamo mbele ya kipeo hiki cha kibinadamu, badala yake ni kutoa kupaumbele  zaidi ya mambo mengine.  Papa Francisko ameomba sana kusali kwa ajili ya watu wanaoteseka wa Kaskazini Magharibu mwa Siria na mji wa Idlib.

Ukaribu wa Papa kwa wenye maambukizi ya Corona na wahudumu. Papa Francisko ameonesha ukaribu wake kwa watu wanaoteseka na maambukizi ya sasa ya mafua ya virusi cya Corona na wale wote ambao wanashughulikia  au kutoa huduma kwa ajili yao. Anaungana na ndugu maaskofu kuwatia moyo waamini wote ili waishi kipindi hiki kigumu kwa nguvu ya imani, uhakika wa matumaini na upendo wa hisani. Kipindi cha Kwaresima kitusaidie kuwapa watu wote maana ya kiinjili hata katika kipindi cha majaribu na uchungu, amesema Papa Francisko na kuhitimisha kwa kuwatikia mlo mwema na Dominika njema!

09 March 2020, 10:53