Tafuta

Vatican News
Tarehe 11 Machi 2020 Papa Francisko ametoa tafakari ya Katekesi yake katika chumba cha Jumba la Kitume kufutatia na harakati za kuzuia maambuzi ya virusi vya corona. Tarehe 11 Machi 2020 Papa Francisko ametoa tafakari ya Katekesi yake katika chumba cha Jumba la Kitume kufutatia na harakati za kuzuia maambuzi ya virusi vya corona.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Mungu anatambua kilio cha wateswa!

Katekesi ya Papa Francisko iliyotangazwa mbashara akiwa ndani ya Ukumbi wa Jumba la Kitume Vatican kufuatia na haraka za kupambana kuenea kwa virusi vya Corona,imejikita kufafanua Heri ya Nne ya mlimani,inayohusu njaa na kiu ya haki.Injili ni kubwa zaidi ya haki Papa amebainisha na kwamb inaweza kweli kupatikana katika moyo wa mwandamu hata kama yeye hatambui.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika maandiko matakatifu, tunaona kilelezo cha kiu ya kina zaidi ya kile ya kimwili na ambacho ni shauku inayochukua nafasi katika mzizi wa uhai wetu. Ni katika tafakari ya Papa Francisko Jumatano 11 Machi 2020 kama sehemu ya katekesi yake bila waamini iliyotangazwa mbashara kutoka Chumba cha Jengo la Kitume kutokana na harakati za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Akianza tafakari hii amesema: Katika katekesi ya leo tuendelee kutafakari njia angavu ya furaha amabayo Bwana anatukabidhi katika heri na mbali mbali ka maana hiyo tuongeze ile ya Nne isemayo “Heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa”( Mt 5,6). Papa Francisko amesema tulikuwa tayari tumekutana na umaskini wa kiroho na machozi; sasa ni kukabiliana kwa undani na aina ya udhaifu ambao unatokana na njaa na kiu. Njaa na kiu ni mahitaji msingi ya kuishi. Hii lazima kusisitiza kuwa si shauku ya kawaida kwa ujula bali ni mahitaji ya kweli ya maisha ya kila siku na kama umwilisho.

Lakini ina maana gani ya kuwa na njaa na kiu ya haki? Siyo kuzungumza juu ya wale kwa hakika ambao wanataka kulipza kisasi na badala yake katika Heri iliyotanguliwa ilikuwa imeelezewa vema juu ya wapole. Kwa hakika haki inakosa kwa ubinadamu; na katika jamii ya kibinadamu, ipo dharura ya usawa, ya ukweli na haki kijamii. Ni lazima kukumbuka mabaya yanayowakumba wanawake na wanaume wa dunia yanafikia katika moyo wa Mungu Baba. Ni Baba yupe hasiweze kuteseka kwa ucuhungu wa wanae?

Maandiko matakatifu yanasimulia uchungu wa maskini na wanaokandamiza kuwa Bwana anautambua na kushirikishana nao.  Bwana akasema, “Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri,(Kut 3,7-10)”. Mungu alishuka kuwakomboa watu wake. Papa amesema. Lakini njaa na kiu ya haki ambayo Bwana anasema na sisi ni kubwa zaidi kuliko hitaji halali la haki ya mwanadamu ambayo kila mtu hubeba moyoni mwake., Yesu anasema “Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mt 5,20).  Hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mungu kwa mujibu wa barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto (1 Kor 1,30).

Katika maandiko matakatifu, tunaona kilelezo cha kiu ya kina zaidi ya ile ya kimwili na ambayo ni shauku inayochukua nafasi katika mzizi wa uhai wetu. Katika Zaburi inasema “ Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Mababa wa Kanisa wanazungumza juu ya mahangaiko ambayo yamo ndani ya mtu. Kwa mfano Mtakatifu Agostino anasema “kwa kuwa umetuumba kwa ajili yako na moyo wetu hautatulia  mpaka ustarehe ndani mwako”. Papa aidha ameongeza kubainisha kwamba:“Kuna kiu ya ndani, njaa ya ndani na  wasiwasi.

Katika kila moyo, hata katika mafisadi  mbali  na mema, imefichwa ile nuru hata kama ni ndogo inayopatikana katika kivuli cha udanganyifu na makosa, lakini daima kuna kiu ya kutaka ukweli na wema ambao ni kiu ya Mungu. Ni Roho Mtakatifu ambaye anaamsha kiu hii. Yeye ni maji hai, yanayonyunyiziwa katika vumbi letu, ni Yeye pumzi la uumbaji ambayo ilitoa maisha. Kwa maana hiyo Kanisa limeitwa kutangaza kwa watu wote Neno la Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kwa sababu Injili ya Yesu Kristo ndiyo haki kubwa zaidi inayoweza kutolewa kwa moyo wa ubinadamu, ambao unahitaji maisha hata kama hatambui. Papa Francisko ametoa mfano mwanaume na mwanamke wanaoana na hasa wanapokuwa na nia ya kufanya jambo kubwa na zuri na ikiwa wanahifadhi uhai wa kiu hiyo kwamba watapata daima njia kwa ajili ya kwenda mbele hata katikati ya matatizo mengi  na kwa msaada wa neema. Hata vijana wanayo njaa na ahawapwi kuipoteza. Lazima kuilinza na kumwilisha katika moyo wa watto ile shuku ya upendo, ya upendo, ya ukarimu  ya kukaribisha na ambayo inatafsiriwa katika msukumo wao wa ari  za kweli na angavu.

Kila mtu anaitwa kugunduwa kwa upya kile cha muhimu kweli, kile ambacho kweli anahitaji, kile ambacho kinafanya kuishi kwa wema na wakati huo huo kile ambacho ni cha pili na kile ambacho kweli kinaweza kufanyika kwa utulivu. Yesu anatangaza heri hii ya njaa na kiu ya haki kwa maaa kuna kiu kisichoweza kukatishwa tamaa; kiu ambaco kikifuatwa, kitaridhishwa na kitafanikiwa kila wakati, kwa sababu kinalingana na moyo wa Mungu, cha Roho wake Mtakatifu ambaye ni upendo na hata mbegu ambayo Roho Mtakatifu alipnda katika mioyo yetu. Bwana aweze kutujalia neema hii, ya kuwa na kiu ya haki ambayo kweli ni utashi wa kutafuta  na  kuona Mungu na kutenda mema kwa wengine.

KATEKESI YA PAPA
11 March 2020, 13:23