Katekesi ya Papa 25 Machi 2020.Kiini cha Katekesi ni Injili ya Uhai kwa mujibu wa Waraka wa Mtakatifu Yohane Paulo II alioutangaza miaka ishirini na tano iliyopita Katekesi ya Papa 25 Machi 2020.Kiini cha Katekesi ni Injili ya Uhai kwa mujibu wa Waraka wa Mtakatifu Yohane Paulo II alioutangaza miaka ishirini na tano iliyopita 

Papa Francisko:Katika Katekesi kiini ni Waraka wa Injili ya Uhai!

Wakati wa tafakari ya katekesi ya Papa Francisko tarehe 25 Machi 2020,ikiwa Mama Kanisa anadhimisha Siku Kuu ya Kupashwa Habari Maria.Kitovu cha tafakari kimekuwa ni Waraka wa Evangelium Vitae-Injili ya Uhai.Mwisho wa Katekesi Papa amerudia kutoa wito kwa wakristo wote duniani kusali na kumwomba Mungu ili asitishe mlipuko vya virusi.Amekumbusha hata Ijumaa 27 Machi 2020 kushiriki Sala naye katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Miaka ishirini na tano iliyopita katika tarehe hii ya 25 Machi, ambapo katika Kanisa ni Siku kuu ya Kupashwa Habari ya Bwana, Mtakatifu Yohane Paulo II alichapisha Waraka wake wa kitume wa Evangelium vitae, (Injili ya Uhai) kuhusu thamani ya maisha ya mwanadamu. Leo hii tunajikuta kwa mara nyingine tena kutangaza mafundisho hayo katika muktadha wa mlipuko ambao unahatarisha maisha ya mwanadamu na uchumi duniani. Ni hali halisi inayosikika tena, ambayo inahitaji jitihada zaidi katika maneno ambayo yanaanza na Waraka huu. Maneno hayo ni: “Injili ya maisha iko moyoni mwa Yesu. Kwa kupokelewa na Kanisa kila siku kwa upendo inakwenda kutangaza kwa ujasiri wa imani kama habari njema kwa watu wa kila wakati na utamaduni”(n.1).

Ndiyo mwanzo wa maneno ya Papa Francisko wakati wa Katekesi yake tarehe 25 Machi 2020 akiwa katika maktaba ya Jumba la Kitume mjini Vatican, iliyotangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari Vatican, katika muktadha wa mlipuko wa janga la Virusi vya Corona Covid-19. Papa Francisko akiendelea amesema kuwa, kama ilivyo kila tangazo la kiinjili, hata hilo lazima awali ya yote kulishuhudia.  Anafikiria kwa shukrani kubwa ushuhuda wa ukimya wa watu wengi ambao kwa namna nyingi hali zozote wako  wanajitahidi kutoa huduma kwa wagonjwa, kwa wazee na wale ambao wako pekee yao na wenye kuhitaji. Hawa wako wanajikita katika matendo ya dhati ya Injili ya maisha, kama  Maria ambaye alipokea habari kutoka kwa Malaika na alikwenda mara moja kumsaidia binadamu yake Elizabeth ambaye pia alikuwa anahitaji msaada. Papa Francisko amebainisha.

Kiukweli maisha ambayo tunaalikwa kuhamasisha na kulinda siyo suala lisilofikirika bali linajionesha daima katika mtu mwenye mwili na mfupa. Mtoto ambaye punde ametungwa mimba, katika maskini aliyebaguliwa, kwa mgonjwa ambaye yuko peke yake na kukata tamaa au yuko katika hali ya mwisho, kwa yule ambaye amepoteza kazi au hawezi kupata ajira, mhamiaji ambaye amekataliwa au kuwekwa pembeni… Maisha yanajionesha katika hali halisi kwa mtu! Papa Francisko amesisitiza. Kila mwanadamu ameitwa na Mungu ili afurahie utimilifu maisha; na kwa kuwa amekabidhiwa katika ulinzi wa umama wa Kanisa, kila hatari ya hadhi na maisha ya mwanadamu hayawezi yasiguse katika moyo huo, katika umbu la kimama. Ulinzi wa maisha kwa ajili ya Kanisa siyo itikadi za mawazo ni hali halisi , hali halisi ya mwanadamu ambayo inawazunguka wakristo wote  na zaidi kwa sababu ni wakristo na hata kwa sababu ni wanadamu. Siyo itikadi za mawazo! Papa Francisko amesisitiza.

Mashambulio juu ya hadhi na maisha ya watu kwa bahati mbaya yanaendelea hata katika zama zetu, ambazo ni zama za haki za binadamu katika ulimwengu wote; kwa upande huo, tunakabiliwa na vitisho vipya na utumwa mpya, na sheria siyo wakati wote wanalinda  maisha ya walio zaidi dhaifu na wanadamu waathirika. Ujumbe wa Waraka wa Evangelium vitae ( Injili ya uhai)kwa maana hiyo inafaa zaidi wakati huu kuliko hapo awali. Zaidi ya dharura, kama ile tunayoishi, ni swala la kutenda kwa kiwango cha kiutamaduni na kielimu ili kuweza kuonesha kwa vizazi vijavyo ule mtazamo wa mshikamano, utunzaji, ukarimu, kwa kutambua  kabisa kuwa utamaduni wa maisha siyo urithi wa kipekee wa wakristo, bali  ni kwa ajili ya  wale wote wanaojitahidi katika ujenzi wa uhusiano wa kidugu, kugundua thamani ya kila mtu, hata wakati yeye ni dhaifu na mateso.

Kila maisha ya mwanadamu, ni ya kipekee na yasiyoweza kuelezewa, yako halali yenyewe, yana thamani kubwa isiyo isha. Hii lazima itangazwe kila wakati tena, kwa ujasiri wa neno na ujasiri wa vitendo. Hii inahitaji mshikamano na upendo wa dhati kwa familia kubwa ya wanadamu na kwa kila mmoja wa washiriki wake. Kwa njia hiyo Mtakatifu Yohnae Paulo II aliyetangaza Waraka huo pamoja naye, mimi pia ninathibitisha kwa kusadikishwa tena wito ambao aliwaelekeza  watu wote miaka ishirini na mitano iliyopita: "Heshimu, tetea, penda na hudumia maisha, kila maisha, kila maisha ya mwanadamu! Ni kwa njia hii tu utapata haki, maendeleo, uhuru, amani na furaha” (Enc. Evangelium vitae, 5). Asante. Amehitimisha Papa Francisko katekesi yake  tarehe 25 Machi 2020.

KATEKESI-PAPA
25 March 2020, 11:22