Misa ya Papa Francisko Dominika tarehe 22 Machi 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa ya Papa Francisko Dominika tarehe 22 Machi 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta 

Virusi vya Corona,COVID-19:Papa Francisko awaombea marehemu!

Katika misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican,tarehe 22 asubuhi,mwendelezo wa nia zake kwa siku hii amekumbuka wale wote wanaokufa peke yao bila kuagwa na ndugu zao kutokana na janga la Covid-19.Katika mahubiri anawaalika waamini watambue Yesu ambaye anapita katika maisha binafsi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameadhimisha misa Takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican asubuhi tarehe 22 Machi 2020 ikiwa ni katika Misa ya Dominika ya IV ya kwaresima. Misa kama hii imeanza kuadhimishwa ikitangazwa moja kwa moja kupitia  vyombo vya mawasiliano Vatican tangu tarehe 9 Machi 2020 kwa mujibu wa  maamuzi ya Papa Francisko ambaye anataka kuonesha ukaribu wake sana wa kiroho  kwa waamini wote ambao hawawezi kushiriki misa kutokana na janga la virusi vya corona (COVID-19). Wakati wa utangulizi wake Papa Francisko amerudia kuwaombea waathirika wa ugonjwa huu.  “Katika siku hizi tunasikia habari za vifo vingi, wanaume na wanawake wanakufa peke yao bila kusindikizwa na wapendwa wao. Tufikirie wao na kusali kwa ajili yao. Lakini pia hata kwa ajili ya familia ambao hawawezi kuwasindikiza wapendwa wao katika hatua yao  ya mwisho. Sala zetu maalum ni kwa ajili ya marehemu na familia zao”.

Papa Francisko katika tafakari yake kwa kuongozwa na Injili ya siku kutoka  (Yh 9,1-14) kuhusu uponywaji wa mtu kipofu tangu kuzaliwa, ameshauri kukesha ili kuweza  kumtambua Yesu anayepita karibu katika maisha yetu na ili kuweza kumwongokea Yeye. Sehemu ya Injili ya Yohane (9,1-41) inazungumzia yeye binafsi, Papa anasema, “Ni tangazo la Yesu Kristo na hata katekesi. Ninapendelea nitaje jambo moja. Mtakatifu Agostino ambaye daima ananishangaza anasema “nina hofu ya Kristo anapopita.” “Timeo Dominum transeuntem”. “Nina hofu atakapopita Kristo”. “Lakini kwa nini una hofu ya Bwana?  Nina hofu kutokana na kwamba hasije pita Kristo bila kumtambua na kumwacha apite”. Jambo moja ni wazi anaongeza Papa kwamba, “katika uwepo wa Yesu hisia za kweli ndani ya moyo zinaweza kuchanua, na   tabia za kweli ziweza kufumka nje.

Ni neema na ndiyo maana Agostino alikuwa na hofu ya kuweza kumwacha Yesu apite bila hata kutambua kuwa anapita”.  Aidha Papa amesema “hii  ni wazi kwani anapita na kumponya kipofu na wakati huo  kuamsha manung’uniko. Baadaye anakuwa mtu bora zaidi na mbaya zaidi ya watu. Yeye alikuwa amezoea kuzungusha mikono yake, alikuwa na hisia ya hatari, alikuwa na hisia za vitu vya hatari ambavyo vingeweza kumfanya ateleze. Na alikuwa akitembea kama kipofu. Katika hoja ya wazi na sahihi, pia ametumia kejeli, kwa kupewa sifa hii.

Walimu wa Sheria walikuwa wanajua sheria zote, lakini walikuwa wameshikilia pale tu. Hawakuwa na utambuzi ni lini Mungu atapita. Walikuwa wakali, wameshikilia tabia na kasumba zao tu. Yesu mwenyewe anawaleza katika Injili kwamba wameshikilia kasumba zao. Na  katika kuhifadhi kasumba zao walikuwa wanatenda pasipo haki,  lakini kwao haikuwa ni tatizo, kwa maana kasumba yao ilikuwa siyo  makosa kwao; ule ugumu wao uliwapelekea watende pasipo haki. Mbele ya Kristo walikuwa na moyo uliofungwa.

Papa Francisko ametoa ushauri wa kuchukua Injili ya Yohane  katika  sura ya tisa na kusoma  kwa utulivu nyumbani. Inawezekana kusoma mara moja, mara mbili ili kuelewa vizuri  ni kitu gani kinatokea ikiwa Yesu anapita. Papa Francisko amehitimisha misa kwa kuabudu Ekaristi na kutoa baraka ya Ekaristi huku akiwaalika waamini waipokee kiroho.

23 March 2020, 10:00