Afya ya Baba Mtakatifu Francisko inaendelea kuimarika zaidi. Anaadhimisha Ibada ya Misa takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican na kufuatilia Mafungo ya Kwaresima. Afya ya Baba Mtakatifu Francisko inaendelea kuimarika zaidi. Anaadhimisha Ibada ya Misa takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican na kufuatilia Mafungo ya Kwaresima. 

Afya ya Baba Mtakatifu Francisko inaendelea kuimarika zaidi!

Afya ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye hivi karibuni alikumbwa na mafua makali inaendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba, anaendelea pia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican. Baba Mtakatifu pia anaendelea kufuatilia tafakari za mafungo ya Kwaresima zinazotolewa kwa wafanyakazi wa “Curia Romana” huko Ariccia!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Dr. Matteo Bruni Msemaji mkuu wa Vatican katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, afya ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye hivi karibuni alikumbwa na mafua makali inaendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba, anaendelea pia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican. Baba Mtakatifu pia anaendelea kufuatilia tafakari za mafungo ya Kwaresima zinazotolewa kwa wafanyakazi wa “Curia Romana” huko Ariccia, nje kidogo ya mji wa Roma. Dr. Matteo Bruni amefafanua kwamba, Baba Mtakatifu anasumbuliwa na mafua ambayo hayana uhusiano wowote na magonjwa mengine!

Tafakari wakati wa mafungo maisha ya kiroho Kipindi cha Kwaresima kwa Mwaka 2020 kwa wasaidizi wa karibu wa Baba Mtakatifu, “Curia Romana” kuanzia tarehe 1 Machi hadi 6 Machi, 2020 huko Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma, inaongozwa na Padre Pietro Enrico Bovati, SJ, Katibu mkuu wa Tume ya Kipapa ya Biblia na Mtaalam wa Sayansi ya Maandiko Mtakatifu. Kauli mbiu ya mafungo haya ni “Kile kijiti kiliwaka moto: mkutano kati ya Mwenyezi Mungu na binadamu mintarafu mwanga wa Kitabu cha Kutoka, Injili ya Mathayo na Sala ya Zaburi”.

04 March 2020, 14:15