Wosia wa Kitume wa Papa Francisko baada ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia unaoongozwa na kauli mbiu “Querida Amazonia” yaani mpendwa Amazonia” Wosia wa Kitume wa Papa Francisko baada ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia unaoongozwa na kauli mbiu “Querida Amazonia” yaani mpendwa Amazonia”  

Querida Amazonia ni Wosia wa Kitume wa Papa ukiangazia Kanisa la Amazonia

Umetangazwa wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia unaoongozwa na kauli mbiu “Querida Amazonia” yaani mpendwa Amazonia” ambao umeandikwa kwa lugha ya kihispania.Hati hii inajikita katika michakato ya uinjilishaji mpya na utunzaji wa mazingira na maskini.Ni matumaini na mwamko mpya wa kimisionari na kutia moyo nafasi ya walei katika jumuiya za Kanisa.

Na Alessandro Gisotti – Vatican

Mpendwa Amazonia, unajionesha mbele ya dunia  kwa uzuri wake wote, janga lake na fumbo lake. Ndivyo unavyoanza Wosia wa Kitume baada ya Sinodi uitwao “Querida Amazonia”. Papa Francisko katika sura ya (2 -4) anaelezea maana ya Wosia huo wenye utajiri kutokana na hati nyingine za Mabaraza ya Maaskofu wa Kanda za Nchi za Amazonia, lakini hata kutumia mashairi ya waandishi wanaogusa Amazonia. Papa Francisko anabainisha kwa jinsi gani  anavyotaka kutoa ufafanuzi wake kwa kile ambacho Sinodi ilithibitisha na kukabidhiwa yeye. Papa anabainisha kwamba hataki kuondoa au kurudia Hati ya mwisho na ambayo anawaalika kuisoma yote nzima na ni matarajio ya Kanisa lote kuacha watajirishwe na kuchangamotishwa nayo  na kutokana nayo Kanisa lote la Amazonia lijitahidi   kuweka katika matendo.

Papa Francisko anashirikisha ndoto zake kwa ajili ya Amazonia (5-7) na ili hatima yake iweze kuangaikia wote, na ardhi hiyo ambayo iwe pia kanuni ya ndoto hizo nne ambazo ni:  Amazonia ipambanie haki za walio maskini zaidi; iweze kulinda utajiri wa utamaduni; iweze kuhifadhi kwa shauku kubwa uzuri wa asili na mwisho jumuiya za kikristo ziwe na uwezo wa kujikita katika jitihada za kina kwa ajili ya Amazonia.

Ndoto kijamii: Kanisa liwe karibu na wanaokandamizwa

Katika sura ya kwanza ya Querida Amazonia, inajikita  kuhusu ndoto ya kijamii (8) Papa anasisitiza kuwa mbinu za kiekolojia pia ndizo mbinu za kijamii  lakini pamoja na kuwpongeza kwa namna ya kuishi vizuri watu wa asilia, anatoa onyo dhidi ya kasumba za kuhifadhi ambazo zinaangaikia mazingia tu. Na kwa namna hiyo anazungumza kuhusu ukosefu wa haki na uhalifu  (9-14). Papa  anafafanua zaidi kwamba tayari hata Papa Benedikto XVI alikuwa amekwisha tangaza  juu ya utumiaji  hovyo wa mazingira ya Amazonia. Maskini asilia anaonya wanateseka na kuwa  kama watumishi, iwe kwa upande wa wenye madaraka mahalia, na hata wale wanaotoka nje. Kwa mujibu wa Papa opereshi za kiuchumi ambazo zinaongoza uraruaji, mauaji, ufisadi, zinastahili kupewa jina la ukosefu wa haki na uhalifu. Pamoja na Mtakatifu Yohane Paulo II ,wanasema kuwa utandawazi haupaswi kugeuka kuwa ukoloni mpya.

Maskini wasikilizwe kuhusu wakati endelevu wa Amazonia

Mbele ya ukosefu mwingi wa haki, Papa Francisko anaomba kuacha hasira na badala yake kuomba msamaha (15-19). Kwa  mujibu wa Papa Francisko, inahitaji mitindo ya mshikamano na maendeleo na kuwaalika wote wakiwemo viongozi wa kisiasa. Kufuatana na hiyo Papa anasisitiza juu ya mada ya maana ya Kijumuiya (20-22). Analalamikia watu wa Amazonia kuhusu uhusiano kibinadamu ambao unatokana na mzunguko wao wa  asili. Kwa maana hiyo anaandika kwamba wanaishi kama  vile ni kuondolewa katika mizizi  yao hasa wakati wanapolazimishwa kuhamia kwenye miji. Na Sehemu ya mwisho wa sura ya kwanza imejikita kutazama Taasisi zilizoharibika (23-25) na  Majadiliano ya kijamii (26-27. Hata hivyo Papa Francisko anatamka juu ya ubaya wa rushwa ambao unatoa sumu katika Taifa na taasisi zake.  Ni matashi yake kwamba Amazonia inaweza kugeuka kuwa sehemu ya majadiliano kijamii awali ya yote na walio wa mwisho. Na kwa Maskini anawapa ushauri  wawe  sauti ya nguvu kuhusu Amazonia.

Ndoto ya Utamaduni: kuwa na ulinzi wa mzunguko wa Amazonia

Katika sura ya Pili imejikita kutazama juu ya ndoto ya Utamaduni. Papa Francisko anaweka wazi kuwa ili kuhamasisha Amazonia, haina maana ya kuwekwa ukoloni wa utamaduni (28). Kwa kufafanua hilo ametumia picha ya umbo lenye pande nyingi mviringo  ambayo anapendelea kuitumia mara nyingi kama Amazonia (29-32). Ni lazima kupambana dhidi  ya ukoloni mamboleo. Kwa mujibu wa Papa ni dharura ya kulinda mizizi(33-35). Kwa kutaja  Wosia wa Laudato Si na Christus vivit    anabainisha kuwa maono ya utumiaji hovyo wa kibinadamu, unataka kupelekea ufafanisho  wa utamaduni  na matokeo hayo zaidi yanawakumba vijana. Kwa upande wa vijana Papa anawaomba wajitwike ile mizizi na kuirudisha ile  kumbu kumbu iliyo jeruhiwa.

Hapana uasilia uliofungwa:inahitaji kukutana kiutamaduni

Katika wosia pia inasisitiza juu ya makutano ya kiutamaduni (36-38). Papa anasema kuwa hata tamaduni  ambazo utafikiri zimeendelea zaidi, zinaweza pia kujifunza kutoka kwa watu ambao wamedumisha na kuendeleza thamani ya utamaduni fungamani asilia. Utofauti kwa maana hiyo usiwe kizingiti bali kuwa daraja  na anakataa katu ile  hali ya uasilia wa kujifungia kabisa. Sehemu ya mwisho ya sura hiyo imejikita katika mada ya tamaduni zinazotishiwa na watu walio hatarini (39-40). Kila aina ya mpango kwa ajili ya Amazonia anashuri kwamba  lazima uchukue  wajibu wa maono na matarajio ya haki za watu. Kwa kutofanya hivyo watu asilia wanaweza kuhisi hawastahili ikiwa mazingira ambayo walizaliwa na kukua yanaharibiwa.

Ndoto ya kiekolojia: kuunganisha ulinzi wa mazingira na utunzaji wa watu

 Sura ya tatu  inayohusu ndoto ya kiekolojia ni ile ambayo inaungana moja kwa moja na Wosia wa Laudatosi. Katika utangulizi wake ( 41-42) inasisitiza kuwa Amazonia ipo na uhusiano wake unaoungana moja kwa moja na ubinadamu  na asilia. Kuwatunza ndugu kama Bwana anavyo tutunza sisi, ndiyo ekolojia ya kwanza ambayo tunahitaji. Kutunza mazingira na kutunza maskini ni vitu viwili visivyo tengenishwa. Aidha Papa Francisko anaongeza kuelezea umakini wa ndoto ile ya maji ( 43-46). Anataja Pablo Neruda  na washairi wengine mahalia kuhusu nguvu na uzuri wa Rio na Amazonia.  Kwa njia ya Mashairi yao anaadika: “yanatusaidia kujikomboa dhidi ya dhana za kiteknolojia  na utumiaji hovyo ambao unasonga asili.

Kusikiliza kilio cha Amazonia, maendeleo yawe endelevu

Kwa mujibu wa Papa Francisko  anasema kuna dharura ya kusikiliza kilio cha Amazonia ( 47-52). Anakumbusha kuwa usawa wa sayari hii unategemeana  na afya yake. Kuna hitaji la matakwa binafsi na siyo tu mahalia bali hata kimataifa. Suluhisho kwa namna hiyo siyo kimataifa kuhusu Amazonia, bali lazima kukua kwa uwajibikaji na majukumu ya  serikali za mataifa. Maendeleo endelevu yanataka kwamba watu daima wajulishwe kuhusu mipango inayotazama nchi na ni matarajio ya Papa kuwa inawezekana kuwapo uundaji wa mfumo wa kawaida ambao uwekwe hata vidhibiti vya ukiukwaji. Anawaalika kwa namna hiyo katika unabii wa kutafakari (53-57). Kwa kusikiliza watu asilia, anasisitiza tunaweza kupenda Amazonia na siyo tu kuwatumia, tunaweza kupata kutoka kwao nafasi ya kitaalimungu, nafasi ambamo Mungu anajionesha na kuita watoto wake. Sehemu ya mwisho ya sura ya tatu, inajikita kuhusu Elimu na tabia za ekolojia (58-60) ambapo Papa Francisko anabainisha kwamba Ekolojia siyo suala la kiufundi, bali ni uelewa daima wa dhana ya elimu.

Ndoto ya kikanisa: kukuza Kanisa moja lenye sura ya Amazonia

Sura ya mwisho ni nzito zaidi ambayo imejikita moja kwa moja kwa upande a suala la  wachungaji na waamini katoliki na kwa maana hiyo inajikita katika ndoto ya Kikanisa. Papa Francisko anawaalika wakuze Kanisa moja lenye uso wa Amazonia kwa njia ya tangazo kuu la Kimisionari (61), na ambalo ni tangazo muhimu katika Amazonia (62-65). Kwa upande wa Papa anasema haitoshi kupeleka ujumbe wa kijamii.  Watu hawa wanayo haki ya kutangaziwa Injili la sivyo kila muundo wa kikanisa utakuwa kama shirika lisilo la kiserikali (ONGs). Kwa upande mwingine anaelekeza juu ya utamadunisho. Hapa Papa anajikita katika Barua ya  Gaudium et Spes, na kuzungumzia juu ya utamadunisho(66-69) kama mchakato ambao unapelekea ukamilifu wa mwanga wa Injili na kile kilichomo ndani ya utamaduni wa Amazonia.

Upyaishaji wa utamadunisho wa Injili huko Amazonia

Papa Francisko ana mtazamo wake wa kina kwa kuekeleza njia za utamadunisho huko Amazonia ( 70-74). Thamani  zilizomo katika jumuiya asili, anaandika zinapaswa kuzingatiwa katika uinjilishaji. Katika sehemu mbili zinazofuatana, anajikita  kuelezea juu ya utamadunisho kijamii na kiroho(75-76). Papa anabainisha wazi  kwamba kutokana na hali ya umasikini wa wakazi wengi wa Amazonia, utamadunisho lazima uwe na mhuri wenye nguvu kijamii. Kwa wakati huo lakini,  ukuu wake kijamii ni lazima ufungamanishwe na ule wa kiroho.

Sakramenti zitolewe kwa wote hasa maskini

Wosia wa Papa Francisko unaelekeza  pia  eneo la kuanzia kwa utakatifu wa Amazonia (77-80) na kwamba hautakiwi kuiga mitindo  ya maeneo mengine.  Papa anafafanua kuwa inawezekana kutambua  kwa namna moja ishala  Fulani ya asili bila ulazima wa kutafuta ubora wa kinyago. Inawezekana kuthamanisha jambo la asili lenye kina  na  maana ya kiroho bila ulazima wa kufikiria kama ni la kipagani.  Hii ni sawa sawa hata kwa baadhi ya sikukuu za kidini ambazo zinahitaji mchakato wa utakaso na ambazo zina maana yake ya utakatifu.

Sehemu nyingine yenye maana katika ‘Querida Amazonia’, ni kuhusu utamadunisho wa liturujia  (81-84). Papa anaeleza kuwa tayari katika Mtaguso wa Vatican II ulikuwa umeomba kuwepo juhudi za utamadunisho wa liturujia ya watu asilia. Anakumbusha pia katika maandiko ambayo Sinodi imejikita ndani ya mapendekezo ya kufanyiwa kazi kuhusu ibada ya amazonia. Sakrameti kwa maana hiyo anashauri zinapaswa zitolewe kwa wote hasa masikini. Kwa kutumia Wosia wa Amoris Laetitia Papa anasisitiza kuwa Kanisa haliwezi kujigeuza kuwa “mpaka”.

Maaskofu wa Amerika Kusini watume wamisionari huko Amazonia

Kulingana na suala la sakramenti pia kuna  mada ya utamadunisho wa huduma (85-90) ambapo Kanisa linapaswa kutoa jibu la kijasiri. Kwa upande wa Papa anasema lazima kuhakikisha kwa kiasi kikubwa juu ya maadhimisho ya mara kwa mara ya Ekaristi. Kwa mtazamo  huo anasema ni muhimu kuwa na uamuzi ambao ni maalum kwa makuhani. Jibu liko katika Sakramenti ya Wakfu ambayo ina uwezo tu kwa makuhani ambao wanaadhimisha Ekaristi. Je ni kwa jinsi gani ya kuhakikisha huduma ya kikuhani katika maeneo hayo? Papa Francisko anashauri Maaskofu wote hasa wa Amerika ya Kisini kuwa wakarimu ili kuwaelekeza wale ambao wanajionesha kuwa na wito wa kimisioanri wa kuchagua Amazonia na anawaalika kutazama kwa upya kuhusu mafundisho ya kikuhani.

Kukuza mwamko wa walei ili wawe mstari wa mbele katika jumuiya

Katika  suala la Sakramenti kwenye ‘Querida Amazonia’, Papa anajikita  kufafanua kuhusu Jumuiya yenye uhai wa maisha(91-92) ambapo walei lazima wachukue majukumu muhimu. Kwa mujibu wa Papa siyo tu kukuza kwa kiasi kukubwa uwepo wa makuhani waliotiwa wakfu lakini pia lengo ni kuhakikisha unakuwapo uhai wa maisha katika jumuiya nzima. Inahitaji kwa maana hiyo huduma mpya ya kilei.  Ni kwa njia ya kukuza uhai wa maisha ya walei kuwa mstari wa mbele ambapo Kanisa Kanisa linaweza kujibu changamoto  za Amazonia. Kwa upande  wa Papa, nafasi maalum wanayo pia watawa  na wakati huo  huo anakumbusha nafasi ya Jumuiya ndogo ndogo ambazo zimeweza kulinda haki kijamii na anawatia moyo kwa namna ya pekee katika shughuli ya REPAM, na makundi ya kimisionari yanayotoa huduma yake kwa kuzunguka.

Nafasi mpya kwa wanawake lakini bila kuwa mashemasi

Nafasi ambayo Papa amejikita nayo kufafanua ni kwa upande wa nguvu na zawadi ya wanawake ( 93-103). Anatambua kuwa baadhi ya Jumuiya za Amazonia zimeweza kuwapo shukrani kwa uwepo wa wanawake wenye nguvu na wakarimu. Anaweka taadhari kwamba suala hili lisije fikiriwa  katika Kanisa kama mfumo wa kikazi.  Kama ingekuwa hivyo, ingejulikana kama nafasi ya kuwekwa wakfu. Kwa maana hiyo  Papa anakataa ushemasi wa wanawake, lakini kinyume chake na anapokea  na kukubali mchango wao  unatolewa na wanawake,  ambao umedumu kwa nguvu na huduma ya Maria. Anawatia moyo ili kuzaliwe huduma mpya za kilei ambazo zinaweza kutambuliwa katika umma na maaskofu kwa  maamuzi kwa ajili ya jumuiya.

Wakristo wapambane kwa pamoja ili kulinda maskini na Amazonia

Kwa mujibu wa Papa lazima kuongeza maono zaidi ya mipaka (104-105 na kuacha kuchangamotishwa na Amazonia ili kushinda dhana za vikwazo ambavyo vinabaki vimefunga mantiki fulani. Sura ya IV inahitimisha kwa mada  ya kuishi pamoja kiekumene na kidini(106-110). Papa anawaalika waamini kutafuta nafasi za kujadiliana na kutenda kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa pamoja. Je ni kwa jinsi gani ya kukosa kupambana pamoja? Anauliza Papa Francisko, Je ni kwa namna gani ya kutosali pamoja na kufanya kazi bega kwa bega ili kulinda maskini  wa Amazonia?

Tuikabidhi Amazonia na watu wake kwa  Maria

Papa Francisko anahitimisha ‘Querida Amazonia’ na sala kwa Mama Maria wa Amazonia (111). Mama, tazama maskini wa Amazonia… na kusali sehemu ya maombi, kwa sababu nyumba yao inaharibiwa kwa sababu ya matakwa yao ya ubahili (…) gusa hisia za wenye nguvu hata kama tunahisi tumechelewa, wewe unatuita kuokoa kile ambacho bado kinaishi.

12 February 2020, 12:00