Tafuta

Vatican News
Papa alikutana na Watu wa Amazonia wa Coliseo Madre de Dios Papa alikutana na Watu wa Amazonia wa Coliseo Madre de Dios  (Vatican Media)

Mabalozi katika Kanisa la Kimisionari

Uamuzi wa Papa wa kuweka mwaka mzima wa uzoefu wa kimisionari katika curriculum ya mafunzo ya watu wa kidiplomasia kwa ajili ya Vatican.

ANDREA TORNIELLI

Uamuzi wa Papa wa kuingiza curriculum  ya mafunzo kwa watu wa Kidiplomasia kwa ajili ya  huduma ya ubalozi wa kitume kwa mwaka mzima katika ardhi ya kimisionari imewadia miezi michache baada ya kutangaza na Papa mwenyewe wakati wa hotuba yake ya mwisho kwenye Sinodi ya Amazonia.  Tamko ambalo sasa linakuwa hali halisi kwa wanafunzi wapya wa Taasisi ya Kipapa ya Mafunzo ya Kanisa kwa muhula wa mwaka 2020/2021. Ni vema kutambua awali ya yote kuwa mantiki ya mpango huu ilikuwa imekwisha julikana, kwa ulazima wa kupta  makuhani kwa ajili ya utume na matatizo ya kuwapata. Papa alikuwa alikuwa ameonesha jibu hali ambalo alisema mara nyingi asikia wakisema kuwa, “mimi siwezi hilo”. Sawa alikuwa  amesema Papa kwamba “ lakini hilo linapaswa lifundishwe..Vijana wa dini wanao wito mkubwa sana na wanahitaji kufunzwa kwa shauku ya kitume ili waweze kwenda katika miisho ya dunia”

Baadaye Papa alikuwa amezungumza hata kuhusu wanadiplomasia wa wakati ujao, akitaja mojawapo ya pendekezo alilopata sasa: katika curriculum ya huduma ya kidiplomasia ya Vatican  makuhani vijana waweze kupitia angalau mwaka mmoja katika ardhi za kimisionari na siyo kama kufanya mazoezi kwenye ofisi ya ubalozini, kama ilivyokuwa ikifanyika hadi sasa, na ambayo anasema  ni vema, lakini kwa urahisi katika huduma ya Askofu kwenye maeneo ya utume wa  kimisonari. Kwa sasa jambo hili linatimizwa na kwa kuhitimisha barua yake kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Kipapa, Papa anasisitiza kuwa “uzoefu wa kimisionari ambao unapaswa kuhamasishwa utarudia kuwa muhimu na siyo tu kwa vijana wanafunzi, lakini pia hata kwa makanisa mahalia ambao watashirikiana na ninawatakia kwamba izaliwe ile  shauku kwa makuhani wengine  katika Kanisa la ulimwengu ili kuwezesha kuwa na jukumu la kufanya kipindi cha huduma ya utume wa kimisionari nje ya jimbo lake binafsi”.

Hakuna shaka kwamba uamuzi sasa wa mtindo wa Mfuasi wa Petro unawakilisha mapinduzi ya kweli na yenye  maana katika mchakato wa mafunzo kwa wale ambao wanataweza kutoa huduma ubalozio wa kitume, na itakuwa ndiyo kama mtindo kwa ajili ya kufikia utume wa mahusiano na vijana katika ofisi za maaskofu. Ni jambo msingi katika curriculum ambayo sasa inakuwa mwaka mzima wa kujikita katika huduma ya utume wa kimisionari katika katika kambi nje ya bustani ya nyumba, ili kujichafua mikono ya kichungaji, katika makanisa yaliyoko kwenye miisho ya dunia.

Ni mwaka wa mapinduzi wa kazi ngumu, uzoefu mpya ambao utaruhusu ubora na uelewa wa kina wa hali halisi ya Kanisa, matatizo yake, shida zake, lakini pia hata matumaini yake  hata uzuri wa kutiwa moyo wake wa kila siku. Ni mwaka ambao utaruhusu wanafunzo ya wenye kitengo hicho na wakuu wao na maaskofu wao wa jimbo asili ili  kufanya mang’amuzi mema kwa kila miito. Mwaka ambao unaweza kusaidia kuendelea au kutoendelea na huduma hiyo. Kwa hakika hii itakuwa ni zuoefu ambao utaleta mapinduzi ya mtazamo na matarajio kwa wale ambao siku moja wataitwa kuwakilisha Papa katika sehemu mbalimbali za Nchi kwa kusisitizia namna hii umuhimu wa Kanisa mahalia ili kusaidia Papa kwa kutuma huduma yake kwa njia ya makuhani wema na wenye uwezo.

Ni kwa mara nyingine tena Papa Francisko anatukumbusha kuwa “Kanisa lote, huduma ya kidiploasia iliyo ngumu  au ya kimisonari au siyo.  Kanisa au ni la kutoka nje au siyo Kanisa, au ni la kutangaza au siyo Kanisa. Ikiwa Kanisa halitoki nje linaharibika na kupoteza maana yake ya Kanisa”. Linatakiwa jambo jingine alibainisha hili katika Kitabu cha mahojiano na Gianni Valente chenye jina “ Bila Yeye hatuwezi kufanya kitu”.

Kwa maana hiyo, “utume siyo mpango wa kampuni iliyoandaliwa vema. Na wala siyo tamasha lililoandaliwa kwa kuhesabu ni watu wangapi watashiriki kwa njia ya upropaganda wetu. Roho Mtakatifu anafanya kazi kama navyotaka, muda anaotaka na anapotaka kuelekeza. Matunda ya utume  hauhusiani na nia yetu, njia zetu, msukumo wetu na mipango yetu, bali  hukaa katika ukweli huu: hisia za mshituko katika mwili zinasikika kabla ya maneno ya Yesu, wakati anasema: “bila mimi huwezi kufanya kitu’. Alikuwa amesema Papa katika kitabu hicho cha mahojiano.

17 February 2020, 16:27