tarehe 4 Februari Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa afla ya kuadhimisha mwaka mmoja baada ya kitiwa sahihi ya Udugu wa kibinadamu kunako februari 2019 tarehe 4 Februari Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa afla ya kuadhimisha mwaka mmoja baada ya kitiwa sahihi ya Udugu wa kibinadamu kunako februari 2019 

Ujumbe wa Papa baada ya mwaka 1 tangu kutiwa sahihi ya udugu wa Kibinadamu!

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya video kwa washiriki wa afla huko Abu Dhabi katika fursa za kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutiwa sahihi ya Hati ya Udugu wa kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya kukukumbuka mwaka mmoja tangu kutiwa sahihi ya Mkataba wa Hati ya Udugu Kibinadamu huko Abu dhabi kati ya  mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyeb, na Papa Francisko kunako tarehe 4 Februari 2019, Papa  ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa afla hiyo akisema “leo tunaadhimisha mwaka wa kwanza tangu tukio la kibinadamu litokee, kwa tumaini la wakati endelevu ulio bora kwa ajili ya ubinadamu, uhuru endelevu, dhidi ya chuki, dhidi ya hasira, ubaguzi, misimamo mikali na ugaidi, vitu ambavyo vinatishia thamani ya amani, ya upendo na udugu.

Katika ujumbe huo aidha Papa anawatumia salam kwa namna ya pekee watu wote ambao wanasaidia shuguli za kibinadamu wote kwa ndugu maskini, wagonjwa, wanaoteswa na wadhahifu bila kujali dini, rangi, kabila na mahali  watokako. Ka maana hiyo anawapongeza kwa msaad uliotolewa na Shirikisho la Nchi za Uarabuni na Kamati Kuu kwa ajili ya kutekeleza wa Hati ya Udugu wa Kibinadamu na kushukuru hata shughuli iliyoanzisha na Nyumba ya Abrahamic iliyotangazwa na Waziri Mkuu kwa ajili ya udugu kibinadamu.

Papa Francisko katika Ujumbe wake kwa njia ya video anaonesha furaha kubwa ya kuweza kuona ushiriki wa kipinshi hicho cha kuwakilishi duniani tuzo ya Kimataifa  ya Udugu wa Kibinadamu ili liweze kuwatia moyo wote, hasa wale wenye mitindo ya kifadhila kwa  wanawake na wanaume katika dunia ambayo inayojikita ndani ya shuguli za kupenda kwa njia ya matendo  ya hisani na sadaka zilizotimizwa kwa ajili ya manuafa ya wengine. Na hii anathibitisha haijalishi  utofauti wa dini au kabila na utamaduni.

Hatimaye  Papa Francisko anaomba mwenyezi Mungu aweze kubariki kila jitihada  ili ziweze kustawisha wema wa kibinadamu na kwa msaada wa kuendeleza mbele ule udugu. Katika afla hiyo huko Abu Dhabi,  Papa amewakilishwa na Katibu wake maalum Monsinyo Yoannis Lahzi Gaid,na amesema kuwa Papa tuzo aliyokea kuhusu Udugu Kibinadamu aiwandee watu wa rohingya walioko Myanmar.

05 February 2020, 10:28