Tafuta

Vatican News
Ujumbe wa Papa Francisko wa Kwaresima 2020,unaoongozwa na kauli mbiu “twawaomba ninyi kwa jina la Kristo:mpatanishwe na Mungu”(2Kor 5,20) Ujumbe wa Papa Francisko wa Kwaresima 2020,unaoongozwa na kauli mbiu “twawaomba ninyi kwa jina la Kristo:mpatanishwe na Mungu”(2Kor 5,20)  

Ujumbe wa Papa wa Karesima 2020:Kwa jina la Kristo,mpatanishwe na Mungu!

Fumbo la Pasaka,msingi wa uongofu,dharura ya uongofu,upendo upeo wa mapenzi ya Mungu katika kujadiliana na watoto wake,utajiri wa kushirikishana,siyo kulimbikiza kwa jili ya binafsi,ni mambo yaliyomo katika Ujumbe wa Papa Francisko wa Kwaresima 2020,ukiongozwa na kauli mbiu:“twawaomba ninyi kwa jina la Kristo:mpatanishwe na Mungu”.Papa anathibitisha kuwa kuanzia tarehe 26-28 amehitisha Mkutano huko Assisi wa vijana wanauchumi,wajasiriamali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Umetolewa Jumatatu tarehe 24 Februari 2020 Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Kwaresima, unaongozwa na kauli mbiu kutoka katika Kitabu cha Pili cha Wakorinto: “twawaomba ninyi kwa jina la Kristo: mpatanishwe na Mungu” (2Kor 5,20) ambao ulitiwa sahini katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Laterano tarehe 7 Oktoba 2019, wakati wa siku ya kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Rosari. Papa anasema hata mwaka huu Bwana anatujalia kipindi muafaka kwa ajili ya kujiandaa kusheherekea kwa moyo uliyo pyaishwa na Fumbo la kifo na ufufuko wa Yesu, kichwa cha maisha ya kikristo binafsi na kijumuiya. Katika  Fumbo hili ndimo tunapaswa kuijiwa na kumbu kumbu akilini mwetu na moyoni. Kwa hakika kufanya hivyo hakuishi kukukuza ndani mwetu kile kipimo ambacho tunajihusisha na mwendelezo wa kiroho ili kupata jibu huru na ambalo ni karimu.

Fumbo la Pasaka, msingi wa uongofu

Furaha ya kikristo inatokana na usikivu na ukarimu wa Habari  Njema ya kifo na Ufufuko wa Yesu, yaani Kerygma. Hiyo inajikita katika Fumbo la upendo halisi wa kweli na wa dhati, ambao unaruhusu kuwa na uhusiano mtimilifu wa mazungumzo ya kweli na yenye kuwa na matunda (soma Christus vivit, 117). Mwenye kuamini anapata nguvu ya kusukumiza mbali ule ulaghai  ambao ni wa kujidanganya kuwa maisha yanatokana na asili yetu binafsi na kumbe maisha yenyewe yanatokana na upendo wa Mungu Baba, kwa njia ya mapenzi yake ya kujitoa maisha yake ili wote wawe nayo tele ( Yh 10,10).  Ikiwa unatoa umakini wa kusikiliza sauti ya ‘baba wa ulaghai’ ( Yh 8,45) ni dhahiri kuishia kuteleza pasipo na maana, kwa kufanya uzoefu wa jehanamu hapa duniani, kama inavyo shuhudiwa kwa bahati mbaya katika matukio mengi ya majanga ya uzoefu binafsi wa kibinadamu na kwa ujumla, Papa anandika.

Katika kwaresima ya mwaka 2020, Papa Francisko anapenda kwa namna hiyo kuweka mtazamo mpana wa kila mkristo  na kwamba, kama kile ambacho tayari amewaandikia vijana katika Wosia wa Kitume wa Chritus vivit: “tazameni mikono iliyowazi ya Yesu Kristo msulibiwa, jiachie kwa upya kuokolewa daima. Unapokaribia kuungamana dhambi zako, amini kwa uhakika katika huruma yake ambayo inakupa uhuru dhidi ya makosa. Tafakari kwa kina katika damu yake iliyomwagika kwa upendo mwingi na jiachie utakaswe nayo. Kwa namna hiyo unaweza kuzaliwa ndani mwake upendo mpya daima (Christus vivit,123).  Papa Francisko anabanisha kwamba, Pasaka ya Yesu siyo tukio la wakati uliopita, kwa maana nguvu ya Roho Mtakatifu  bado inaendelea daima na inaturuhusu kutazama na kugusa kwa imani ule mwili wa Kristo kwa njia ya  wanaoteseka wengi.

Dharura ya uongofu

Papa Francisko katika ujumbe wake anasema, ni  jambo jema kabisa kutafakari kwa kina Fumbo la Pasaka na shukrani ambayo tumepewa huruma ya Mungu. Uzoefu wa huruma unawezekana tu, kuwa  uso kwa uso na Bwana msulibiwa na mfufuka “ambaye alinipenda na kutoa maisha yake kwa ajili yangu” (Gal 2,20). Hayo ni majadiliano ya moyo kwa moyo na rafiki kwa rafiki. Ndiyo maana sala ni muhimu sana katika kipindi cha Kwaresima. Kabla ya kuwa wajibu, Papa anafafanua, sala inaelezea dharura ya kujibu ule upendo wa Mungu ambaye daima anatutangulia na kutusaidia. Mkristo kwa hakika anasali akiwa na utambuzi  kuwa amependwa bila kustahili. Sala inaweza kuwa yenye mtindo tofauti, lakini kinachohesabika mbele ya macho ya Mungu ni kwamba, sala zinachimba ule  undani wa moyo na kuondoa ule ugumu wa mioyo yetu, ili kuwa na uongofu daima wa kweli  na kwa mapenzi yake. Katika kipindi hiki muafaka,  Papa anasema "tuache  kwa namna hiyo, Yeye atuongoze kama Wana wa Israeli katika jangwa (Os 2,16) na ili  hatimaye katika kusikiliza sauti ya Mchumba wetu na kumwacha ili akae ndani mwetu kwa kina na sisi tuwajibike".  Aidha anafafanua: " Kwa kadiri tutakavyo acha tujumuishwe na Neno lake, ndivyo tutakavyoweza kufanya uzoefu wa huruma yake ya bure. Tusiache kwa namna hiyo kupita kipindi cha neema bure, kwa majidai yasiyo na maana kama vile sisi ndiyo mabwana wa nyakati na mitindo ya uongofu wetu kwake".

Upendo upeo wa mapenzi ya Mungu katika kujadiliana na watoto wake

Tendo la Bwana la kutupatia kwa mara nyingine kipindi muafaka kama hiki, Papa anasema katika uongofu wetu, hatupaswi kuuchukulia kama vile wa mbali.Badala yake, fursa hii mpya inapaswa ilete kwetu maana ya utambuzi na kutuzindua kutoka lepe la usingizi. Licha ya uwepo wakati mwingine wa majanga, mabaya ya maisha yetu, kama yale ya Kanisa na ulinwenguni, nafasi hii katika mabadiliko ya mapambano inajielezea ukarimu wa mapenzi ya Mungu, ili kutokatisha mazungumzo ya wokovu na sisi. Kwake  Yesu Msulibiwa, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa mdhambi kwa ajili yetu, (2Kor 5,21), mapenzi yake yalifikia kiasi cha kuangukia kwa Mwanaye kwa ajili ya dhambi zetu hadi “kumweka Mungu awe dhidi ya Mungu” kama alivyosema Papa Mstaafu Benedikto XVI (soma  Wosia wa Deus caritas est, 12). Mungu kwa dhati uwapenda hata maadui zake (Rej Mt 5,43-48). Majadiliano ambayo Mungu anataka kuthibitisha kwa kila mtu, kwa Fumbo la Pasaka ya mwanaye, siyo ule uliotolewa kwa wakazi wa Athene na wageni, ambao “walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya”(Mdo 17,21). Tabia ya maneno kama hayo, yenye kuamuru, kuwa na utupu kwa udadisi  na ujuu juu ni tabia ya ulimwengu wa kila wakati na katika siku zetu pia zinaweza kujiendeleza katika matumizi mabaya ya njia za mawasiliano, Papa Francisko amebainisha.

Utajiri wa kushirikishana na siyo kulimbikiza kwa ajili ya ubinafsi

Maisha kuyaweka kama kiini cha  Fumbo la Pasaka ina maana ya kuhisi huduma kwa ajili ya madondo ya Kristo Msulibiwa anayejionesha kwa  waathirika wengi wasio na hatia katika vita, waliobaguliwa katika maisha, tangu kuzaliwa hadi kufikia uzee; mitindo  mbalimbali ya vurugu na ghasia, majanga ya mazingira, ukosefu wa usawa katika ugawaji wa mali za nchi, biashara ya binadamu na mitindo yake yote, tamaa za kupata faida zisizo na kikomo na ambazo ni mtindo wa kufuata miungu, Papa anasisitiza. Aidha anasema  kwamba hata leo hii, ni muhimu kuwaalika wanaume na wanawake wenye mapenzi mema katika kushirikishana mali binafsi kwa watu wenye shida zaidi, kwa njia ya sadaka na hisani kama mtindo wa ushiriki binafsi na wa kujenga dunia iliyo na usawa zaidi. Ushirikishwaji katika upendo wa hisani, unamfanya mtu awe binadamu zaidi; na kulimbikiza ni hatari ya kujifungia na ubinafsi.

Wito wa Mkutano wa vijana wanauchumi tarehe 26-28 Machi 2020

Kufuatia na utajiti wa kushirikishana mali,  Papa ameendelea kuwabinisha kuwa “tunaweza na tunapaswa kusukumwa hata kwenda mbali zaidi kwa kufikiria ukuu wa miundo ya kiuchumi. Kwa maana hiyo katika Kwaresima ya mwaka 2020, kuanzia tarehe 26-28 Machi, Papa Franciso anambainisha kwamba, amehitisha Mkutano huko Assisi wa Vijana wanauchumi, wajasiriamali, na 'change makers', yaani watengenezaji wa mabadiliko, kwa lengo la  kuchangia kuweka msimamo wa uchumi ulio wa haki zaidi na uunganishi zaidi kuliko wa sasa. Kama ambavyo amekwisha rudia mara nyingi kwenye Hati za  Kanisa akibainibisha kwamba: “siasa ni mtindo fulani wa hisani” ( soma Hotuba ya  Pio XI FUCI, 18 Desemba 1927). Vivyo hivyo itakuwa kweli  katika kushughulikia na uchumi na roho hiyo ya kiinjili, ambayo ni roho ya Heri, Papa Francisko amefafanua. Kwa kuhitimisha anamwomba Maria Mtakatifu kwa ajili ya Kwaresima ijayo ili tupokee wito wa kuacha tupyaishwe na Mungu. Tuelekeze macho yetu katika moyo wa Fumbo la Pasaka na ili tuweze kuongoka katika mazungumzo ya wazi na ya dhati na Mungu. Katika mtindo huo, tunaweza kweli kugeuka kile ambacho Kristo aliwaambia wafuasi wake “kuwa chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu (soma Mt 5,13-14).

PAPA:UJUMBE WA KWARESIMA 2020
24 February 2020, 11:30