Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametoa tafakari yake katika Katekesi ya tarehe 12 Februari 2020 kwa mwendelezo wa heri ambapo amejikita katika heri ya pili" heri wenye huzuni maana watafarijika" Papa Francisko ametoa tafakari yake katika Katekesi ya tarehe 12 Februari 2020 kwa mwendelezo wa heri ambapo amejikita katika heri ya pili" heri wenye huzuni maana watafarijika"  (Vatican Media)

Papa Francisko:wenyeheri wanateseka na kulia kwa undani bila kuhuzunika!

Heri wenye huzuni,maana hao watafarijika.Wenye heri hawahuzuniki bali wanateseka na wanalia lakini kwa ndani.Ndiyo kiini cha roho ya kikristo kwa mujibu wa mababa wa jangwani.Uchungu wa ndani unafungulia uhusiano na upyaisho wa Bwana na jirani.Ni kutoka katika tafakari ya Papa Francisko tarehe 12 Februari 2012.Amehitimisha kuomba Bwana atujalie kupenda,upendo wa tabasamu,ukaribu,huduma hata kwa machozi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika mwendelezo wa tafakari  ya Katekesi ya kuhusu Heri za Mlimani  tarehe 12 Februari 2020 katika Ukumbi wa Papa Paulo VI kwa waamini na mahujaji ameanza kusema:Tumeanza safari  kuhusu Heri na leo hii tunajikita katika Heri ya pili. “Heri wenye huzuni, maana hao watafarijika”. Katika Lugha ya kigiriki ambamo iliandikwa Injili, Heri hii inaelezea neno ambalo halisimami. Kwa maana wenye heri hawahuzuniki bali wanateseka na wanalia lakini kwa undani.  Papa anatoa ufafanuzi wa heri za mlimani, kwamba hii ndiyo tabia ya ambayo imekuwa kiini cha roho ya kikristo ambapo mababa wa jangwani, yaani wamonaki wa kwanza wa historia walikuwa wanaita “penthos” yaani uchungu wa ndani ambao unafungalia uhusiano na Bwana na jirani; kwa maana ya upyaisho wa uhusiano na Bwana na jirani amesisitiza Papa!

Dhana mbili za kilio:uchungu wa kifo na dhambi

Papa Francisko anasema kilio hiki  katika Maandiko kinaweza kuwa na dhana mbili:Kwanza ni ile ya  kifo au kwa ajili mateso ya mtu.  Dhana ya pili ni ile ya machozi kwa ajili ya dhambi, yaani kwa ajili ya dhambi binafsi, hasa moyo unapobubujika hata  damu ya dhambi dhidi ya  kumkosea Mungu na jirani. Kwa njia  hiyo, hii ina maana ya kumtakia mema mwingine kwa namna ya kufanya uungane naye hadi kufikia kushirikishana uchungu wake. Hata hivyo Papa amebainisha kuwa, wapo hata  watu ambao ubaki mbali yaani kuwa kurudi hatua ya nyuma; na kumbe kinyume chake ni muhimu kwamba wengine waweze kuwa na nafasi ndani ya moyo wetu kwa dhati.

Kuna wanaoteseka watulizwe na wengine mioyo yao migumu kama jiwe

Vile vile Papa Francisko amkumbusha ni kwa jinsi gani mara nyingi amesisitiza juu ya zawadi ya kuwa na machozi na ambayo ni tunu! Je unaweza kupenda kwa namna ya ubaridi?  Je unaweza kupenda kwa udanganyifu? Kwa hakika hapana. Kuna wanaoteseka na ambao wanapaswa watulizwe, lakini pia mara nyingi kuna hata wale wenye faraja ambao wanahitaji wapate msuko suko ili wapate kuamka, hawa wenye moyo kama jiwe na hawajuhi kulia.  Kuna haja hata ya kuamsha watu ambao hawajui kusikitikia uchungu wa wengine. Akotolea mfano wa matanga anasema ni njia chungu lakini ambayo ni muafaka wa kufungua macho kuhusu thamani takatifu isiyo badilishwa na kila mtu na kwa maana hiyo inatoa fursa ya kuwa na utambuzi ni kwa jisngi gani maisha yetu hapa duniani ni mafupi.

Njia nyingine ya kuliwa kwa ajili ya dhambi

Kuna maana nyingine kinyume na heri hasa ya kulia kwa ajili ya dhambi. Hapa kuna haja ya kutofautisha, kwa maana kuna anayeshikwa hasira kwa sababu amekosea. Na kumbe hicho ni kiburi. Kinyume chake kuna anayelia kwa sababu ya ubaya aliyo utenda  na ambao amekosa kutenda wema na kusaliti uhusiano wake na Mungu. Kwa hakika hicho kilio cha ndani ya moyo kwa maana ya kumkosea mwingne. Ni kulia kutokana na kwamba hukufanya vema na ndiyo maana ya dhambi. Huyo mtu anasema nimedhuru nimpedaye na imememuhuzunisha hadi kufikia machozi. Mungu ashukuriwe hasa kufika hatua ya kutoa machozo Papa Francisko amesema. Hii  ndiyo mada ya makosa ya kukabiliana nayo ambayo ni vigumu kuzuia na ndiyo uhai. Papa ametoa mfano wa kufikiria machozi ya Mtakatifu Petro yaliyomfikisha katika upendo mpya na wa kweli zaidi. Machozi yanatakasa na kupyaisha. Petro alimtazama Yesu na kulia.  Moyo wake ulipyaishwa. Tofauti na Yuda  ambaye hakukubali kosa lake, maskini hadi kufikia kujiua mwenyewe.

Zawadi ya Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu

Kujua dhambi ni zawadi ya Mungu, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Sisi peke yetu hatuwezi kujua dhambi. Ni neema ambayo tunapaswa kuiomba. Ee Bwana ili niweze kutambua mabaya ambayo nimefanya au ambayo nitafanya. Hiyo ni zoezi kubwa na baada ya kujua hilo  ni kulia kwa uchungu sana wa kuomba toba. Aidha ametoa mfano mwingine kwamba mmoja wa mmonaki wa kwanza, Efraim wa Siro anasema kuwa uso uliolowanishwa na machozi ni mzuri sana (hotuba ya kiroho)  huo ni uzuri wa kutubu, uzuri utokanao na  machozi ya kina ya toba. Kama ilivyo hekima ni heri yule anayepokea uchungu unaoshikamana na upendo kwa sababu anatafakari  kutoka kwa Roho Mtakatifu ambaye ni huruma ya Mungu anaye tusamehe na kukosoa

Mungu anasamehe daima,sisi tunachoka kuomba msamaha

Mungu anasamehe damia. Tusisahu hilo Papa amesisitiza. Hata dhambi zilizo mbaya sana. Tatizo letu ni kwamba sisi tunachoka kuomba msamaha, tunajifungia sisi binafsi na wala hatuombi msamaha. Ndilo tatizo kubwa wakati yeye yupo pale kwa ajili ya kusamehe. Papa Francisko amfafanua kuwa tunapaswa kuzingatia kuwa “Mungu Hakututendea sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu”. Kutoka Zaburi. Tunaishi kwa huruma yake na upendo wake. Kwa njia hiyo amehitimisha akiomba Bwana atujalie kupenda kwa wingi na upendo wa tabasamu, kwa ukaribu, kwa huduma hata kwa machozi.

12 February 2020, 13:07