Tafuta

Vatican News
Kuhudumia ndugu  anayeteseka maana yake ni kuweka nafasi ya Bwana.Ni wagonjwa na watu wadhaifu  katika majengo ambamo wahudumu wanawezesha kuwa karibu Kuhudumia ndugu anayeteseka maana yake ni kuweka nafasi ya Bwana.Ni wagonjwa na watu wadhaifu katika majengo ambamo wahudumu wanawezesha kuwa karibu   (ANSA)

Papa:wagonjwa siyo namba wanahitaji ukaribu na si mantiki kiuchumi!

Papa alipokutana na Kikundi cha Villa Maria care and research,ambacho ni hali halisi inayojikita katika sekta ya Afya amewakumbusha ukaribu kuwa ni njia iliyotumiwa na Mungu ili kutukuomba.Wagonjwa na wanaoteseka ni ishara hai ya uwepo wa Kristo.Ni matashi ya Papa ya kuanza utamaduni mpya wa huduma ya maisha ya kibinadamu katika maono ya maandalizi ya kiufundi na kimaadili kwa wahudumu wa afya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa kikundi cha Kituo cha Utunzaji na utafiti kiitwacho Villa Maria, tarehe Mosi Februari 2020 mjini Vatican. Amewakaribisha wawakilishi wote wakiwa ni madaktari, manesi, wakuu tawala na wahudumu wote kwa ujumla. Papa Francisko amebainisha juu ya kusikiliza kwa makini hotuba ya mwenyekiti wa kituo hicho cha afya na ambacho anasema  kinaongozwa na malengo muhimu ya maisha kwa miaka arobaini, katika lengo la sekta ya  afya na huduma ya afya ya watu. Anawapongoza kwa mwendelezo ambao wameounesha hadi leo hii katika shughuli zao nchini Italia zaidi hata katika nchi nyingine, ikiwa  daima ni kutoa huduma ya maisha ya binadamu wanaoshambuliwa na udhaifu na magonjwa. Anawashukuru kwa kujikita kwao katika shughuli waliyoanzisha na kuwatakia kwamba miundo ya majengo, mahali pa mateso, lakini hata ni penye matumaini, uzoefu wa kibinadamu na kiroho, na kwamba wanaweza daima kupata mshikamano ulio tayari na umakini kwa watu ambao wanaumwa

Maendeleo ya teknolojia ya kijamii, kiuchumi na kisiasa

Mapinduzi ya teknolojia na maendeleo yenye asili ya kijamii, kiuchumi na kisiasa Papa Francisko amesema yameleta mabadiliko makubwa ndani mwake na ambamo maisha yanaegemea kwenye mahospitali na majengo yote ya afya.  Lakini hapo ndipo kuna ulazima wa kuwa na  utamaduni mpya hasa katika kujiandaa kiufundi na kimaadili kwa upande wa wahudumu wa wafya kwa ngazi zote.  Katika muktadha huo, Papa anasema  ni muhimu kuendeleza kile ambacho  kimefanyika hadi sasa kama  Kikundi cha Villa Maria ili kwenda kukutana na dharura za wagonjwa na familia zao, ambao mara nyingi wanalazimika kuhamia katika vituo maalum vilivyo mbali sana na maeneo yao.

Papa anasema kuna mahitaji ya kuwa na jitihada za kuongeza mwanga wa matendo kwa ajili ya ununuzi au kuunda majengo mapya na kupanua kwakwe, kuwa na uhakika wa zana za kisasa na ulazima kwa ajili ya wagonjwa na kwa ajili ya uponyaji wao. Ili kufikia malengo haya, inahitajika kuepuka kufyonzwa na mifumo inayolenga tu sehemu ya kifedha-kiuchumi, walakini katika  kutekeleza mtindo wa ukaribu na mtu huyo, ili kuweza kuwasaidia kwa  joto la kibinadamu mbele ya wasiwasi unaowekeza katika wakati mgumu zaidi wa ugonjwa. Kwa njia hiyo inachangia kwa dhati dawa ya kibinadamu na hospitali na ukweli wa afya.    

 Yote mliyotendea wadogo hawa ni kwa ajili yangu

Papa Francisko akitaka kuwaonesha ukweli wa uduuma yao unatokana na nini kama wakristo anasema: “Kwa wale ambao wanajitambua kama wakristo, wanaalikwa kutoa huduma katika roho ya maneno ya Yesu yasema: “ Yote ambayo mlitenda kwa ajili ya hawa wadogo mlinifanyia mimi Mt 25,40. Hapo ndipo ndipo kuna  injili msingi ya huduma kwa jirani. Na kwa kufanya hivyo wagonjwa na wanaoteseka wanakuwa ka yule aliye na imani ishara hai ya uwepo wa Kristo, Mwana wa Mungu aliyekuja kutibu na kubeba udhaifu wetu wetu”. Kuhudumia ndugu  anayeteseka maana yake ni kuweka nafasi ya Bwana.

Katika maneno hayo na mafunzo na uchungu kuna hata ujumbe wa maisha kwa wote; kuna funzo kubwa sana ambalo hakuna darasa lolote linaweza kuzidi hapo, amesisitiza Papa. Mtu anayeteseka kwa hakika anahitaji zaidi na thamani ya zawadi ya Mungu ya wokovu na imani na inasaidia hata wale ambao wako karibu kushukuru na kutafuta zawadi kama hiyo. Ni wagonjwa na watu wadhaifu  katika majengo yao ambamo wanawezesha kuwa karibu ,  na ambao Papa Mwenyewe anawaomba wamfikishie salam zake.  Anasema kwamba yeye “anaungana nao katika matarajio ya kupona, kwa kushirikishana kiroho na  majaribu na matarajio ya uponywaji, na ili kila mmoja aweze kurudi katika familia yake. Kwa wote Baba Mtakatifu amehitimisha kwa kuwapa baraka na kuwatumia baraka.

01 February 2020, 14:38