Tafuta

Vatican News
Leo hii tunaalikwa kufikiria na kijiuliza “je mwelekeo wangu huko kwa Bwana au kwangu binafsi?Anayetambua kujua kwanza neema ya Mungu anaigunduambele ya ukosefu wa imani na tamanio la  kidunia Leo hii tunaalikwa kufikiria na kijiuliza “je mwelekeo wangu huko kwa Bwana au kwangu binafsi?Anayetambua kujua kwanza neema ya Mungu anaigunduambele ya ukosefu wa imani na tamanio la kidunia  (Vatican Media)

Papa:maisha ya kitawa ni kuona neema,kutumaini na kumtafuta jirani!

Kutazama kwa kina historia binafsi ya zawadi ya Mungu na kupyaisha mtazamo kwa mwanga wa neema ya Mungu bila kuteleza kwenye mambo ya kidunia ndiyo umekuwa mwaliko wa Papa Francisko kwa watawa wote katika maadhimisho ya misa kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro Vatican wakati wa mkesha wa Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni sambamba na Siku ya Watawa duniani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Macho yangu yameuona wokovu (Lk 2,30) ni maneno ya Simeoni ambayo yanawakilishwa katika Injili na kuoneshwa kama aliye kuwa mtu rahisi, mtu mwenye haki. Lakini kati ya watu wote waliokuwamo katika hekalu ni yeye tu aliyemwona Yesu Mwokozi. Je aliona nini? Aliona mtoto mdogo, mdhaifu  na rahisi. Japokuwa  alikuwa ni mwokozi kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa amemfanya atambue ukweli wa mtoto Kristo wa Bwana. Na baada ya kumwekwa kwenye mikono yake alihisi imani ambayo ilikuwa ni ya Mungu katika kutimiza ahadi yake.

Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Papa Francisko wakati wa kuadhimisha misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Jumamosi jioni tarehe 1 Februari 2020 wakati mkesha wa kuadhimisha Siku Kuu ya Kutolewa kwa Bwana Hekaluni, sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Watawa duniani. Papa Francisko akiendelea na mahubiri hayo anasema Simeoni kwa wakati huo alikuwa anaweza kwenda kwa amani kwa maana alikuwa ameona neema ambayo inafaa  maisha na hakuwa anasubiri jambo jingine. Papa anasema “ hata ninyi  kaka na dada, watawa  ni watu rahisi ambao mmeona tunu inayostahili zaidi ya vitu vingine duniani”. Na kwa maana hiyo waliamua  kuacha  yote yenye thamani kwao kama vile mali na  kuunda familia yao.  Lakini je ni kwa nini walifanya hivyo? Papa auliza na kutoa jibu: Ni kwa sababu walivutiwa na upendo wa Yesu na kuona kuwa Yeye ndiye kila kitu na kuvutiwa kwa haraka mtazamo wake na kuacha yote yanayobaki.

Maisha ya kitawa yako katika maono hayo, ni kuona kile kilicho muhimu katika maisha. Ni kupokea zawadi ya Bwana na kuikumbatia kwa mikono wazi kama alivyo fanya Simeoni. Na tazama ni kitu gani watawa wanaona kwa macho yao: neema ya Mungu iliyowekwa kwenye mikono yao. Aliyewekwa wakfu ni yule ambaye kila siku anatazama na kusema yote ni neema. Papa anabainisha kwamba “tulichaguliwa bila kustahili katika maisha ya kitawa kwa maana tuna zawadi ya upendo ambao tumeupokea”.

Macho yangu yameona wokovu wako:ibilisi, vishawishi vya dunia

Haya ni maneno tunayorudia katika sala za usiku kabla ya kulala. Katika sala hiyo tunahitimisha siku tukisema: “Bwana wokovu wangu unatoka kwako, mikono yangu siyo mitupu, bali imejaa neema yako”. Ni kutambua kutazama neema ni hatua ya kuanzia. Kwa kutazama nyuma na kuona historia binafsi na kuziona kwa mara nyingine tena zawadi za uaminifu wa Mungu. Papa anashauri lakini si kuona katika kipindi kikuu cha maisha, bali hata katika hali ya udhaifu, na udogo wetu. Ibilisi anajitokeza mara nyingi katika udhaifu wetu, na katika utupu wetu. Hata baada ya  miaka mingi hujawa bora  hujatimiza kile ambacho ungeweza, hakukuacha ufanye kile ulicho dhamiria, hujawa mwaminifu , huna uwezo...” Tunaona kwa upande ni kweli na kwenda mbele na mawazo na hisia ambazo zinatupoteza”.   Papa Francisko akiendelea kubainisha juu ya kishawishi kinachokumba zawadi ya Mungu anasema,  Mungu daima anapenda yule anayejitoa zawadi hata udhaifu wetu. Tukitazama uso wake na kujifungua katika msamaha anapyaisha na kutuimarisha imani yetu.

Leo hii tunaalikwa kufikiria na kijiuliza “je mwelekeo wangu huko kwa Bwana au kwangu binafsi?. Anayetambua kujua kwanza neema ya Mungu anaigundua mbele ya ukosefu wa imani na tamanio la  kidunia. Kwanini katika maisha ya kitawa yanakumbana na kishawishi hiki, yaani kuwa na mtazamo wa kidunia?. Ni mtazamo ambao hauoni tena neema ya Mungu kama kiongozi wa maisha yake na kwenda kutafuta sehemu nyingine kama zile za mafanikio, faraja ya mapenzi na hatimatìye kila ambacho anataka kufanya.

Lakini maisha ya kitawa hayaendi katika mambo hayo, ni  katika neema ya Mungu kwakuwa katika yeye  yamejitenga na  umimi. Kwa maana baadaye ni kupoteza kabisa nafasi na haki  yake, anaajiachia kuteleza katika masengenyo na mabaya, vishawishi vinakuondolea kila aina ya hadhi na kukupeleka mbali kukugeuza ufanye litania ya malalamiko dhidi ya kaka na dada katika jumuiya unayoishi, juu ya Kanisa na jamii kwa ujumla. Hakuna kuona Bwana kwa kila kitu, bali ni kuona dunia na mambo yake wakati ndani ya moyo unajazwa na huzuni na kukata tamaa matokeo ni kishindwa. Huo ndiyo mtazamo wa kidunia. Papa ametoa  mfano akimtaja  Mtakarifu Teresa wa mtoto Yesu kuwa kuhusiana na suala hili alisema: ole  wake mtawa yoyote anayesema sijatendewa haki”.

Macho yangu yameona wokovu wako:kuishi kwa ajili ya huduma

Simeoni aliona Yesu mtoto, mnyenyekevu aliyekuja kwa ajili ya kuhudumia na siyo kitumikiwa na anajìeleza mwenyewe kama mtumishi. Yeye anasema : “sasa waweza acha mtumishi wako ee Bwana aende kwa amani”... Anayekazia macho yake kwa Yesu anajifunza kuishi kwa ajili ya huduma. Hasubiri wengine waanze bali, anajikita kutafuta jirani kama Simeoni Amesisitiza Papa. Je katika maisha ya kitawa, jirani anapatikana wapi? Hili ni swali, jirani yangu yuko wapi? Awali ya yote katika jumuiya binafsi. Ni lazima kuomba neema ya kujua namna ya kutafuta Yesu katika ndugu, kaka na dada ambao wamepokelewa. Ni pale unapoanzia zoezi la upendo. Nafasi ambayo unaishi kwanzaa kwa kupokea kaka na dada na  umaskini wao kam Simeoni alivyompokea Yesu kwa urahisi na maskini.

Leo hii Papa anasema kuna tabia ya kuona wengine kama vizingiti na usumbufu. Kuna haja ya kitafuta na kuwa na mtazamo wa jirani, ambaye ni wa kukaribia aliye mbali Watawa wa kike na kiume,wanawake na waname ambao wanaishi kwa ajili ya kumuiga Yesu wanaalikwa kuweka duniani  mtazamo huo huo wa huruma, mtazamo ambao unakwenda kutafuta walio mbali, mtazamo ambao hautoi hukumu bali kutia moyo, huru, fariji, na mtazamo wa huruma. Katika Injili kuna kiitikio cha mara kwa mara kisemacho Yesu alishikwa na huruma. Ni kuinama kwa Yesu kuelekea kwa kila mmoja wetu.

Macho yangu yameona wokovu wako: tumaini na mtazamo

Macho ya Simeoni yaliona wokovu kwa sababu alikuwa anasubiri.Yalikuwa ni macho yaliyokuwa yanasubiri na kutumaini. Yalikuwa yanatafuta mwanga na kuona mwanga wa watu. Yalikuwa macho ya uzee, lakini yaliyofungulia matumaini. Mtazamo wa watawa hauwawezi kutokuwa na mtazamo wa matumaini, anafafanua Papa. Ni kutambua matumaini japokuwa anaongeza, kutazama kinachotuzunguka ni rahisi kupoteza tumaini ya mambo mengi ambayo  hayaendi, upungufu wa miito,...bado vishawishi vya kidunia vinavyoangusha matumaini. Lakini kwa kutazama Injili na pia Simeoni na Anna, walikuwa ni wazee  napeke yao lakini hawakupoteza tumaini, kwa maana walikuwa wanawasiliana na Bwana. Anna hakuwa anakwenda mbali na hekalu akihudumia Mungu usiku na mchana kwa kufunga na sala. Siri iko hapo, Papa anasisitiza yeye hakwenda mbali na mtazamo na Bwana,.kisima cha matumaini. sisi ni vipofu iwapo hatutazami Bwana kila siku na  kuabudu Bwana. Baba Mtakatifu anawaomba kushukuru Mungu kwa kwa zawadi ya maisha ya kitawa na kuomba  kuwa na mtazamo mpya ambao unaona neema na kutafuta ukaribu ambao unatambua kutumainia . Na kwa kufanya hivyo macho yetu yataona wokovu.

 

01 February 2020, 18:23