Papa amesema anapotoa ushauri kwa wanandoa wapya hasa wanaomwomba ni namna gani waweze kupeleka mbele ndoa yao anawambia maneno matatu muhimu, kuomba ruhusa, asante, samahani Papa amesema anapotoa ushauri kwa wanandoa wapya hasa wanaomwomba ni namna gani waweze kupeleka mbele ndoa yao anawambia maneno matatu muhimu, kuomba ruhusa, asante, samahani  

Papa:Maneno matatu muhimu ni kuomba ruhusa,asante na samahani!

Papa Francisko mara baada ya katekesi yake hakusahau kuwasalimia vijana,wazee,wagonjwa na wanandoa wapya. Hata hivyo katika katekesi yake,amerudia kuwakumbusha maneno matatu msingi ambayo hayapaswi kukosa katika familia ya kikristo nayoni kuomba ruhusa,asante,samahani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya tafakari ya Katekesi kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI mjini  Vatican tarehe 5 Februari 2020 amwasalimia kutoka mataifa mbalimbali. Hata hivyo katika katekesi yake,amerudia kuwakumbusha maneno matatu msingi ambayo hayapaswi kukosa katika familia ya kikristo nayoni kuomba ruhusa, asante, samahani. 

Sisi sote hatujakamilika maana ni wadhaifu

Papa Francisko akiendelea amebainisha kuwa kila mtu nafsini mwake, anajua vema kwamba hata kama atajaribu kufanya vipi yeye daima huwa hajakamilika na ni mdhaifu. Hakuna ujanja ambao unafunika udhaifu huu. Kila mmoja wetu ni mwathirika wa ndani. Na kwa maana hiyo lazima aone ni wapi.  Akitoa mfano Papa anasema: “Ni kwa jinsi gani unaishi vibaya ikiwa unakataa mipaka yako! Unaishi vibaya. Kikomo hakikichimbwi, ni pale. Watu wenye kiburi hawaombi msaada, hawaombi msaada kwa sababu wanataka kujidhihirisha kuwa wao wanajitosheleza. Watu kama hao wanahitaji msaada lakini kiburi chao kinawazuia kuomba msaada. Jinsi gani ilivyo nguvu kukubali makosa na kuomba msamaha!  amesisitiza.

Ikiwa tunateleza katika makosa omba msamaha

Papa Francisko ametoa mfano mwingine kwamba yeye anapotoa ushauri kwa wanandoa wapya hasa wanaomwomba ni  namna gani  waweze kupeleka mbele ndoa yao anawambia: “ Kuna maneno matatu muhimu: “kuomba ruhusa, asante, samahani ”. Ni maneno ambayo hutokana na umaskini wa roho. Siyo lazima uingilie kati, lakini omba ruhusa. Je ni vema kufanya hivyo? Anauliza Papa Francisko. Kwa namna hiyo kuna majadiliano ndani ya familia kati ya bi arusi na bwana arusi wanajadiliana.  “Wewe umefanya hivyo kwa ajili yangu, ...asante  nilikuwa na hitaji”. Na ikiwa unateleza katika makosa, daima ni kuomba samahani”. Papa Francisko aidha ametoa mfano mwingine wa  wanandoa wapya kama wale waliokuwapo kuwa,  mara nyingi wanamwambia neno la tatu ni gumu hasa la kuomba msamaha. Lakini hiyo ni kutokana na kiburi, kwa maana mwenye kiburi anasema, hawezi kufanya hivyo. Hawezi kuomba msamaha kwani anaona hajakosea. Huyo si maskini wa roho.

Bwana hachoki kusamehe: ni ugonjwa kukosa kuomba msamaha

Kinyume chake Bwana hachoki kamwe kusamehe; kwa bahati mbaya Papa amebainisha sisi tunachoka kuomba msamaha (Angelus 17 marzo 2013). Uchovu wa kuomba msamaha ni ugonjwa mbaya sana! Ni kwanini inakuwa vigumu kuomba msamaha? Kwa sababu sura zetu za kinafiki zinakosa unyenyekevu. Pamoja na hayo kuishi kwa kujaribu kuficha mapungufu binafsi ni kazi ngumu na ya kuhuzunisha. Yesu Kristo anatuambia: kuwa maskini ni fursa ya neema; na inatuonyesha njia ya kuondokana na  ugumu huo.

 

05 February 2020, 13:13