Katika warsha iliyofanyika kwa wanauchumi,wanabenki na mawaziri wa benki Papa katika hotuba yake anasema sehemu zenye utajiri na zenye uchumi ulioendelea zinaweza na zinapaswa kusitisha umasikini na kutoa majibu ya ubunifu. Katika warsha iliyofanyika kwa wanauchumi,wanabenki na mawaziri wa benki Papa katika hotuba yake anasema sehemu zenye utajiri na zenye uchumi ulioendelea zinaweza na zinapaswa kusitisha umasikini na kutoa majibu ya ubunifu. 

Papa:Inawezekana kushinda ukosefu wa usawa na umaskini kwa njia ya matajiri kujali ubinadamu!

Katika warsha iliyofanyika Casina Pio IV mjini Roma kwa kuongozwa na mada “njia mpya za udugu wa mshikamano,wa kuunganisha,kufungamanisha na ubunifu”,Papa Francisko amehitimisha kwa hotuba yake jioni tarehe 5 Frebruari 2020 akihimiza nchi na watu matajiri kujihusisha katika suala la usitishaji wa umasikini.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko katika hotuba yake jioni tarehe 5 Februari 2020 kwa wanabenki, wanauchumi, na mawaziri wa fedha waliounganika katika Taasisi ya Kipapa ya Sayansi Jamii kwa kuongozwa na mada “njia mpya za udugu wa mshikamano, wa kuunganisha, kufungamanisha na ubunifu, amesisitiza kuwa inahitaji muundo mpya wa ujenzi wa fedha kimataifa ambao utaweza kusaidia maendeleo ya nchi zilizo maskini. Hatujahukumiwa kuwa na ukosefu wa usawa kijamii na wala kukandamizwa mbele ya ukosefu wa haki. Sehemu zenye tajiri na zenye uchumi ulioendelea zinaweza na zinapaswa kusitisha umasikini kwa kutengeneza majibu ya ubunifu, ili kuunganisha na kuwalisha wale walio wa mwisho, badala ya kuwabaugua.  Kwa kuundwa kwa usanifu ulio mpya wa kifedha kimataifa unaounga mkono maendeleo ya nchi masikini, unaweza kupunguza deni lao, bila ushuru mkubwa, ukwepaji na utapeli wa pesa chafu ambazo zinaibiwa jamii, na serikali zinazotetea haki na faida ya wote kwa heshima ya maslahi ya kampuni zenye nguvu na kimataifa.Papa amesema.

Tufanye kazi pamoja dhidi ya ukosefu wa haki kiuchumi ulimwenguni

Kwa kuonesha juu ya Mafundisho jamii ya  Kanisa yanavyofanya kazi, Papa Francisko amependekeza kwa wanabenki, wachumi na mawaziri wa fedha duniani kote, walioalikwa mjini Vatican katika Taasisi ya Sayansi kijamii katika warsha hiyo. Hata hivyo nia  Papa Francisko ni kuwahusisha katika kazi ya pamoja ili kuweza kusitisha ukosefu wa haki katika uchumi wa sasa duniani. Kwa maana hiyo anasema “sisi ni washiriki wa kazi ya Bwana ambayo inaweza kubadili mchakato wa historia kwa ajili ya hadhi ya kila mtu leo hii na kesho hasa wale ambao wametengwa na kwa ajili ya wema mkubwa wa amani.”

Dunia ni tajiri lakini mamilioni ya watu hawana chakula

Papa Fracisko akiendelea na hotuba yake kwa washiriki wa warsha hii anatumia takwimu za hali halisi ya sasa na kusema kwamba, “dunia ni tajiri, lakini bado umaskini unazidi kuongezeka karibu nasi. Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya mwaka huu ya mapato ya dunia yatakuwa karibu dola za kimarekani  12,000 kwa mwaka huu. Na wakati huo bado mamia ya mamilioni ya watu wanaishi katika mazingira ya umaskini uliokithiri, bila chakula, makazi, huduma za afya, shule, umeme, maji safi na usafi wa kutosha na vitu muhimu vya lazima.

Watoto milioni 5 watakufa kwa umaskini

Papa anaongeza kusema kuwa “wastani wa watoto milioni tano chini ya umri wa miaka mitano watakufa kutokana na sababu ya umaskini mwaka huu. Watoto wengine milioni 260 hawatapata elimu kutokana na ukosefu wa rasilimali, vita na uhamiaji. Hali, kama hii analaani Papa, kuwa “imesababisha mamilioni ya watu waathirika kwa usafirishwaji na aina mpya za utumwa, kama vile kulazimishwa kazi, ukahaba na usafirishaji wa viungo vya binadamu. Hawana haki na dhamana; hata hawawezi kufurahia urafiki au na familia.”

Hatuhukumiwi kuwa na ukosefu wa usawa kijamii

Hata hivyo hali halisi hiyo kiukweli anafafanua Papa Francisko kuwa, siyo lazima iwe sababu ya kukata tamaa, bali ni kujikita katika  matendo kwa sababu hizi ni shida zinazoweza kutatuliwa na siyo ukosefu wa rasilimali. “Ninarudia: hatuhukumiwi kukosa usawa wa ulimwengu”. Hii inafanya kuwa na uwezekano wa njia mpya ya kushughulikia matukio, ambayo huruhusu kupata na kutoa majibu ya ubunifu kwa ajili ya mateso ya kuepukika ya watu wengi wasio na hatia; hii inamaanisha kukubali kuwa, katika hali nyingi, tunakabiliwa na ukosefu wa utashi na azimio la kubadili mambo na, zaidi ya yote, vipaumbele”.

Katika utajiri na mbinu zilizopo leo hii hakuna kutafuta sababu zaidi

Papa Francisko aidha anasema katika utajiri na mbinu zilizopo leo hii, haiwezekani kukwepa. Ni suala la kujiuliza na kuona ukweli huu kwa mwanga mpya. Kwa sababu, ulimwengu ulio na utajiri na uchumi wenye nguvu unaweza kumaliza umaskini. Nguvu zenye uwezo wa pamoja, zinaweza kuzalishwa, kulisha, kutunza na kuvalisha walio wa mwisho katika jamii badala ya kuwatenga. Ni suala la kutoa kipaumbele. Ikiwa ni kukuza mifumo ya kijamii na kiuchumi ambayo inaboresha jamii, au, kwa upande mwingine, mfumo ambao unasahihisha vitendo ambavyo vinaweza tu kuongeza kiwango cha ukosefu wa haki na dhuluma ya kijamii. Leo, hii kiwango cha utajiri na mbinu iliyokusanywa na ubinadamu, na vile vile umuhimu na dhamana ambayo haki za binadamu zimepata, hairuhusu kukwepa kwa samahani tena! Amesisitiza Papa Francisko

Watu zaidi ya 50 duniani matajiri wanaweza kuokoa mamilioni ya maisha

Sisi sote tunawajibika, Papa anaendelea, kwa kuwa tumeruhusu pengo kati ya umaskini uliokithiri na (kwa upande wake, utajiri ukiongezeka kuwa mkubwa zaidi katika historia). Watu tajiri hamsini ulimwenguni wanayo urithi mkubwa. Watu hawa hamsini peke yao matajiri wanaweza kufadhili utunzaji wa afya na elimu ya kila mtoto masikini ulimwenguni, kupitia ushuru au kupitia mipango ya uhisani au zote mbili. Watu hawa hamsini wanaweza kuokoa mamilioni ya maisha kila mwaka”

Hatima la muundo wa fedha ni dhambi

Utandawazi wa kutojali, Papa Francisko anakumbuka, umeitwa “kutokuwa na uwezo”. Mtakatifu Yohane Paulo II aliuita  kuwa ni “miundo ya dhambi”. Miundo ambao, Papa, anasema “hupata hali nzuri ya upanuzi wa ustawi wa kila wakati, unapopunguzwa au kwa sekta fulani au uchumi na fedha unageuka kuwa wenyewe, kama ibada ya sanamu ya pesa, tamaa na uvumi. Ubunifu mkubwa wa kiteknolojia huruhusu shughuli za leo za haraka sana na unaruhusu kutoa faida kubwa ambayo haifungamani na michakato ya uzalishaji au kwa uchumi wa kweli”. Ni uvumi wa kifedha, uliolaaniwa na Aristotle, kwa sababu ndani yake pesa  inakuwa yenye tija, amefafanua Papa. Mafundisho Jamii ya Kanisa, Papa Francisko anasisitiza yanaelekeza mitindo kwa  serikali na benki wakati zinatimiza kusudi lao, ambalo ni kutafuta mema ya kawaida, haki ya kijamii, amani, na vile vile maendeleo muhimu ya kila mtu, ya kila jamii, binadamu na watu wote.

Hawakati ushuru kwa matajiri na walipa kodi

Papa Francisko amebainisha kwamba Mafundisho ya  Kanisa linaonya, kwamba taasisi hizi zenye faida, za umma na za binafsi, zinaweza kutumbukia katika miundo ya dhambi. Miundo ya dhambi leo ni pamoja na kupunguzwa kwa ushuru kwa watu tajiri, mara nyingi huhesabiwa haki kwa jina la uwekezaji na maendeleo; Kodi kubwa kwa faida binafsi ya makampuni,na uwezekano wa ufisadi wa makampuni mengine makubwa ulimwenguni, mara nyingi hupatana na uanzishwaji wa kisiasa ulioko madarakani. “Kila mwaka mabilioni ya dola, ambayo yanapaswa kulipwa ushuru ili kufadhili huduma za afya na elimu, hujilimbikizia katika akaunti za nyumba za ushuru, hivyo kuzuia uwezekano wa maendeleo yenye heshima na endelevu kwa watendaji wote wa kijamii.

06 February 2020, 10:55