Katekesi ya Papa Francisko tarehe 19 Februari 2020 Katekesi ya Papa Francisko tarehe 19 Februari 2020 

Papa Francisko:Kiwango cha upole kinapimwa kupitia magumu!

Heri wenye upole, maana watairithi nchi,ndiyo heri ya tatu ambayo Papa Francisko amejikita nayo katika katekesi yake tarehe 19 Februari 2020 na kufafanua kwamba hakuna ardhi nzuri zaidi kuliko mioyo ya wengine,hakuna eneo zuri zaidi la kupatikana kwa amani na nduguyo.Na hiyo ndiyo nchi itakayorithiwa kwa upole!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika Katekesi yake kwa mahujaji na waamini waliofika katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Jumatano tarehe 19 Februari 2020 akiwa katika mwendelezo wa tafakari kuhusu heri za mlimani amendeleza kujikiata katika heri ya tatu kati ya Nane  za Injili ya Matayo, isemayo “Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi” (Mt 5,5). Neno upole hapa lina maana ya kusema, mkarimu, mpole na bila kuwa na dhuluma. Upole unajionesha hasa wakati wa migogoro, unajionesha ni kwa namna gani ya kukabiliana na hali ya ugumu. Kila mtu anaweza kufikiria ni mpole ikiwa kila kitu kina utulivu, lakini je, anajionesha namna gani wakati wa shinikizo, iwapo anashambuliwa, anaudhiwa na kudharauliwa?

Katika sehemu ya somo la Mtakatifu Paulo anabainisha upole na wema wa Kristo (2 Kor 10,1). Mtakatifu Petro kwa mara nyingine anakumbusha tabia ya Yesu wakati wa Mateso kuwa “ alipotukanwa  yeye hakujibu kwa tukano, alipoteseka  yeye hakutoa vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki  (1Pt 2,239) Upole wa Yesu ulijionesha kwa nguvu zote katika Mateso. Katika Maandiko Matakatifu, neno upole linaelekeza hata yule ambaye hana ardhi yake binafsi: kwa maana hiyo inashangaza jambo hili la heri ya tatu kwa hakika kusema kuwa “wapole watairithi nchi”. Kwa dhati heri hii ya “upole inatajwa katika Zaburi ya 37, ambayo imesomwa mwanzoni mwa Katekesi. Papa Francisko amesisitiza; Zaburi hiyo inasema “Umtumaini Bwana ukatende mema, ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya. Maana watenda mabaya wataharibiwa, bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi. Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo. Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo. Bali wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani. (Zab 37, 3.8-11)”.

Kwa kufafanua amesema hatua hiyo inaeleza kuhusua upole na umiliki wa ardhi. Mambo haya mawili, kwa kufikiria vema, utafikiri hayaendeani. Kwa hakika kumiliki ardhi ni katika mantiki ya aina za migogoro, kwa mfano wanaopambana mara nyingi ni kwa ajili eneo, ili kuweza kutawa katika eneo fulani. Katika vita mwenye nguvu anashinda na kupata ardhi nyingine. Lakini tutazame vizuri neno lililotumika kwa kuelezea umiliki wa wenye upole. Hawa siyo kwamba wanapata ardhi; haisemi heri wao kwa sababu watapata ardhi “hapana, Heri haisemi hivyo. Bali “wao watairithi”. Heri wenye upole maana wao watairithi nchi. Papa amefafanua vema .

Katika Maandiko Matakatifu, neno “kurithi” lina maana, tena kubwa sana. Watu wa Mungu wanaitwa kurithi nchi yao Israeli ambayo ni Nchi ya ahadi.  Nchi ile ni ahadi na zawadi ya watu wa Mungu.  Na inageuka kuwa kitu kikubwa sana na rahisi katika eneo hilo. Kuna nchi ambayo ni Mbingu, yaani nchi, mahali ambamo tunatembea kuekelea katika mbingu mpya na nchi mpya  (soma Is 65,17; 66,22; 2 Pt 3,13; Mdo 21,1). Kwa maana hiyo mpole ni yule ambaye anarithi kwa kiasi kikubwa eneo. Yeye siyo mwoga, “mdhaifu” ambaye hupata maadili ya haraka ya kujikunja na kukaa nje na shida. Mbali na hilo! Yeye ni mtu ambaye amepokea urithi na hataki kuupoteza. Mpole siyo mtu wa kutulia, lakini ni mfuasi wa Kristo ambaye amejifunza kutetea vema nchi nyingine. Yeye anatetea amani, anatetea uhusiano wake na Mungu, hutetea au kulinda zawadi zake, zawadi za Mungu, kuhifadhi huruma, udugu, imani, na matumaini. Kwa sababu watu wapole ni watu wenye huruma, kiasi na imani, na watu wenye matumaini.

Papa Francisko aidha amependa kutaja hata juu ya dhambi ya hasira, iliyo kinyume, kwani amesema ni ghadhabu mbaya ya nguvu ambayo kila mmoja anatambua.  Ni nani ambaye hajawahi kikasirika? Papa anau,iza na kutoa jibu kuwa ni  wote! Tunapaswa kuielekea heri na kujiuliza ni mambo mangapi tumeharibu kutokana na hasira? Ni mambo mangapi tumepoteza? Papa Francisko amebainisha kuwa  wakati wa ghadhabu, unaweza kuharibu mambo mengi, unaweza kutojithibiti na wala hakuna kutathimini kile ambacho ni muhimu kweli, na unaweza kuharibu uhusiano na ndugu, na wakati mwingine bila kuweza kuurudisha. Kwa njia ya kisirani ndugu wengi hawazungumzi tena, wanaachana mmoja na mwingine.  Ni kinyume na upole, kwa maana upole unaunganisha, wakati hasira inatenganisha.

Upole unakuwezesha kupata mambo mengi. Upole una uwezo wa kushinda moyo, kuokoa urafiki na mambo mengi, kwa maana watu wanakuwa na hasira lakini baadaye wanatulia, wanafikiria kwa upya na kurudia katika hatua zao za safari na kwa maana hiyo inawezekana kujenga upya urafiki kwa njia ya upole. Nchi itakayoshinda kwa upole ni wokovu wa huyo ndugu aliyetajwa katika Injili ya Mathayo mwenyewe kwamba: “ikiwa atakusikiliza, umempata nduguyo (Mt 18,15). Papa amesisitiza kwamba hakuna nchi nzuri zaidi ya moyo wa mwingine, lakini tufikire hili kwamba  hakuna ardhi nzuri zaidi kuliko mioyo ya wengine na hakuna eneo zuri zaidi la kupatikana kwa amani na nduguyo. Na ndiyo hiyo nchi itakayorithiwa kwa upole.

19 February 2020, 12:43