Vatican News
Papa Francisko akiwa anawasalimia vijana watumikiaji kanisani mara baada ya katekesi yake Papa Francisko akiwa anawasalimia vijana watumikiaji kanisani mara baada ya katekesi yake   (Vatican Media)

Papa Francisko:salam kwa mahujaji na waamini wote!

Papa Francisko amesalimia waamni na mahijaji wote mara baada ya katekesi yake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari ya katekesi yake Papa Francisko kwa waamini na mahujaji waliofika mjini Vatican, amewakaribisha na kuwasalimia watu wote kutoka pande zote za dunia na kwa kila lugha za wawakilishi hao. Katika lugha ya kiitalino, kwa namna ya pekee amesewasalimia watuawa, wa kike na kiume, wawalishi wa Fiaccola Benedettina, wakiwa na Askofu Mkuu wa  Spoleto-Norcia, Askofu Mkuu  Renato Boccardo  na Abate wa  Montecassino, Abate Donato Ogliari.

Aidha vijana, wazee, wagonjwa, wanandoa wapya, akiwashauri kumwamini Bwana na kujaribu kuingia kwa kina katika ishara zake na kukubali wokovu wake ambao unaweza kuwafikia katika njia tofauti na zile ambazo walikuwa wanatarajia. Kwa lugha ya kingereza, amewasalimia waamini kutoka Uingereza, Norway, Ufilippini, Saud Arabia, Vietnam na Marekani.  Juu yao anawabariki familia zao na kuwatakia wawe na furaha na amani ya Bwana Yesu Kristo.

 

19 February 2020, 12:54