Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, Jumapili tarehe 16 Februari 2020, Papa Francisko amewasalimia wote kwa namna ya pekee mahujaji kutoka Krotia na Serbia; Trappes, Ufaransa; Jimbo la Toledo, nchini Hispania; wanafunzi kutoka Taasisi ya Cuestablanca, jijini Madrid.
Aidha amesalimia waamini wa Biancavilla, Fiuggi, Aprilia, Pescara na Treviso; Vijana waliopata kipaimara wa Serravalle Scrivia, Quarto ya Altino na Rosolina. Kwa wote amewatakia Dominka njema na kuwaomba kama kawaida yake ili kusali kwa ajili yake.