Katekesi ya Papa tarehe 5 Februari 2020 mwendelezo wa heri za mlimani: heri maskini wa roho maana ufalme wa mbingu ni wao Katekesi ya Papa tarehe 5 Februari 2020 mwendelezo wa heri za mlimani: heri maskini wa roho maana ufalme wa mbingu ni wao 

Papa Francisko: mwenye kiburi hawezi kuomba msamaha si maskini ra roho!

Katika mwendelezo wa Katekesi kuhusu Heri za Mlimani Papa Francisko,hata tarehe 5 Februari kwa mahujaji na waamini amejikita juu ya Heri ya kwanza.Ni kwa njia ya kujitambua udhaifu binafsi tu,unaweza kupenda kweli kwa namna huru na kutoa maisha kwa ajili ya wengine.Ni muhimu kutambua kuwa hata kama utajaribu kufanya vipi daima mtu hajikamilishi ni mdhaifu.Hakuna ujanja ambao unafunika udhaifu huu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wapendwa ndugu kaka na dada habarini za Asubuhi! Leo tukabiliana na moja ya Heri Nane za Injili ya Matayo. Yesu alianza kutangaza njia yake ya furaha kwa kutangaza mfananisho wa “Heri maskini wa Roho, kwa maana ufalme wa mbingu ni wao”( Mt 5,3). Barabara ya kushangaza, na kitu cha kushangaza cha heri na umaskini. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI mjini  Vatican tarehe 5 Februari 2020. Papa Francisko kama alivyokuwa amehidi katika katekesi iliyopita ameanza kufafanua heri ya kwanza  na kusema tunapaswa kujiuliza hapa:nini maana ya umaskini? Kama Matayo angeweza kutumua neno hili peke yake, ingekuwa na maana rahisi tu ya kiuchumi, yaani ingekuwa inamaanisha mtu aliye na kidogo au hasiye kuwa na zana yoyote ya kumsaidia na ulazima wa msaada kutoka kwa wengine.

Injili ya Matayo inazungumza umaskini kiroho

Injili ya Matayo tofauti na Luka inazungumza juu ya umaskini wa kiroho anasema Papa. Je ni kusema nini? Roho kwa mujibu wa Biblia ni pumzi ya maisha ambayo Mungu anawasiliana na Adamu; ni ukuu wetu zaidi wa kiundani, tusema ukuu wa kiroho ambao unatufanya kuwa wanadamu, yaani msingi wa ndani wa mwili wetu. Kufuatana na hiyo, “maskini katika roho” ni wale ambao ni, na  wanahisi kuwa maskini, waomba omba, udhati wa kina wa kuwapo kwao. Anafafanua Papa. Yesu anawatangazia kuwa ni wenye Heri kwa sababu Ufalme wa mbinguni ni wao. Ni mara ngapi wamekuwa wakisema hili kinyume! Ni lazima kuwa kitu fulani katika maisha, kuwa mtu… ni lazima kuwa na jina… Na kwa suala hili ndipo kunatokana na upweke na ukosefu wa furaha. Kwa mfano, ikiwa mimi ninataka kuwa mtu, ninaanza kushindana  na wengine na kuishi na wasiwasi kutokana na ubinafsi wangu. Ikiwa mimi sikubali kuwa maskini, ninaanza kuwa na chuki na kile ambacho kinakumbusha udhaifu wangu. Hii ni kutokana na kwamba udhaifu wangu unanizuia kuwa mtu muhimu, kama vile tajiri na si wa fedha tu, lakini hata kuwa maarufu au  wa yote. Papa Francisko amefafanua.

Sisi sote hatujakamilika maana ni wadhaifu

Papa Francisko akiendelea amebainisha kuwa kila mtu nafsini mwake, anajua vema kwamba hata kama atajaribu kufanya vipi yeye daima huwa hajakamilika na ni mdhaifu. Hakuna ujanja ambao unafunika udhaifu huu. Kila mmoja wetu ni mwathirika wa ndani. Na kwa maana hiyo lazima aone ni wapi.  Akitoa mfano Papa anasema: "Ni kwa jinsi gani unaishi vibaya ikiwa unakataa mipaka yako! Unaishi vibaya. Kikomo hakikichimbwi, ni pale. Watu wenye kiburi hawaombi msaada, hawaombi msaada kwa sababu wanataka kujidhihirisha kuwa wao wanajitosheleza. Watu kama hao wanahitaji msaada lakini kiburi chao kinawazuia kuomba msaada. Jinsi gani ilivyo nguvu kukubali makosa na kuomba msamaha!  amesisitiza.

Kuna maneno matatu muhimu:kuomba ruhusa, asante, samahani 

Papa Francisko ametoa mfano mwingine kwamba yeye anapotoa ushauri kwa wanandoa wapya hasa wanaomwomba ni  namna gani  waweze kupeleka mbele ndoa yao anawambia: “ Kuna maneno matatu muhimu: “kuomba ruhusa, asante, samahani ”. Ni maneno ambayo hutokana na umaskini wa roho. Siyo lazima uingilie kati, lakini omba ruhusa. Je ni vema kufanya hivyo? Anauliza Papa Francisko. Kwa namna hiyo kuna majadiliano ndani ya familia kati ya bi arusi na bwana arusi wanajadiliana.  “Wewe umefanya hivyo kwa ajili yangu, ...asante  nilikuwa na hitaji”. Na ikiwa unateleza katika makosa, daima ni kuomba samahani”. Papa Francisko aidha ametoa mfano mwingine wa  wanandoa wapya kama wale waliokuwapo kuwa,  mara nyingi wanamwambia neno la tatu ni gumu hasa la kuomba msamaha. Lakini hiyo ni kutokana na kiburi, kwa maana mwenye kiburi anasema, hawezi kufanya hivyo. Hawezi kuomba msamaha kwani anaona hajakosea. Huyo si maskini wa roho.

Bwana hachoki kusamehe: ni ugonjwa kukosa kuomba msamaha

Kinyume chake Bwana hachoki kamwe kusamehe; kwa bahati mbaya Papa amebainisha sisi tunachoka kuomba msamaha (Angelus 17 marzo 2013). Uchovu wa kuomba msamaha ni ugonjwa mbaya sana! Ni kwanini inakuwa vigumu kuomba msamaha? Kwa sababu sura zetu za kinafiki zinakosa unyenyekevu. Pamoja na hayo kuishi kwa kujaribu kuficha mapungufu binafsi ni kazi ngumu na ya kuhuzunisha. Yesu Kristo anatuambia: kuwa maskini ni fursa ya neema; na inatuonyesha njia ya kuondokana na  ugumu huo. Tumepewa haki ya kuwa maskini katika roho, kwa sababu hii ndiyo njia ya Ufalme wa Mungu. Lakini kuna jambo moja la msingi  Papa anasema:  hatupaswi kujigeuza ili kuwa maskini katika roho, hatupaswi kufanya mabadiliko yoyote kwa sababu tayari tunayo! Sisi ni masikini ... au kwa uwazi zaidi: sisi ni maskini wa kutisha katika roho! Tunahitaji kila kitu. Sisi sote ni maskini katika roho, tunaomba omba. Ni hali ya mwanadamu.

Ufalme wa Mungu ni wa maskini wa roho

Ufalme wa Mungu ni wa maskini katika Roho. Wapo ambao wanatawala dunia hii. Wenye mali na wanaishi vema. Lakini ni falme ambazo zinaisha. Uwezo wa wanadamu, hata falme kubwa zaidi, hupita na kutoweka. Mara nyingi tunaona kwenye habari au kwenye magazeti kwamba mtawala huyo mwenye nguvu, au serikali hiyo ambaye ilikuwapo jana leo haupo tena  au  ameshuka. Utajiri wa ulimwengu huu umepita, na pesa pia. Wazee walitufundisha kwamba shuka la maziko halina mifuko. Ni kweli. Sijawahi lori la  kubeba maiti linachukua chochote. Hakuna apelekaye chchote. Utajiri huu unabaki hapa. Ufalme wa Mungu ni mali ya maskini katika roho. Kuna wale ambao wana falme za ulimwengu huu, wana bidhaa na wana faraja. Lakini tunajua jinsi zinaisha. Wale wanaojua kupenda mema ya kweli zaidi kuliko wao wenyewe hutawala ni kwa kweli. Na hiyo ni nguvu ya Mungu. Papa amesisitiza tena.

Yesu alitambua kufanya kile ambacho wafalme wa dunia hii hawafanyi

Ni kitu gani Yesu anajionesha nguvu? Yeye alitambua kufanya kile ambacho wafalme wa ulimwengu huu hawatendi , anasema Papa,  yanii kutoa maisha kwa ajili ya watu. Na huo ndiyo uwezo wake wa kweli. Uwezo wa kidugu, uwezo wa hisani, uwezo wa upendo  na uwezo wa unyenyekevu. Ndicho alifanya Yesu, anasisitiza.  Katika hili ndiyo kuna uhuru wa kweli. Mwenye uwezo wa unyenyekevu, wa huduma, wa udugu  yeye ni huru. Katika huduma ya uhuru huu, ndiyo umaskini unaosifiwa Heri. Kwa sababu kuna umaskini ambao lazima tukubali, huo wa kuwa kwetu, na umaskini ambao lazima tuutafute, ule wa kweli, dhidi ya   vitu vya ulimwengu huu, ili kuweza kuwa huru na kuweza kupenda! Lazima kila wakati tutafute uhuru wa moyo, ambao una mizizi yake katika umaskini wetu sisi binafsi. Amehitimisha Papa Francisko

05 February 2020, 13:02