Papa Francisko kwa mara nyingine tena ameonesha mshikamano wake wa dhati na waathirika wa virusi vya Corona, COVID-19. Papa Francisko kwa mara nyingine tena ameonesha mshikamano wake wa dhati na waathirika wa virusi vya Corona, COVID-19. 

Mshikamno wa Papa Francisko na waathirika wa Virusi vya Corona!

Ugonjwa wa Virusi vya Corona: Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru wahudumu katika sekta ya afya wanaoendelea kuwatibu na kuwaganga wagonjwa, viongozi wa Serikali na watu wote ambao wamekuwa mstari wa mbele ili kuhakikisha kwamba maambuzi ya ugonjwa wa unaosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19 yanadhibitwa, ili kurejesha amani, utulivu, ustawi na maendeleo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

 

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake, Jumatano ya Majivu, tarehe 26 Februari 2020, ameyaelekeza mawazo yake kwa kuonesha uwepo wake wa karibu kwa wagonjwa na waathirika wa virusi vya Corona, COVID-19. Baba Mtakatifu amewashukuru wahudumu katika sekta ya afya wanaoendelea kuwatibu na kuwaganga wagonjwa, viongozi wa Serikali na watu wote ambao wamekuwa mstari wa mbele ili kuhakikisha kwamba maambuzi ya ugonjwa wa unaosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19 yanadhibitwa, ili kurejesha amani na utulivu.

Hofu kubwa imetanda sehemu mbali mbali za dunia kutokana na kusambaa kwa kasi kwa virusi hivi. Wakati huo huo, Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kuwa hofu yake kubwa zaidi hivi sasa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, COVID-19 kuingia katika mataifa yenye mifumo dhaifu ya afya hususan Barani Afrika.

Papa: Crono Virus

 

 

26 February 2020, 14:37