Tafuta

Vatican News
Maparokia na jumuiya tofauti za Kanisa zinaalikwa kukuza jitihada zaidi kwa ajili ya vijana,familia na wazee. Maparokia na jumuiya tofauti za Kanisa zinaalikwa kukuza jitihada zaidi kwa ajili ya vijana,familia na wazee. 

Papa Francisko:mkristo yuko daima safarini kutangaza Yesu!

Papa Francisko katika Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni anakumbusha kuwa dunia inahitaji wakristo ambao wanatembea katika njia za maisha wakipeleka neno la Yesu.Maparokia na jumuiya tofauti za Kanisa zinaalikwa kukuza jitihada zaidi kwa vijana,familia na wazee.Sambamba na Siku ya Watawa dunia,wazo lake ni juu ya kazi nyingi wanazofanya mara nyingi watawa wakiwa wamejificha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumapili tarehe 2 Februari 2020 kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Papa ameanza tafakari kwa kusema: Leo tunaadhimisha Siku Kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni. Kwani Yesu akiwa mdogo alipelkea hekaluni na Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu. Siku hii pia ni maadhimisho ya Siku ya watawa ambayo inataka kukumbusha juu ya thamani katika Kanisa ambao wanamfuasa Bwana kwa karibu kwa kufunga nadhiri za kiinjili.

Maria, Yosefu, Simeoni na Anna ni mifano ya mtindo wa ukarimu

Injili ya Lk 2,22-40) inasimulia kwamba siku arobaini baada ya kuzaliwa kwa Yesu, walimpeleka mtoto huko Yerusalemu kwa ajili ya kumweka wakfu kwa Mungu kama ilivyokuwa  sheria ya kiyahudi. Papa anabainisha katika kufafanua  ibada  kiutamaduni,  tukio hili linajikita ndani mwetu kuwa na  umakini kwa ajili ya kuona mifano ya baadhi ya watu. Hawa wanaonekana  katika uzoefu wao wa kukutana na Bwana, mahali ambamo Yeye  yumo na kuwa karibu na binadamu. Watu hawa ni Maria, Yosefu, Simeoni na Anna ambao wanawakilisha mtindo wa ukarimu  na kujitoa maisha kwa Mungu. Watu hawa wanne hawakufanana , walikuwa ni tofauti lakini wote walikuwa wanamtafuta Mungu na waliacha waongozwe na Bwana, Papa anathibitisha. Mwinjili Luka anawafafanua wote wanne katika  tabia mbili, tabia ya kwanza ya mwendo na ya pili ya mashangao

Tabia ya kuwa katika mwendo

Papa Francisko akianza kufafanua tabia ya kwanza ya mwendo anasema: “ Maria na Yosefu walikuwa wanatembele kuelekea Yerusalemu; kwa upande wa Simeoni, yeye aliongozwa na Roho na kuelekea katika hekalu na wakati Anna yumo Hekaluni anahudumia Mungu usiku na mchana bila kuchoka. Katika mtindo wa watu hawa wanne kwenye  Injili tunaona kuwa maisha ya kikristo yanahitaji kuwa katika mwendo na kututaka tuwe na uwajibikaji, ulazima  wa kutembea na kuacha kuongozwa na Roho Mtakatifu.  Kusimama siyo ishara ya kuonyesha ushuhuda wa kikristo na katika utume wa Kanisa. Dunia inahitaji wakristo ambao wanajiachia katika mwendo na wala hawachoki kutembea katika njia za maisha huku wakitafuta wote kuwafariji kwa Neno la Yesu.

Maparokia yote na jumuiya tofauti za Kanisa zinaalikwa kukuza jitihada za vijana, falimilia na wazee

Kila mbatizwa alipokea wito wa kutangaza jambo, kutangaza Yesu, wito katika utume wa uinjilishaji. Kwa maana ya kutangaza Yesu ! Maparokia yote na jumuiya tofauti za Kanisa zinaalikwa kukuza jitihada za vijana, falimilia na wazee ili hatimaye kuweza kufanya uzoefu wa kikristo na kuishi mstari wa mbele wa maisha na utume wa Kanisa.

Tabia ya pili ni kuwa na mshangao

Tabia ya pili ambayo Mtakatifu Luka anawakilisha kwa watu hawa wanne kwenye simulizi ya Injili ni mshangao. Maria na Yosefu walikuwa wakishangaa mambo hayo yote yaliyokuwa yanasemwa juu mtoto Yesu (Lk 2,  33). Mshangao ni hali inayo jionesha hata kwa mzee Simeoni ambaye katika Mtoto Yesu alimwona kwa macho yake ule wokovu uliotendwa na Mungu kwa ajili ya watu wake. Wokovu ambao alikuwa anausubiri kwa miaka mingi. Vile vile ndiyo mshangao wa Anna ambaye alianza kusifu Mungu (Lk 2,38) na kwenda kuwaonyesha watu Yesu, Papa Francisko ameongeza kusema: “huyo ndiye mtakatifu aliyekuwa na maneno mengi, lakini alikuwa anaongea mambo mazuri na siyo mabaya. Alikuwa anatangaza. Yeye alikuwa anakwenda kwa mwanamke mmoja baada ya mwingine akiwafanya watazame Yesu.

Sura za waamini kama hawa zinashangaza

Sura hizi za waamini wakati mwingine zinashangaza anasema Papa, kwa sababu zinaacha zivutiwe kwa haraka na kujihusisha na matukio ambayo yalikuwa yanatokea machoni pao. Huo ndiyo uwezo wa kushangaa mambo ambayo yanatuzunguka na kukuza uzoefu wa kidini ambao unakuwa mwafaka katika kukutana na Bwana. Kinyume na hiyo ukosefu wa mshangao unatufanya kuwa na sintofahamu na kuweka umbali sana kati ya kutembea kwa imani na maisha ya kila siku. Papa Francisko anawaalika waamini wawe katika mwendo daima  hasa kwa kujifungulia mshangao. Bikira Maria atusaidie kutafakari kila siku katika Yesu ile zawadi ya Mungu kwa ajili yetu na kujiachia kuvutiwa na Yeye katika mwendo wa zawadi, kwa furaha ya mshangao ili maisha yetu yote yageuke kuwa sifa kwa Mungu katika huduma ya ndugu.

03 February 2020, 09:30