Tafuta

Papa amekumbusha Siku ya Watawa duniani na kuomba wasali kwa ajili ya watawa wote na kwamba wanafanya kazi kubwa na mara nyingi wakiwa wamejificha Papa amekumbusha Siku ya Watawa duniani na kuomba wasali kwa ajili ya watawa wote na kwamba wanafanya kazi kubwa na mara nyingi wakiwa wamejificha 

Papa Francisko:hakuna kukiuka hadhi ya maisha!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko ameungana na Maaskofu wa Italia katika Siku ya Maisha inayoongozwa na mada“fungueni milango kwa ajili ya maisha” na kuomba jitihada za kulinda na kutetea maisha ya binadamu tangu kutungwa kwake hadi mwisho.Pia amekumbusha Siku ya Watawa duniani na kuomba wasali kwa ajili ya watawa wote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 2 Febrauri 2020, Papa Francisko amesema: "Leo nchini Italia wanaadhimisha Siku ya Maisha ambayo inaongozwa na mada “Fungulieni milango maisha”. "Ninaungana na Ujumbe wa Maaskofu nikiwatakia siku hii iwe fursa ya kupyaisha jitihada za kulinda na kutetea maisha ya binadamu tangu kutungwa kwake hadi mwisho wake wa asili". Aidha Papa ameongeza kusema: "Ni lazima kupingana na kila mtindo wa ukiukwaji wa hadhi hata panapoingia ule mchezo wa kiteknolojia au kiuchumi, na badala yake kufungua milango mipya ya mitindo ya mshikamano kidugu".

Siku ya Watawa duniani

Akiendelea, Papa Francisko pia amesema "leo ni siku ya Watawa duniani" kwa maana hiyo ameomba watu wote katika uwanja huo wasali kwa ajili ya watawa wote kike na kiume ambao amebainisha kuwa wanafanya kazi nyingi sana na mara nyingi zilizo fikichika. Kwa wote wamesali salam Maria pia kuwapigia makofi watawa wote kike na kiume. Salam pia kwa mahujaji wote kutoka pande zote za dunia na hatimaye kuwatakia Jumapili njema na mlo mwema lakini pia wasisahau kusali kwa ajili yake.

Ujumbe wa maaskofu wa Italia :hakuna kutoa mimba, kubagua na manyanyaso

Katika Ujumbe wa Maaskofu nchini italia, katika  fursa ya Siku ya 42 ya Ulinzi na utetezi wa maisha inasisitiza juu ya kupinga kila mtindo wa utoaji mimba, ubaguzi na manyanyaso. Ni mwaliko wa maaskofu kwa wote katika kuhamasisha usawa wa hadhi ya kila mtu. Katika Ujumbe huo umetiwa sahihi na Baraza la Kudumu la Maaskofu ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza inajikita juu ya hali za  shauku ya maisha yasiyo na maana, pili inaelezea juu ya utambuzi wa kutunza na tatu inajikita katika kufafanua maana ya ukarimu wa kupokea hata kile kisichotarajiwa.

03 February 2020, 09:42