Tafuta

Vatican News
Tarehe 15 Januari 2020 Papa Francisko amezindua mwaka wa 91 wa Mahakama ya mji wa Vatican Tarehe 15 Januari 2020 Papa Francisko amezindua mwaka wa 91 wa Mahakama ya mji wa Vatican   (Vatican Media)

Papa Francesco:Fuateni njia ya haki na taadhari ya nafsi zenu!

Papa Francisko,Jumamosi,tarehe 15 Februari 2020 amezindua Mwaka wa 91 wa Mahakama ya Rufaa ya Kipapa,akikazia juu ya haki na kuwawezesha udugu kwa wote hasa kulinda walio wadhaifu zaidi.Ushauri wa Papa ni kuwa macho kwa ajili ya nafsi zao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Kwa  kufuata na kuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa njia ya haki, kama njia ambayo inatoa  uwezekano wa udugu halisi na ambao kila mtu analindwa, hasa walio dhaifu zaidi, ndiyo umekuwa mwaliko wa Papa Francisko,alioutoa wakati wa kuzindua mwaka wa 91 wa Mahakama ya Rufaa ya Kipapa Vatican, mbele ya wahamasishaji wa Haki, wachunguzi, maafisa, wanasheria na wahudumu wa Mahakama, Jumamosi tarehe 15 Februari 2020.

Papa amesema, “Ninajua kuwa wengi wenu mnajihusisha na taasisi zinazosimamia usimamizi wa haki na ulinzi wa utaratibu wa umma”, ameanza hivyo Papa  Francesco, mara  baada ya salamu kutoka kwa Mhamasishaji wa haki, Bwana Gian Piero Milano: “Hasa kwa sababu hii kazi yenu inachukua dhamana yenye thamani, kwa sababu ni dhamana  na siyo tu ya utaratibu, lakini zaidi ya jukumu katika ubora wa uhusiano wa kibinadamu uliofanywa uzoezo katika maeneo yenu”.Tendo la kwanza lililoonyeshwa na Papa Francisko kwa washiriki wa afla hii katika hotuba yake ilikuwa ni Injili, ambayo amesema “inatufundisha mtazamo wa kina kuliko mawazo ya kidunia  na inatuonyesha kuwa haki inayopendekezwa na Yesu siyo seti rahisi ya sheria zilizotumika kiufundi, lakini ni mpangilio wa moyo ambao unaongoza mwenye kuwa na  jukumu”.

Akiendelea na ufafanuzi ni ushauri wake  mkubwa wa Injili ni “kuanzisha haki kwanza ndani mwetu, huku  tukijitahidi sana kupamba na magugu ambayo yanaishi ndani mwake”,na kukumbusha kuwa “ Ni vizuri kufikiria kuwa Yesu anaweza kuondoa mzizi wowote wa uovu ndani mwetu bila kuharibu hata ngano nzuri. Vile vile anasema,  “Lakini kuwa macho dhidi ya mapambano ya ndani yanatusaidia tusiangukie ndani ya mego wa ubaya na kuacha mema. Mbele ya kukabiliwa na hali hii, hakuna mfumo wa kisheria unaoweza kutuokoa”: Kwa maana hiyo Papa anatoa onyo na kuwaalikwa kila mmoja aliyekuwapo onyo la Papa, ambaye alimwalika kila mmoja aliyekuwepo “kuhisi kuhusika na siyo tu katika ahadi ya jitihada ya ya nje inayojali wengine, bali pia katika kazi binafi ya ndani ya kila mmoja wetu yaani kubadilika kwetu binafsi katika uongofu. Ni kwa njia hiyo tu haki inaweza kutoa haki nyingine” Papa amesisitiza. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mwaka wa 91 wa Mahakama ya Kitume Vatican  Papa amesema  “Haki peke yake haitoshi, inahitaji kuandamana na fadhila nyingine pia, hasa zile msingi yaani busara, ujasiri na utulivu. “Busara utupatia uwezo wa kutofautisha ukweli na uwongo na unaruhusu kuutumia kwa kila mmoja kadiri ya matumizi yake”.

Tabia ni kama nyenzo ya kusawazisha na usawa katika tathmini ya ukweli na hali inatufanya tuwe huru wa kuamua kwa kuzingatia dhamiri zetu. Uvumilivi ni kama ngome inayoturuhusu kushinda shida tunazokutana nazo na kupinga shinikizo na tamaa. Kwa upande wao, amaesema,  inaweza kuwasaidia katika wakati wa  upweke ambao mara nyingi unawapata katika kufanya maamuzi magumu na nyeti. Papa anawahimiza wasisahu kwamba katika jitihada  zao za  kila siku mara nyingi hujikuta wanakabiliwa na watu ambao wana njaa na kiu ya haki, watu wanaoteseka, wakati mwingine wanakabiliwa na uchungu na tamaa za maisha. Kufuatana na hiyo  Papa Francisko ametoa wito:  “Wakati wa kuhukumu ni lazima muwe ninyi, kwa kuchimba katika ugumu wa mambo ya wanadamu, kutoa majibu sahihi, kwa kuunganisha usahihi wa sheria hizo na huruma nyingi tulizo fundishwa na Yesu. Huruma  kiukweli kwa upande wa   Papa “ siyo  kusimamishwa kwa haki, bali ni  kutimiza kwake, kwa sababu inarudisha kila kitu katika utaratibu uli wa juu zaidi ya yote ambapo hata wale wanaohukumiwa adhabu kali wanapata ukombozi wa matumaini”.

Ni kazi, hiyo ya kuhukumu, ambayo inahitaji  siyo  kujiandaa na usawa tu , bali pia shauku ya haki na ufahamu wa majukumu makubwa na umuhimu unaohusiana na  jukumu la  hukumu”. Papa anasema kwamba kazi yao  haiwezi kupuuza jitihaza za  mara kwa mara katika kuelewa sababu ya makosa na udhaifu wa wale waliokiuka sheria.

15 February 2020, 16:17