Papa amezindua “Super Nuns” kusaidia watawa dhidi ya biashara ya utumwa!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Kwa bofya la kwanza, Papa Francisko amezindua jukwaa hili la “Super Nuns”, ambalo ni jukwaa la Patreon lililobuniwa kwa ajili ya kukusanya fedha kwa ajili ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu na kufadhili miradi ya utunzaji na msaada kwa upande wa watawa wote wanaojikita na shughuli hii ya kusaidia waathirika.
Mradi uliozinduliwa na Talitha Kum ambao ni Mtandao wa Kimataifa wa Kitawa unajikita katika kujenga maisha ya watu, wakati huo wakiwalinda dhidi ya wanafanya biashara haramu na uliofadhiliwa na Mfuko wa chama cha Galileo ambao hutoa ushirikiano kwa wadau mbali mbali kutoka kwa wasanii tofauti wa michoro ya barababarni mmojawapo akiwa ni Stephen Power, wa Amerika kwa usanii wake wa ESPO. Huyu ni msanii wa kuchora michoro mbali mbali mikubwa barabarani, na Leiji Matsumoto, maarufu wa michoro wa Kijapani.
Mara kadhaa Papa amewasha na kutazama juu ya janga hili la biashara ya watu na kuomba viwepo vitendo halisi. Katika tukio hili Papa amesalimiana na kila mtu binafsi na na Sr. Gabriella Bottani, mratibu wa kimataifa wa Talitha Kum, ambaye ameeleza juu ya kuanzishwa wa tovuti hii . Msanii Stephen Power alimemwomba Papa atie sahihi yake katika nakala ya picha ya kwanza na moja amepewa Papa Francisko mwenyewe.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watawa wengine wa Talitha Kum, walioanzisha kwa mpango wa Jumuiya ya Kimataifa ya wa Mama Wakuu wa mashirika ya Kitawa (UISG) na kwa miaka 10 pia amekuwa wakikuza ushirikiano na kubadilishana habari kati ya wanawake na wanaume waliowekwa wakfu katika nchi 70 ulimwengu ili kuweza kupambana na kuondoa kabisa janga la utumwa.