Tafuta

Vatican News
Ufunguzi wa Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Jose, huko Costa Rica kufuatia na maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Kanisa nchini humo Ufunguzi wa Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Jose, huko Costa Rica kufuatia na maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Kanisa nchini humo 

Papa ametuma ujumbe kwa Mwaka wa Jubilei huko Costa Rica!

Katika fursa ya Mwaka kwa ajili ya Jubilei ya miaka 100 ya Kanisa la Costa Rica,kuanzia tarehe 16 Februari 2020 hadi tarehe 16 Februari 2021,Papa Francisko ametuma barua yake akiwashauri kuinjilisha bila kuchoka.Katika Kanisa kuu tatu za Costa Rica waamini wataweza kupokea rehema ya msamaha wa dhambi.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko anaungana kiroho  na watu wa Mungu wakati wa kufungua mwaka wa Jibileonchini Costa Rica kwenye barua iliyotiwa sahihi na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, kunako tarehe 16 Februari 2020, katika fursa ya uzinduzi wa Miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Costa Rica. Katika ujumbe wake Papa anaungana nao kiroho kwa  shukrani  kwa Bwana kwa matunda yote yaliyopatika kwa  kipindi cha miaka 100  ya utume wake kwa  kusindikiza, kuangaza na kuwatia moyo watoto wote (kike na kiume) wa Taifa hilo.

Katika barua hiyo Papa Francisko anawatia moyo ili kuzingatia wakati uliopo  katika siku ambayo wanaanza maadhimisho ya Mwaka wa Jubilei ili kuweza kufanya kumbu kumbu ya matukio muhimu namna hiyo, upendo wa huruma ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambamo panabubujika kila ukweli, wema na uzuri, ili walei  na watawa waweze kuendelea bila kuchoka katika shughuli zao za uinjilishaji, kwa kuwapelekea wote furaha ya Injili, kwa namna ya pekee wale wahitaji na walio mbali zadi aidha waweze kuonesha ushuhuda wa kweli wa maisha ya kikristo katika mazingira mbalimbali ya kijamii.  Barua ya Papa Francisko inahitimishwa kwa kuomba ulinzi wa Mama Yesu Maria wa Malkia wa malaika ambaye ni msimamizi  wa Costa Rica. Papa Francisko anawatumia Baraka ya kitume ili iwashukuie washiriki wote wa Maadhimisho makuu.

Mwaka wa Jubilei umekubaliwa hata kuwa na  Msamaha wa kitume kutoka Vatican kuanzia tarehe 16 Februari 2020 hadi tarehe 16 Februari 2021, na kukumbusha kuwekwa msingi wa Kanisa la Costa Rica kwa upande wa Papa Benedikto XV kwa Hati ya  “Praedecessorum” ya Mwaka 1921, ambapo ilikwekwa Jimbo la Mtakatifu José  ambalo ni makao makuu ya mji na ambayo iliunda majimbo mengine ya Limón na  Alajuela.  Kanisa Kuu na majimbo mengine yatakuwa ndiyo maeneo ya kufanya hija na waamini na ambapo wanaweza kupata neema ya kiroho na rehema ya msamaha wa dhambi (Indulgentia plenaria).

Tume ya maaskofu iliyoundwa kwa ajili ya maadhimisho ya Jubilei, imeandaa maadhimisho katika sehemu kuu tatu. Ya kwanza imedhimisha tarehe 13 Februari 2020 kwa maadhimishao ya Ekaristi katika Kanisa kuu la Limón.  Jimbo la Limo kihistoria linajulikana sana kama ndimo waliadhimisha Misa ya kwanza kunako mwaka 1502, wakati wa toleo la 4 la sasfari ya Cristoforo Colombo ilipokanyaga mguu katika ardhi ya Costa Rica.

Vipindi viwili vingine muhimu vitafanyika tarehe 19 Julai kwa kufanya mkutano wa Kitaifa katika jimbo Kuu la Mtakatifu José, wakati kunako Februari 2021 wakifunga  mwaka wa Jubilei, watafanya Kongamano la Ekaristi kitaifa katika Jimbo la Alajuela. Jumapili  tarehe 16 Februari 2020, wamefungua milango mitakatifu katika Makanisa Makuu  matatu ambayo yatakuwa ni makao makuu ya matukio ya Kikanisa kitaifa kwa ajili ya mwaka mzima maadhimisho ya Jubilei hiyo.

18 February 2020, 11:24