Tafuta

Papa ametoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa na wadau wote wanahusika na vikosi vya kijeshi nchini Siria kusitisha mapambano kwa ajili ya usalama wa watu wasio na hatia Papa ametoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa na wadau wote wanahusika na vikosi vya kijeshi nchini Siria kusitisha mapambano kwa ajili ya usalama wa watu wasio na hatia 

Masikitiko ya Papa na uchungu nchini Siria:inahitajika majadiliano na diplomasia!

Wito kwa Jumuiya ya kimataifa na wadau wote wanahusika na vikosi vya kijeshi nchini Siria ili kusitisha janga hil la kivita,ndiyo wito uliotolewa na Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 9 Februari 2020.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa  Bwana kwa mahujaji na waamni waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican Jumapili tarehe 9 Februari 2020 amesema: “Jana  katika liturujia ilikuwa ni siku ya Mtakatifu  Giuseppina Bakhita, na wameadhimisha siku ya dunia ya Sala na tafakaridhi dhidi ya biashara ya watu. Katika kuponesha janga hili kwa maana ni kidonda cha kweli, ambacho kinanyonya walio wa dhaifu, ni lazima zipatikane jitihada za wote kuanzia hali halisi, vyama na taasisi za elimu.

Papa Francisko akiendelea juu ya janga hili amesema: “Katika upande wa kuzuia, ningependa kusema jinsi tafiti mbalimbali zinavyoonyesha kuwa mashirika ya uhalifu wa jinai yanazidi kutumia njia za kisasa za mawasiliano ili kushawishi waathiriwa na udanganyifu. Kwa hiyo, inahitajika kwa upande mmoja kuelimisha juu ya utumiaji mzuri wa njia za kiteknolojia, kwa upande mwingine kusimamia na kuonya juu ya  wauzaji wa huduma hizi za simu kwa sababu ya  majukumu yao”.

Kuhusiana na vita nchini Siria

Papa Francisko amebainisha juu ya  habari zenye maumivu zinavyo endelea kufika kutoka kaskazini-magharibi mwa Siria, hasa kwa hali ya wanawake na watoto, ya watu waliolazimishwa kukimbia kutokana na kuongezeka kwa wanajeshi. “Ninasasisha wito wangu kutoka moyoni kwa Jumuiya ya kimataifa na kwa wadau wote wanohusika ili kutumia vyombo vya kidiplomasia, majadiliano na mazungumzo, kwa kufuata Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu, ili kulinda maisha na hatima ya raia”. Kwa njia hiyo Papa Francisko ameomba waamini na mahujaji wote waliokusanyika kuomba kwa ajili ya nchi hii pendwa Siria  inayosumbuliwa. " Salam Maria..."

10 February 2020, 09:40