Papa Francisko akiwa na washiriki wa Jukwaa lwa Mkati wa elimu duniani ulioandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Sayanis Kijamii kuanzia tarehe 6-7 Februari 2020 mjini Vatican Papa Francisko akiwa na washiriki wa Jukwaa lwa Mkati wa elimu duniani ulioandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Sayanis Kijamii kuanzia tarehe 6-7 Februari 2020 mjini Vatican 

Francisko:kwa kufikiria elimu ni kufikiria wakati endelevu

Elimu ni moja ya changamoto msingi ambazo zinatazama jamii ya sasa.Papa Francisko anakumbusha hayo wakati wa kukutana na washiriki wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Sayanis Jamii katika matazamio ya tukio la kidunia kuhusu “Mpango mkakati wa Elimu duniani” mkutano utakatofanyika kunako tarehe 14 Mei 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 7 Februari amezungumza na washiriki wa semina kuhusu: “Elimu:mpango mkakati ulimwenguni”. Semina hii imeandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya  Sayansi jamii katika matazamio ya tukio la kidunia kuhusu  Mkutano wa “Mpango mkakati wa Elimu dunaini ” mkutano utakatofanyika kunako tarehe 14 Mei 2020. Lengo la Mkutano huo likiwa ni kuwasaidia vijana kuwa na mwamko wa kujikita katika elimu fungamanishi inayowataka vijana wote kuwa wasikivu, wajenzi wa haki, amani, umoja na udugu wa kibinadamu katika usawa. Katika hotuba ya Papa Francisko anaonesha  furaha yake kuzungumza juu ya mada hiyo kwa sababu “leo  hii ni lazima kuunganisha jitihada ili kufikia mshikamano wa elimu iliyo pana na hatimaye kuunda mtu aliyekomaa, na mwenye uwezo wa kujenga uhusiano na kuunda ubinadamu wa kidugu Zaidi”. (rej hotuba kwa wanadiplomasia, 9 Januari 2020)

Elimu yenye viwango inazidi kuwa na changamoto

Elimu fungamani na bora na yenye viwango vya elimu vinaendelea kuwa changamoto ulimwenguni. Licha ya malengo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine na jitihada muhimu zilizotimizwa kwa baadhi ya nchi, elimu inaendelea kukosa usawa kati ya watu duniani. Umasikini, uhalifu, mabadiliko ya tabia nchi, utandawazi wa sintofahamu, uumbaji wa mwanadamu hufanya maua ya mamilioni ya viumbe kukauka anasisitiza Papa. Matukio ya kweli yanaonesha kwa walio wengi kuta ambazo ni vigumu kuzipita na kuzuia kufikia malengo ya maendeleo endelevu na uhakika ambao watu wanaweza kupendekeza.

Elimu ya msingi leo hii ni wazo la kawadia duniani kote

Takwimu  ambazo kama wasomi wanashirikishana zinaoneshwa maendeleo ambayo yamekuwapo kwa ushiriki wa watoto wa kike na kiume. Orodha ya kujiandikisha kwa vijana katika elimu msingi leo hii duniani lakini inaonesha mapengo na kupunga.  Hayo ni matokeo yasiyoweza kusahulika a, anasema papa. Kizazi kipanapaswa kifikirie kwa namba gani  kinaweza kurithisha wenzake ile thamani kwa wale wanaofuata, kwa sababu ni kwa njia ya  ya elimu tu ambayo inamkamilisha mwanadamu na uwezo wake na kuwa na utambuzi na uwajibikaji. Kufikiria elimu ni kufikiria kizazi endelevu na bubinadamu endelevu; na zadi kile cha kina ambachao kina mzizi katika matumaini na kutaka ukarimu na ujasiri. Kuelimisha siyo tu kuonesha mantiki bali ni zoezi linalohitaji wote  ambao wanajukumu, kama vile familia, shule na taasisi za kijamii, kitumaduni na kidini, wanashiriki kwa namna ya mshikamano. Katika kuelimisha inahitaji kufungamanisha lugha ya akili, lugha ya moyo na ya mikono. Hiyo ndiyo isaidie mwanafunzi kufikiria anachohisi na kutenda kile anacho sikia na kusikia anachokiri. Kuhamasisha  elimu  kutoka kichwani, moyoni na katika mikono, elimu ya kiakili na hisia-jamii, kurithisha thamani na fadhila za kila mtu kwa haki na kuanzia na uwezo na utambuzi unaounda kijana kwa ajili ya dunia ya kazi na jamii, familia , shule na taasisi zinageuka kuwa injini muhimu kwa ajili ya kukuza kizazi kijacho.

Kuna kipeo na uhusiano wa familia na shule kuvunjika

Leo hii kuna kipeo na kumevunjika kile kiitwacho mkakati elimu; mkakati  elimu ambao unaundwa  uhusiano kati ya familia, shule, nchi mahalia na dunia, utamaduni na tamaduni. Kwa hakika  vyote vimevunjika; haiwezekani vigundisha au kuunganisha iwapo si kwa njia ya kupyaisha juhudi za  ukarimu  wa mikataba  ya ulimwengu, anasisitiza Papa. Mkataba wa elimu uliovunjika unamaanisha kuwa jamii zote mbili, familia, na taasisi tofauti ambazo zinaitwa kutoa elimu ya kukabidhi kazi hiyo ya maamuzi kwa wengine, na kwa hivyo tofauti za  taasisi za msingi na nchi zenyewe  ambazo zimekataa  mpango mkakati wa kielimu kutoroka wajibu huo. Leo hii tumeitwa, kwa njia fulani, Papa amesema, kupyaisha na kufungamanisha kwa kila mtu,  watu na taasisi katika elimu, ili kuunda  kwa mpango mkakati mpya wa elimu, kwa sababu ni kwa njia hii tu, elimu inaweza kubadilika. Kwa namna hiyo  maarifa, utamaduni, michezo, sayansi, furaha na burudani lazima vifunganishwe; kwa sababu hiyo inahitaji kujenga daraja za kuunganishwa, ili kuondokana na udhaifu ambao hutuingiza kwenye ulimwengu wetu mdogo, na kwenda kwenye bahari ya wazi ya ulimwengu, kwa kuheshimu mila zote.

Kukubali utofauti na mabadiliko ya kitamaduni

Vizazi vipya lazima vielewe wazi mila na tamaduni zao, katika  uhusiano na wengine, ili kukuza uelewa wao, wanaokabiliwa na kukubali utofauti na mabadiliko ya kitamaduni. Hii itakuza utamaduni wa mazungumzo, kukutana na uelewa wa pande zote, kwa njia ya amani, heshima na uvumilivu. Elimu ambayo inatuwezesha kutambua na kuhamasisha maadili ya kweli ya kibinadamu kwa mtazamo wa kiutamaduni na na kidini.  Familia inahitaji kuimarishwa thamani  katika mpango mpya wa kielimu, kwani jukumu lake linaanza tayari tumboni, wakati wa kuzaliwa. Lakini mama, baba,  babu, bibi na familia kwa ujumla, katika jukumu lake la kimsingi la elimu, wanahitaji msaada kuelewa, katika muktadha mpya wa ulimwengu, umuhimu wa hatua hii ya kwanza ya maisha, na kuwa tayari kuchukua hatua ipasavyo.

Walimu ni mafundi wa vizazi vijavyo

Njia moja ya msingi ya kuboresha ubora wa elimu katika kiwango cha shule ni kupata ushiriki mkubwa wa familia na jamuiya mahalia katika miradi ya elimu. Hizi ni sehemu za elimu hii muhimu fungamani  inayofaa kwa wakati na kwa ulimwengu wote. Kwa wakati huu, Papa amependea kutoa heshima kwa waalimu, kwa sababu wanakabiliwa na ujasiri na kujitolea wanapokabiliwa na changamoto ya elimu. Ni mafundi wa vizazi vijavyo. Kwa ufahamu wao, uvumilivu na kujitoa kwao hupitia njia ya kuwa  na ambayo inabadilishwa kuwa mali, siyo mali. Na kubadilisha katika utajiri, si katika zana tu bali katika kuunda mwanaume na mwanamke wa kesho.

Utendaji wa walimu kama wakala wa elimu lazima utambuliwe

Ni uwajibikaji mkubwa. Na kwa maana hiyo mshikamano wa elimu, utendaji wa walimu kama wakala wa elimu lazima utambuliwe na kusaidia na zana iwezekanavyo. Ikiwa lengo letu ni kutoa kwa kila mtu na kwa kila jumuiya ile ngazi ya utambuzi wa lazima ili kuweza kujitosheleza na kuwa na uwezo wa kushirikiana na wengine, ni muhimu kukazia juu ya mafunzo ya walimu kwa kiwango cha hali ya juu, kwa ngazi zote za elimu. Ili kusaidia na kuhamasisha mchakato huo inahitajika kuwa na rasilimali za kutosha za kitaifa, kimataifa na kibinafsi, ili, ulimwenguni kote , waweze kutekeleza kazi yao kwa ufanisi. Katika semina hii kuhusu Elimu: mpango mkakati wa ulimwengu”, Papa anasema wataalam hao na maprofesa wa vyuo vikukuu kutoka duniani wameweze kugundua njia ambayo elimu inaweza kweli kuwa fungamanishi na shirikishi.

Ni muhimu kwa mahitaji ya uchumi wa aina mbambali na jamii za karne ya karne 21

Ni muhimu sana kwa mahitaji ya uchumi wa aina mbambali na jamii za karne ya 21. Kati ya mambo menbine Papa Francisko amesema wamethamanisha juu ya sayansi mpya za akili na elimu , ahadi za kiteknoloja ili kuwafikia watoto wa sasa ambao hawana fursa za mafunzo na mada muhimu sana ya elimu ya vijana wakimbizi na wahamiaji duniani kote. Aidha wamekabiliana na matokeo ya kuongezeka kwa ukosefu wa usawa na mabadiliko ya tabianchi, katika elimu  na kama ilivyo pia zana kwa ajili ya kubadili matokeo hayo yote mawili na uimarishaji wa misingi ya jamii yenye hali nzuri zaidi, yenye afya njema na furaha. Anawatia moyo katika zoezi hili muhimu na shauku waliyo nayo kwa kushirikiana katika elimu kwa ajili ya vizazi vijavyo, siyo jambo la kesho bali la leo hii.

07 February 2020, 13:41