Tafuta

Katika Ujumbe wa Siku  ya Wgonjwa Duninani kwa Mwaka 2020 Papa Francisko anasema wapo  watu masikini na wagonjwa wanaoathirka mifumo kandamizi katika jamii Katika Ujumbe wa Siku ya Wgonjwa Duninani kwa Mwaka 2020 Papa Francisko anasema wapo watu masikini na wagonjwa wanaoathirka mifumo kandamizi katika jamii 

Siku ya wagonjwa duniani:Papa anawakabidhi wagonjwa kwa Bikira Maria!

Katika tweet Papa Francisko anawahakikishia ukaribu wake kwa sala wagonjwa, anafamilia na wahudumu wa afya katika Siku ambayo Kanisa linaadhimisha siku ya 28 ya Wagonjwa Duniani,sambamba na Siku ya kumbukumbu ya Bikira Maria wa Lourdes.Papa anawakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria Afya ya wagonjwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ujumbe wa siku ya XXVIII ya Wagonjwa Duniani 2020 uliolewa tarehe 3 Januari 2020 wakati mama Kanisa anafanya kumbukumbu ya Jina Takatifu la Yesu, umepewa kauli mbiu: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”. Kilele cha Siku hiyo kinaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 11 Februari, sambamba na Sikukuu ya Bikira Maria wa Lourdes. Papa Francisko katika ujumbe wa siku ya wagonjwa duniani amesema kuwa, maneno ya Yesu aliyotamka  kwamba: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”( Mt 11,28) yanaelekeza kwa hakika lile fumbo la safari ya neema ambayo inajionesha kwa watu rahisi na ambao anatoa faraja kwa waliolemewa na kuchoka. Na maneno hayo yanafafanua juu ya mshikamano wa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo mbele ya ubinadamu unaosumbuka na kuteseka. Papa anasema je watu wangapi wanaoteseka katika mwili na roho! Yesu anawaita wote kwenda kwake akisema “njoni kwangu” na anatoa ahadi ya kuwatuliza na faraja. Yesu anaposema hayo , anasema akiwa mbele ya macho yake, anawaona watu anaokutana nao kila siku katika njia za Galilaya. Watu wengi na rahisi, maskini, wagonjwa, wadhambi, waliowekwa pembezoni na kuelemewa na uzito wa sheria na mfumo kandamizi wa kijamii…”Watu hawa walikuwa wanamkimbilia ili kusikiliza neno lake, neno lililokuwa linawapa matumaini (Rej.Malaika wa Bwana 6 luglio 2014). Wapo watu masikini na wagonjwa wanakandamiza na mifumo kandamizi.

Yesu anatoa mwaliko kwa walioelemewa na maskini wanaomtegemea Mungu

Katika Siku ya XXVIII ya Wagonjwa duniani, Papa Francisko amebainisha kuwa, Yesu anatoa mwaliko kwa wagonjwa na waliolemewa, maskini ambao wanatambua kumtegemea Mungu, wakiwa  wamejeruhiwa na uzito wa majaribu, na wanahitaji msaada wa kuponywa. Kwa yule anayeishi kwa uchungu kutokana na hali halisi ya udhaifu na unyong’onyevu,  lakini Yesu hamwekei sheria, bali anatoa huduma yake yaani ya faraja yake. Yesu anatazama ubinadamu uliojeruhiwa. Yeye ana macho ambayo yanaona, yanatambua kwa sababu yanatazama kwa kina na wala hayana utofauti, lakini anasimama na kumkaribisha mtu kamili, kila mtu katika hali yake aliyo nayo bila ubaguzi wa yoyote, huku akimkaribisha kila mmoja aingie katika maisha yake na kufanya uzoefu wa huruma hiyo.

Kwa nini Yesu Kristo anamwilisha hisia hizi?

Papa  Francisko akiendelea na ujumbe wake anauliza swali, Je ni kwa nini Yesu Kristo anamwilisha hisia hizi? Kwa kujibu ni kwamba “Kwa sababu Yeye mwenyewe alijifanya mdhambi, alishiriki uzoefu wa kibinadamu wa kuteseka na baadaye kupata  faraha ya Baba yake. Kwa njia hiyo ina maana ya kusema kiukweli ni kwa yule anayefanya kwanza  uzoefu  binafsi na hatimaye kweli  anaweza kumpati faraja mwingine! Kuna aina mbalimbali za mateso makubwa, Papa Francisko anaeleza, kama vile magonjwa yasiyo na tiba, magojwa sugu, ya asili, kiakili na yale ambayo yanahitaji kusaidiwa kupona taratibu au tiba shufaa na ulemavu tofauti; aidha  magonjwa ya utoto na  yale ya uzee… Katika hali hizo mara nyingi ndipo kuna hatua ya  kugundua vizingiti vya ubinadamu na matokeo yake, kuna ulazima wa kufanya mpangilio kwa ajili ya  mgonjwa hasa kwa kuongezea ile hatua ya kutunnza  ili kuweza kuponyesha ubinadamu fungamani. Katika hali ya ugonjwa mtu uhisi kutotegemea utimilifu wa mwili  wake tu, bali hata ule ukuu wa uhusiano, kiakili, upendo na kiroho; na anasubiri zaidi kwa maana hiyo tiba na msaada, kuhamasishwa na umakini…kwa maana nyingine  ni  ule upendo. Zaidi ya kuwa karibu na mgonjwa vile vile kuna familia ambayo inateseka na ambayo pia inaomba msaada na ukaribu.

Papa Francisko anawageukia wagonjwa kuwa wawe na mtazamo juu ya Yesu

Papa Francisko akiwageukia wagonjwa, anasema ugonjwa unakita  katikati ya wale kwa namna ya pekee walioelemewa na kukandamizwa, ili waweze hasa kuwa na mtazamo na moyo kwa Yesu. Kutoka kwake kuna mwanga hasa katika  kipindi chao kigumu na  cha giza, lakini pia hata matumaini wakati wa  kukata tamaa. Yesu anawalika waende kwake na kusema: “Njoni”. Papa Francisko ameongeza kusema :Kwake yeye kwa hakika anayo majibu y aule  wasiwasi na maswali ambayo katika mwili na roho yanajitokeza wakati wa  usiku ili kuweza kupata nguvu ya kuweza kuyashinda. Ndiyo, anasema Papa Francisko kwamba, Kristo Yesu hakutoa orodha yake, bali yeye alionyesha njia ya mateso, kifo na ufufuko na anatukomboa dhidi ya ukandamizwaji wa ubaya! Katika hali hiyo wagonjwa  kwa  hakika wanahitaji mahali pa kupumzika, anasema Papa Francisko.  Kwa kuonesha njia anasema kwamba “Kanisa linataka kuwa nyumba daima ya kulala ya Msamaria mwema ambaye ni Kristo ( Lk 10,34), ikiwa na maana ya nyumba mahali ambamo wanapata neema yake inayojifafanua katika familia  ya makaribisho na faraja. Katika nyumba hiyo  wagonjwa wanaweza kukutana na mtu ambaye anaweza kuwasaidia kupona kutokana na huduma ya Mungu katika udhaifu wao. Hao wataweza kutambua kuwasaidia  ili kubeba msalaba  wao kwa kuyafanya majeraha yao yawe ya pia ya kwao; kwa njia ya kuona  upeo huo zaidi ya magonjwa na kupokea mwanga na hewa ya maisha yao.

Kazi ya manesi na wauguzi, madaktari na watu wahudumu wa afya

Katika kazi hiyo ya kufarijiwa kwa ndugu manesi, na wauguzi wanajikita katika huduma ya wahudumu wa afya, madaktari, wauguzi na wahudumu wa afya, utawala, wasaidizi, watu wa  kujitolea ambao hushiriki katika kuonesha uwepo wa Kristo anayetoa faraja na kubeba mgonjwa  huku akisafisha majeraha. Lakini hata wao ni wanaume na wanawake ambao pia wana udhaifu wao hata magonjwa yao. Lakini kwa namna ya pekee mara moja wanapokea faraja na nguvu ya Kristo,na kwa maana hiyo Papa Ffarncisko anasema  wote tunaalikwa kwa mara nyingine  kugeuka nguvu na faraja ya ndugu kwa njia ya kuwa na tabia ya kukarimu na unyenyekevu kwa mfano wa kumuiga mwalimu ( Rej Malaika kwa Bwana 6 Julai 2014)

Papa Francisko anatoa onyo dhidi ya eutanasia na kifo laini

Kwa wahudumu wa Afya Papa Francisko anawambia kwamba: “kila tukio la ugunduzi, kuzuia, kutibu, utafiti na kutibu ni tendo linalojikita katika mtu mgonjwa na ambaye ni  binadamu. Yeye  lazima awe ndiyo kiini kabla ya kumwona kama  mgonjwa”. Kwa namna hiyo kazi yao iwe ya kuendeleza utu na mantiki ya hadhi ya  maisha ya mtu ikiwa na lengo la  kuhamasisha hadhi ya binadamu na katika maisha ya mtu bila kuangukia katika vishawishi vya matendo ya kile kinachoitwa eutanasia, kifo laini au ukandamizwaji wa maisha hata kama wakati mwingine hali ya ugonjwa haitabadilika. Katika uzoefu wa vikwazo na uwezekano wa kushindwa hata kwa madawa ya kisayansi, mbele ya kesi za kliniki daima zina matatizo na ugunduzi wa kesi hizo anabainisha Papa Francisko na kuongeza, madaktari wanaalikwa kujifungulia  ukuu wa Mungu ambaye anaweza kwa hakika kuwa msaada kamili wa taaluma yao: “Tukumbuke kuwa maisha ni matakatifu na ya Mungu, kwa maana hiyo hayawezi kukiukwa utu wake”( Rej Istr. Donum vitae, 5; Enc. Evangelium vitae, 29-53).

Maisha yote lazima yapokelewe, yalindwe, yaheshimiwe na hudumiwa

Maisha lazima yapokelewe, yalindwe, yaheshimiwe na kuhudumiwa tangu kuzaliwa hadi kufa kwake. Hii inatakiwa iwe sababu na imani katika Mungu muumba wa maisha. Katika kesi nyingine, Papa Francisko amebainisha kwamba: “kukataa kwao kwa dhamiri katika chaguo muhimu la kukaa thabiti ndiyo kwa ajili ya  maisha na mtu”. Katika hali nyingine taaluma yao, inayoongozwa na upendo wa kikristo, itakuwa bora katika huduma ya kweli, ya haki ya kibinadamu na ile ya maisha. Iwapo hawawezi kuponyesha, anawashauri kwamba wanaweza kutibu daima kwa njia ya matendo mema  na ambayo yanatoa utulivu na faraja kwa mgonjwa. Papa Francisko anabainisha kuwa, “Lakini kwa bahati mbaya katika baadhi ya mantiki ya vita na migogoro ya nguvu wanaolengwa zaidi ni wafanyakazi wa huduma ya afya na miundo ambayo inashughulikia mapokezi na msaada wa wagonjwa. Katika sehemu nyingine hata mamlaka ya kisiasa, yanajaribu kuingilia kati kwa kufanya madai ya uendeshaji wa  misaada ya matibabu kwa niaba yake, huku ikizuia uhuru wa kuendeleza  taaluma ya huduma ya afya. Kiukweli kushambulia wale ambao wanajikita katika kutoa huduma ya watu wanoteseka katika mwili wa kijamii haipendezwi na mtu yeyote. Amebainisha Papa Fancisko.

Mtazamo wa Papa kwa wasio na uwezo wa kupata matibabu

Katika siku ya XXVIII ya wagonjwa duniani, Papa Francisko anawakumbuka  kaka na dada ambao hawana uwezekano wa kupata matibabu, kwa sababu wanaishi katika umaskini. Kwa maana hiyo, anawakegeukia Taasisi za kitaifa  na serikali za nchi zote duniani, ili katika  kufikiria mantiki  ya  kiuchumi kwanza wasisahau haki ya kijamii. Ni matashi yake mema ya  kwamba hawa wanaweza kuunganisha misingi ya mshikamano na ushirikiano ili washirikiane  kwa sababu wote waweze kupata  tiba inayofaa kwa ajili ya kuwalinda na kurudishia afya zao. Papa Francisko anawashukuru kwa moyo wote, watu wote wa kujitolea na ambao wanajikita katika huduma ya wagonjwa, hasa kwenda katika hali nyingi ngumu na ambazo siyo mara chache zina upungufu wa miundo mbinu na kujikita kwa ishara ya huruma na ukaribu kwa mfano wa Kristo aliye Msamaria mwema. Kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria afya ya wagonjwa, Papa Francisko anamkabidhi watu wote ambao wamebeba uzito wa ugonjwa, pamoja na familia zao kama vile hata wahudumu wa afya. Na kwa kwa wote anawahakikishia ukaribu wake na kwa sala na kuwatumia baraka takatifu ya kitume.

03 January 2020, 12:05